efn
Member
- Jul 1, 2016
- 45
- 33
PIA HAWA WANAHISA ZA KAWAIDA WANAPATA HAKI YA KUSHIRIKI VIKAO VYA WANAHISA NA KUPIGA KURA ILHAL PREFERED SHAREHOLDER HAWANA HAKI YA KUPIGA KURA KWENYE VIKAOORDINARY SHARE ni umiliki wa Share katika kampuni ambapo shareholders watapewa gawiwo lao baada ya preferential shareholders kupewa gawiwo(DIVIDEND) lao.
Wamiliki wa ordinary shares/common shares huwa wanapewa kipaumbele kidogo au cha chini sana katika kupewa gawiwo. Hii inamaanisha kwamba kampuni ikipata faida wanaoanza kupewa gawiwo ni wale wanaomiliki wa preference shares halafu wanafuatia hawa wamiliki wa ordinary shares endapo tu gawiwo litabakia.
Wamiliki wa shea za kawaida(ORDINARY SHARES) katika kampuni huwa hawa kiwango dhahiri cha gawiwo lao. Hawa gawiwo lao hutolewa kulingana na DIRECTORS watakavyo amua.
PREFERENCE SHARES -ni umiliki wa shares ambapo preferential shareholders anapewa kipaumbele cha kwanza katika kupewa gawiwo.Hawa preferential shareholders wanapata gawiwo pale tu kampuni inapopata faida.
Katika Preference shares, hapa wana kiwango dhahiri cha gawiwo lao(Specific Dividend Rate).