Faida za ulaji wa tende katika miili yetu

Faida za ulaji wa tende katika miili yetu

ChikoTz

Member
Joined
Feb 26, 2019
Posts
37
Reaction score
33
Kila wakati unashauriwa na watalam wa afya ya kwamba unatakiwa kula tende kwa wingi ili kupata faida zifuatazo katika mwili wako:

1. Huongeza nguvu kutokana na kuwa na sukari ya asili, unaweza kuchanganya na maziwa na kupata mchanganyiko bora!

2. Huzuia meno kuoza, na ni tiba nzuri kwa wagonjwa wa anemia kutokana na kuwa na madini mengi ya chuma.

3. Hupunguza uwezekano wa kupata Kiharusi (stroke) kwani hazina cholesterol kabisa! Pia zina vitamini na madini kwa wingi.

4. Huongeza uwezo wa Kujamiiana kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha nguvu

5. Hupunguza madhara ya pombe mwilini na kurudisha afya ya mtu.

6. Zina kiasi kikubwa cha kamba kamba ambazo hufanya mtu apate choo kirahisi na laini.

7. Licha ya kuwa tamu, tende haziongezi kiwango cha sukari mwilini, hivyo zinaweza kutumika kama mbadala wa sukari

8. Huimarisha Mifupa na kuondoa maumivu ya mara kwa mara ya mifupa kutokana na kuwa na madini ya chuma na potassium kwa wingi.

9. Tende ina msaada mkubwa kwa mama mjamzito, humuongeza nguvu, na hazina madhara kiafya kwa mtoto. Pia husaidia kupata uzazi salama

10. Ulaji wa tende kwa wingi husaidia kuongeza mwili kwa wale waliokonda kupita kiasi. Hivyo hushauriwi kula tende kupita kiasi kama huhitaji kuongeza mwili.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hiko ki`blog cha nini wakati ushatuambia faida za tende?lengo lako ni kutupa faida za tende au una mipango yako mingine?
unazingua mkuu!
 
Kila wakati unashauriwa na watalam wa afya ya kwamba unatakiwa kula tende kwa wingi ili kupata faida zifuatazo katika mwili wako:

1. Huongeza nguvu kutokana na kuwa na sukari ya asili, unaweza kuchanganya na maziwa na kupata mchanganyiko bora!...
Mafarao walitumia Tende kama Dawa na Makokwa yake pia walitumia katika kupambana na Uchawi.
 
... mbona hizo faida hatuzioni kwa waarabu wanaoshindia tende kila siku na hata kuzigeuza kama sehemu ya ibada? Unataka kutuaminisha kwamba mataifa mengine wana afya dhoofu kuliko waarabu kisa hawali tende kama Arabs wa uarabuni? Kila chenye faida hakikosi khasara, ungetuwekea na madhara ya tende ungeonekana mwungwana zaidi.
 
Kitambo tu hicho ndiyo kifungua kinywa changu,Tende na maziwa nkikija kula tena ujuwe ni baadae sana.
 
... mbona hizo faida hatuzioni kwa waarabu wanaoshindia tende kila siku na hata kuzigeuza kama sehemu ya ibada? Unataka kutuaminisha kwamba mataifa mengine wana afya dhoofu kuliko waarabu kisa hawali tende kama Arabs wa uarabuni? Kila chenye faida hakikosi khasara, ungetuwekea na madhara ya tende ungeonekana mwungwana zaidi.
Mkuu mbona hivyo au hujamwelewa mtoa mada.

Mtoa mada kaelezea leo faida za tende.haina maana kwamba nchi zenye walimaji wa tende wanapata faida zote hizo.

Kama ilivyo tanzania kuna rasilimali nyingi lakini haina maana kwamba asilimia kubwa wanapata faida ya rasilimali hizo.

Kwa hivyo faida za tende ambazo zimetajawa na hulimwa sana arabuni kuliko nchi zingine basi huwenda hizo nchi zingine zina matunda ambayo yana faida kama zile za tende.hivyo kama nchi hii inapata faida ya nguvu kwa kuwa wanavuna tende basi na nchi zingine zitapata faida za kuwa na nguvu kupitia tunda lingine.
Hivyo faida ile ile inapatikana katika matunda tofauti na watu tofauti.

Hivyo kutokuonekana kwa faida za tende kwa waarabu haina maana ya kwamba eti tende hazina hizo faida,bali hizo faida zipo katika tende japokuwa hatuzioni kwa wavunaji wake.

Kwa hyo haina haja ya kukoment kimiheemkooooo
 
Tende zina faida nyingi wewe hujuwi faida zake ndio maana unazi dharau
Hazina faida yeyote unapoteza hela tu.
Tende zina faida nyingi faida moja muhimu ya tende ni kuongeza nguvu ya kiume na faida ingine ya tende mwanamke mwenye mimba akifisha mimba ya miezi 8 anatakiwa kula kila siku tende 8 awe anakula mpaka siku ya kujifunguwa. Atajifunguwa psipo na kupigwa kisu aka opereshenia kila tende kwahuo muda. Ukila Tende kilo moja ni sawa na mtu aliyekuwa nyama ya ng'ombe kilo moja faida zake.
 
Back
Top Bottom