Faida za kumiliki hisa za Vodacom

Sudysoko

JF-Expert Member
Aug 19, 2015
449
180
FAIDA ZA KUMILIKI HISA ZA VODACOM

Ukitaka kununua hisa lazima ujiulize maswali ambayo utaweza kuridhika kwa kiwango cha kutosha kununua Hisa za Vodacom ni rahisi kwani kampuni yenye huduma bora na yenye ubununifu wa kiwango cha juu;

•M-Pesa;
Vodacom ni waanzilishi wa huduma ya kutuma hela kwa kutumia mtandao wa simu kupitia M-Pesa, huduma inayosaidia kutuma na kupokea hela kutoka kila pande ya nchi.

•M-Pawa;
Huduma ya kujiwekea akiba, na kuweza kukopa kwa njia rahisi bila kuwa na dhamana.

Biashara ya uwekezaji ndani ya Vodacom ni rahisi na inayoeleweka katika makundi mbalimbali ya Jamii.

Vodacom ina historia nzuri katika uendeshaji wake tangu ilipoanzishwa haijawa kubadili jina lake kama makampuni mengine yalivyofanya.

Kampuni ya Vodacom mipango yake ni mizuri kwa kipindi cha muda mrefu yenye kulenga kufikia makundi yote nchi nzima.

Menejimenti ya Vodacom imekuwa ikifanya kazi kwa uweledi na ufanisi kibiashara katika kutanua mipaka ya kutanua soko lake na kulinda wateja wake.

Kampuni ya Vodacom imekuwa na mahusiano mazuri na share holders wake.

Vodacom imekuwa ikijijengea faida kupitia wateja wake na biashara bora ya huduma yenye kuaminika tangu kuanzishwa kwake nchini.

Vodacom ni Mtandao ulioaminiwa zaidi na watanzania kwa miaka zaidi ya 17, na unaendelea kuaminiwa, Uaminifu kwa wateja umeifanya kuwa kampuni bora ya mawasiliano, Ubora huu unafanya kuwa sehemu salama ya uwekezaji wako.

Wekeza na Vodacom
Nunua Hisa za Vodacom
Vodacom Tanzania.

b216bece79cac927495cd91b50205af8.jpg
 
Vodacom tumbueni huyu marketing manager wenu hapo umemaliza kuainisha na kubainisha faida za ununuzi wa hisa vodacom?

Mbona umeacha maswali muhimu kama
Mpaka mwisho wa wiki hii hisa zimeuzwa na kununuliwa kwa shi ngapi?
Kwa trend ilivyo mtu akinunua labda tuseme hisa za milioni moja baada ya miezi sita au mwaka atatengeneza faida kiasi gani? N.k n.k

Mm nimeshawishika nataka kununua hisa kama mia mbili ivi
 
Ivi kwa Vodacom, wanauza kuanzia shares ngapi kwa iyo Tshs 850.
Alafu nataka kujua kwamba katika HISA unazonunua unakuwa unaweza kuzitumia kama Dhamana ya kuchukulia Mkopo kwy Taasisi za Kifedha na je? Kwa kiwango gani cha HISA ulizo nazo au thamani ya izo hisa, unapata mkopo wa asilimia ngapi?
 
Haya ndo angepaswa kueleza ili tujue faida za hisa
 
Vodacom tumbueni huyu marketing manager wenu hapo umemaliza kuainisha na kubainisha faida za ununuzi wa hisa vodacom?

Mbona umeacha maswali muhimu kama
Mpaka mwisho wa wiki hii hisa zimeuzwa na kununuliwa kwa shi ngapi?
Kwa trend ilivyo mtu akinunua labda tuseme hisa za milioni moja baada ya miezi sita au mwaka atatengeneza faida kiasi gani? N.k n.k
Ni kwel amepwaya sana katka kujieleza.Huenda kuna watakaochangia vzur zaid
 
kwanza mbona naskia mpesa itakua kampuni tofuti na vodacom mani ya kujihusisha na ela?
 
