Faida za ulaji wa mboga aina ya njegere

Faida za ulaji wa mboga aina ya njegere

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,303
Njegere ni mbona yenye virutubisho vingi vinavyofanya kazi ya kujenga mwili, kuboresha ufanyaji kazi wa ini na ni chanzo kizuri cha Protini.

Ulaji wa njegere mara kwa mara husaidia kuboresha kinga ya mwili, hurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu lakini pia huzuia mtu kuzeeka kwa haraka na zina kiwango kidogo cha kalori.

Njegere zina kiwango kikubwa cha nyuzinyuzi, vitamin A,B, na C na hazina mafuta yanayoweza kuganda katika mishipa ya damu.

Lakini pia zinauwezo wa kuzuia saratani ya tumbo. Protini iliyopo katika mboga hii husaidia kuyeyusha damu iliyoganda na kwa wagonjwa wenye upungufu wa damu, wanatakiwa kutumia njegere zilizochemshwa kila siku.

Ulaji wa njegere za kijani huongeza damu, hukabiliana na udhaifu wa afya lakini zinasaidia kupunguza maumivu katika kidonda kinachouma kwa sababu inasaidia kuondoa asid zilizopo tumboni.

Utafiti uliofanywa na mtaalamu wa tiba-lishe wa taasisi moja nchini Marekani, Dk.George Mateljan anasema, njegere ni miongoni mwa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha kamba lishe zenye uwezo wa kushusha kiwango cha lehemu inayosababisha shambulio la moyo.

Matokeo ya utafiti wake huo aliouandikia kitabu kiitwacho The World’s Healthiest Foods, Dk Mateljan anasema asilimia 65 ya mbegu ya njegere ni kamba lishe ambapo pamoja na kushusha lehemu, pia huondoa shinikizo ya damu na kuzuia shambulio la moyo. “Watu wengi wanakula kidogo sana, hawajui faida hizi.

Lakini ukweli ni kwamba njegere ni chakula muhimu mwilini hasa kwa wagonjwa wa moyo na sukari,” alisema Dk Mateljan na kuungwa mkono mtaalamu mwingine Dk Rafael Nyampiga wa jijini Dar es Salaam

Chanzo: Mwananchi
 
Asante sana. Hizi ndizo habari zenye tija.
 
Halafu uwe ubwabwa wa nazi upike na njegere za nazi
Kati ya vitu nisivyovipenda ni pamoja na nazi, chakula chochote kikiungwa nazi hakinibariki kabisa nafikiri ni kwa kuwa kule kwetu bariadi tulizoea samli.

Wahenga hawakukosea waliposema "mzoea nazi samli haiwezi"
 
Mi napenda sana nazi. Tanga tumezoea nazi
 
Njegere kwa kuleta vile vya "yusufuuuu"..... silent but deadly haijambo
 
Kati ya vitu nisivyovipenda ni pamoja na nazi, chakula chochote kikiungwa nazi hakinibariki kabisa nafikiri ni kwa kuwa kule kwetu bariadi tulizoea samli.

Wahenga hawakukosea waliposema "mzoea nazi samli haiwezi"
Mkuu umenikumbusha ubwabwa wa samli!! Daah, kale kaharufu kake ni balaa
 
Mke wangu siku nikimwambia ANIPIKIE NJEGERE MIXER KARANGA, jioni nikirudi ananiambia PERIOD imemuanza ghafla
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] Itakuwa hajui kupika japo anashindwa kukwambia.
 
Kati ya vitu nisivyovipenda ni pamoja na nazi, chakula chochote kikiungwa nazi hakinibariki kabisa nafikiri ni kwa kuwa kule kwetu bariadi tulizoea samli.

Wahenga hawakukosea waliposema "mzoea nazi samli haiwezi"
Walaji wa nazi twatumia samli kwenye kukandia unga wa chapati....si zaidi ya hapo...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom