Faida za Parachichi katika mwili wa Binadamu

avocado.jpg



FAIDA YA TUNDA LA PARACHICHI - PEA (AVOCADO)
Ndani ya tunda hili kuna maji kiasi kidogo sana ukilinganisha na matunda mengine lakini kuna mafuta mengi na unaweza kuchanganya kula na tunda lingine kama vile apple, ndizi, chungwa au hata maziwa kwa kutengeneza juisi.

TINDIKALI
Licha ya kuwa na mafuta parachichi lina tindikali (acid) mbalimbali ikiwemo inayojulikana kama amino ambayo husaidia sana kukinga na kutibu maradhi katika mwili wa binadamu. Tunda hili pia lina protini ya kiwango cha juu.
Pia kuna tindikali inayoitwa oleic acid kwenye parachichi ambayo husaidia kukinga magonjwa ya moyo, kiharusi na kansa.

VITAMINI “E” NA B6
Imeelezwa na wataalamu kuwa tunda hili lina kiwango kikubwa cha vitamini E kuliko ile inayopatikana kutoka kwenye mazao ya wanyama.Parachichi lina vitamini hiyo nyingi kuliko inayopatikana katika mayai ambayo yanasifika kwa kuwa na vitamini e, hivyo hii inathibitisha kuwa lina faida kubwa mwilini.

Licha ya vitamini E pia ndani ya parachichi kuna vitamini B6 na kuna madini ya chuma (Iron) kwa wingi na madini ya potassium, pamoja na vitamin B6 na E mlaji anaweza kuletawa nafuu sana kama alikuwa na matatizo ya stress, matatizo ya uzazi kama ugumba na jogoo kutopanda mtungi Nguvu za kiume pia tunda hili linasaidia (impotence) .

FAIDA ZA PARACHICHI
Licha ya binadamu kufaidika na virutubisho vya tunda hili kuna faida nyingi za parachichi kama vile majani ya mti wake pamoja na magamba, baadhi ya watu hutumia kutibu maradhi ya kuharisha.

Majani na magamba hayo hutibu pia tatizo la gesi tumboni, kutuliza kikohozi pamoja na matatizo ya ini na kusafisha njia ya mkojo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa wataalamu wa dawa za mitishamba, dawa hii haifai kutumiwa na wanawake ambao wana mimba kwani wakitumia inaweza kusababisha kuharibika kwa ujauzito.


HEDHI
Hata hivyo, wataalamu wa tiba mbadala wanasema dawa hiyo inaweza kuwasaidia sana wanawake ambao wameshindwa kuona siku zao kwa wakati, na wakitumia vyema wanaweza kuanza kuona siku zao.

Aidha, tunda
hili linasaidia uyeyushaji wa chakula tumboni hasa kwa wale wenye matatizo ya vidonda vya tumbo, kwani parachichi lina nyuzinyuzi “fiber” ambayo ni muhimu kukinga kuta za utumbo. Watu wenye maradhi ya anaemia, diabetes, matatizo ya mfumo wa neva, matatizo ya mishipa ya moyo hasa wa artery wanashauriwa kula tunda hili mara nyingi.

Lakini pia tunda hili limethibitishwa na wataalamu kuwa linapunguza kwa kiwango kikubwa cholesterol kutoka kwenye damu hasa kwa watu wanene.

Tunda hili husaidia kulainisha ngozi na kuondoa mikunjo, hung`arisha na kulainisha nywele na kuzisaidia kukua pia kuziimarisha na kuzuia kukatikakatika.

Parachichi unaweza kulila kwa kulimenya au kwa kulisaga na kutengeneza juisi na kama nilivyoeleza hapo juu unaweza kuchanganya na matunda mengine kama tulivyoyataja na hutaharibu virutubisho vilivyomo badala yake utaongeza ubora wa juisi yako.

Watoto wadogo pia unaweza kuwapa tunda hili na wakafaidika na haya tuliyoyaandika.
Parachichi pia huweza kutumika kama siagi kwa kupaka kwenye mkate au kuchanganya na wali.​

Haya wale wanaopenda ngozi zao za mwilini zisijikunje hata wakiwa watu wazima wadumu kula tunda hili kila siku katika maisha yao basi ngozi za mwili wao hazitajikunja hata usoni watakuwa kila siku vijana hata wakiwa wazee.

ukweli ni kwamba hili tunda linasaidia kwa mambo mengi. kwa kuongeza nguvu za kiume liko juu haswa
 
Dr.Masmarc wa nchini Urusi pamoja na madaktari bingwa kutoka nchini Brazil wakishirikiana na watafiti kutoka chuo cha Havard wamethibitisha kwamba watu wenye VVU wanaweza kuishi hadi miaka 50 na ugonjwa wa Ukimwi endapo tu watatilia mkazo unywaji wa juisi ya parachichi angalau lita 3 kwa siku.

Aidha katika ripoti hiyo iliyochapishwa kwenye jarida la
THE HEALTH FORUM imeripotiwa kuwa matumizi ya ARV hayafai kwa mwili wa binadamu kwa kuwa vidonde hivyo vina kemikali sana na nchi nyingi hasa kusini mwa jangwa la sahara ARV hazijaweza kusaidia wananchi wa kipato cha chini.
 
Dr.Masmarc wa nchini Urusi pamoja na madaktari bingwa kutoka nchini Brazil wakishirikiana na watafiti kutoka chuo cha Havard wamethibitisha kwamba watu wenye VVU wanaweza kuishi hadi miaka 50 na ugonjwa wa Ukimwi endapo tu watatilia mkazo unywaji wa juisi ya parachichi angalau lita 3 kwa siku.

Aidha katika ripoti hiyo iliyochapishwa kwenye jarida la
THE HEALTH FORUM imeripotiwa kuwa matumizi ya ARV hayafai kwa mwili wa binadamu kwa kuwa vidonde hivyo vina kemikali sana na nchi nyingi hasa kusini mwa jangwa la sahara ARV hazijaweza kusaidia wananchi wa kipato cha chini.

hoax! urusi/brazil????????????????? Science wameitoa wapi
 
Habarini wanajukwaa, kwa wale wenzangu ambao kidogo mmegusa Biology Huwa nikila parachichi hususani ninaposhushia na ubwabwa, nahisi hali ya msisimko wa mwili kuongezeka.

Nimefanyia majaribio kama mara tatu hivi Nimegundua nikila parachichi na wali kwa pamoja msisimko unakuwa mkubwa ajabu.

Naomba Darasa lenu parachichi linaongeza nguvu za kiume?
JE? WAZIJUA FAIDA ZA KUSHANGAZA ZA KUTUMIA ZA KUTUMIA UNGA WA MBEGU ZA PARACHICHI? SI WAKATI WA KUTUPA MBEGU ZA PARACHICHI TENA.
 
Kule kwetu upareni nilikua naona watu wananyang'anyana parachichi na mbwa ikidondoka toka mtini.
Mi spendi vitu visivyo na ladha kama parachichi na ugali pia,ukiulizwa ladha ya parachichi au ugali ni ipi utasemaje?
 
Parachichi la moshi nalikubali sana
Maparachichi ni mazuri haswaa nkipiga na wali au kande..muda mwingine pia sharubati yake ni ya ukweli nikiinywa najisikia poa sana
 
Back
Top Bottom