Faida za Mikoko katika Mazingira ya Viumbe Hai

Faida za Mikoko katika Mazingira ya Viumbe Hai

Ryan Holiday

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
3,491
Reaction score
5,934
MIKOKO
Mikoko ni aina ya miti ambayo inapatikana pembezoni mwa bahari ya hindi kuanzia pwani ya Mtwara mpaka Tanga na kuzunguka pwani ya Unguja, Pemba na Mafia katika nchi ya Tanzania. Mikoko ni miti yenye faida kubwa sana kwenye mazingira ya viumbe hai.

FAIDA ZA MIKOKO KATIKA MAZINGIRA YA VIUMBE HAI
  • Mikoko inasaidia kupunguza kasi ya mawimbi makubwa ya bahari ambayo yangeweza kufanya uharibifu katika maeneo ya pwani mwa bahari.
  • Mikoko pia utoa mazingira mazuri ya samaki kuzaliana na kukwepa kasi ya mawimbi makali.
  • Mikoko inauwezo wa kuifadhi hewa ya ukaa (carbondioxide) kutoka angani na kuzalisha oksijeni kupitia kitendo cha mmea kiitwacho "photosynthesis". Oksijeni inayozalishwa utumiwa na mwanadamu na viumbe hai wengine katika mfumo wa upumuaji .
  • Mikoko inachuja maji ya chumvi na kuondoa 90% ya chumvi inayopatikana katika maji ya bahari na kuingia kwenye mizizi yake
 
Back
Top Bottom