Faiza Ally: Natamani kuhongwa, kwa sababu sijawahi kuhongwa hata siku moja

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Muigizaji na mrembo mwenye vituko kibao, Faiza Ally, amesema atafurahi sana endapo atampata mtu wa kumuhonga kwa sababu hajawahi kuhongwa hata siku moja.

Akizungumza kupitia kipindi cha Kubamba cha Times Fm, Bi dada huyo mwenye mtoto mmoja amedai ameanzia mbali kutafuta fedha na karibu kila kitu chake anajihudumia mwenyewe.

“Natamani nipate mtu wa kunihonga, coz mimi kila kitu najifanyia mwenyewe, hata biashara yangu nmeisimamisha mwenyewe nilishawahi hata kuuza mama ntilie” Alisema.

Katika hatua nyingine muigizaji huyo ambaye anategemea kuiingiza sokoni filamu yake mpya muda si mrefu, ameweka wazi kuwa amenunua gari ya ndoto yake aina ya Landrover.
faiza-A-559x520.jpg
 
Uchumi wa nchi umeyumba sana hadi wasanii wamekuwa cheap kiasi hiki.Hivi mheshimiwa sugu hakumhonga kweli?Au yeye sugu ndo alihongwa?
 
Siamini pamoja na uzuri wote huo hajawai kuongwa hata chips mayai au definition yake ya kuongwa ni tofauti na sisi tunayoijua?
 
Maisha magumu sasa kwa WASANII IKULU hakuna BIASHARA sasa waliokuwa wanafanya BIASHARA wamehama.MIMI mwenyewe enzi hizooo nilijifanya msanii wa kupiga tumba mbona nilikula bata ila sasa thubutuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu. ukiingia tu unaulizwa unalipa KODI .?
 
Wanaume ukiwarembea wanakunyongaa,hehe ukiona hakuhongii ombaaa
 
Do huyu dada ni pasua kichwa hata mheshimiwa ninadhani baada ya heshima ya baby mother angeweza kumkana huyu dada.
 
Muigizaji na mrembo mwenye vituko kibao, Faiza Ally, amesema atafurahi sana endapo atampata mtu wa kumuhonga kwa sababu hajawahi kuhongwa hata siku moja.

Akizungumza kupitia kipindi cha Kubamba cha Times Fm, Bi dada huyo mwenye mtoto mmoja amedai ameanzia mbali kutafuta fedha na karibu kila kitu chake anajihudumia mwenyewe.

“Natamani nipate mtu wa kunihonga, coz mimi kila kitu najifanyia mwenyewe, hata biashara yangu nmeisimamisha mwenyewe nilishawahi hata kuuza mama ntilie” Alisema.

Katika hatua nyingine muigizaji huyo ambaye anategemea kuiingiza sokoni filamu yake mpya muda si mrefu, ameweka wazi kuwa amenunua gari ya ndoto yake aina ya Landrover.
View attachment 354652
Bongo movie actresses are the biggest liars!!!I can bet on earth...they are not trusted at all like our politicians...!!!
So whoever trusts what this gal said ! Should get his medulla examined
 
Back
Top Bottom