Fainali ipi ya 'UEFA Champions League' ilikuvutia kwa miaka 10 iliyopita?

Fainali nyingi zilikuwa hovyo hasa miaka ya karibuni zimekuwa upande mmoja sana.

Ni fainali mbili tu miaka kumi iliyopita unaweza sema ilikuwa 50/50 timu zote zilipambana hadi sekunde ya mwisho

Dortmund v Bayern 2013
Paris v Bayern 2020

Fainali mbovu kuliko zote ni Liverpool v Spurs, ilikiuwa hovyo kupita hata ile ya Milan v Juve mwaka 2003 pale old traffold
Uliingalia fainali ya man utd na chelsea???

Bonge moja la fainali 50/50 ilee
 
Hivi ndo kusema mtiti wa 2011/12 Bayern Munich Vs Chelsea mmeusahau? Au ni hasira zenu na chuki tu dhidi ya Chelsea?

Ngoma imeenda hadi 120 kwa header la kiroho mbaya lililotandikwa na mmatumbi, Robben ananoa penalti ndani ya extra time, watu wanahema vya hatari, game inaisha kwa mbinde la matuta, wanaume wamepambana hadi mwisho ndo bingwa anapatikana!

Mnatuletea habari za game ambazo mtu anakufa 4-1! Fainali unapigwa mabao manne? Imekuwa rede? Fainali tamu mchezee kwenye 1-0, 2-1, 3-2 mwisho, zaidi ya hapo ni NBA.

Mada yenyewe inasema within 10yrs, mnafosi kwenda hadi 1990's huko ili tu msiisifu hii burudani

Semeni kiliumana!!!!
 
Binafsi fainali timu ikifungwa zaidi ya goli mbili naona sio fainali nzuri
 
UEFA 2018/2019 ilikuwa bora sana kwangu. Kuingiza timu zote za premier league
fainali kimiujiza ujiza kwangu ndo iliishia pale. Kwenye fainali nikasema liwalo na liwe na sikutegemea kuona maajabu yoyote.
 
Back
Top Bottom