Wengine pesa wanatafuta mchana na wengine usiku. Mtu kama haujamwajiri wala kumpangia kazi huwezi kujua muda wake wa kufanya kazi ni upi. Kama mtu biashara yake ni night club au Casino, unataka saa nne akafanye kazi gani muda huo? Au kama anamiliki Bar na hapo ndio ofisini kwake na Rais amesema wateja wasije kunywa pombe asubuhi maana ni muda wa kazi, unataka yeye aende wapi muda huo? Kama wakiamua kucheza 'pool', bao, karata, draft wakisubiria wateja waanze kuja saa 10 atakuwa amefanya kosa gani?