Ivi kwa Vodacom, wanauza kuanzia shares ngapi kwa iyo Tshs 850.
Alafu nataka kujua kwamba katika HISA unazonunua unakuwa unaweza kuzitumia kama Dhamana ya kuchukulia Mkopo kwy Taasisi za Kifedha na je? Kwa kiwango gani cha HISA ulizo nazo au thamani ya izo hisa, unapata mkopo wa asilimia ngapi?
hisa kuanzia 100
 
FAIDA ZA KUMILIKI HISA ZA VODACOM

Ukitaka kununua hisa lazima ujiulize maswali ambayo utaweza kuridhika kwa kiwango cha kutosha kununua Hisa za Vodacom ni rahisi kwani kampuni yenye huduma bora na yenye ubununifu wa kiwango cha juu;

•M-Pesa;
Vodacom ni waanzilishi wa huduma ya kutuma hela kwa kutumia mtandao wa simu kupitia M-Pesa, huduma inayosaidia kutuma na kupokea hela kutoka kila pande ya nchi.

•M-Pawa;
Huduma ya kujiwekea akiba, na kuweza kukopa kwa njia rahisi bila kuwa na dhamana.

Biashara ya uwekezaji ndani ya Vodacom ni rahisi na inayoeleweka katika makundi mbalimbali ya Jamii.

Vodacom ina historia nzuri katika uendeshaji wake tangu ilipoanzishwa haijawa kubadili jina lake kama makampuni mengine yalivyofanya.

Kampuni ya Vodacom mipango yake ni mizuri kwa kipindi cha muda mrefu yenye kulenga kufikia makundi yote nchi nzima.

Menejimenti ya Vodacom imekuwa ikifanya kazi kwa uweledi na ufanisi kibiashara katika kutanua mipaka ya kutanua soko lake na kulinda wateja wake.

Kampuni ya Vodacom imekuwa na mahusiano mazuri na share holders wake.

Vodacom imekuwa ikijijengea faida kupitia wateja wake na biashara bora ya huduma yenye kuaminika tangu kuanzishwa kwake nchini.

Vodacom ni Mtandao ulioaminiwa zaidi na watanzania kwa miaka zaidi ya 17, na unaendelea kuaminiwa, Uaminifu kwa wateja umeifanya kuwa kampuni bora ya mawasiliano, Ubora huu unafanya kuwa sehemu salama ya uwekezaji wako.

Wekeza na Vodacom
Nunua Hisa za Vodacom
Vodacom Tanzania.

b216bece79cac927495cd91b50205af8.jpg
umeshindwa kuanisha hizo faida..kwanini usingeliacha tuu?
Watu wanatakiwa kujua faida ikipatikana hugaiwa kulinganana na idadi ya hisa uzomiliki...mwenye hisa 1000 hawezi pata sawa na mwenye hisa 100.
Halafu kama kampuni ikipata hasara hakuna gawio bali wote mwaka huo mtakuwa mmepata hasara.....
Pia gawio hutolewa mwisho wa mwaka.....
 
Haya ndo angepaswa kueleza ili tujue faida za hisa
Ukiwa na share certificate,unapata mkopo kwenye taasisi za fedha,wala usiwe na wasiwasi.tatizo ninaloliona mm,dhaman ya hisa kwa sasa haikui kwa kasi,kama miaka ya nyuma.pia nimeangalia hisa za makampun mengine makubwa kama sigara,tbl,crdb,nmb,nk.naona sinashuka tu,badala ya kuongezeka,napata hofu kidogo hasa hiki kipindi cha serkal hii,kama nitapata faida.
 
Thamani,sio dhaman.
 
Sa

Asante kwa angalizo japo lipo indirectly
 
BANDUGU,BIASHARA YA HISA NI NZURI SANA KAMA WEW NI "RISK TAKER" MAANA KWAMBA HII NI BIASHARA YENYE CHANGAMOTO NYINGI SANA KWA MAANA KUA KUNA HISA ZA AINA TOFAUTI TOFAUT MFANO KUNA PREFERENCE SHARES NA ORDINARY SHARES.SASA KIKAWAIDA IKIWA KAMPUNI ITAPATA FAIDA BASI ATAKAYEANZA KULIPWA NI HUYU MWENYE PREFERENCE SHARES NA HATA KAMPENI IKIPATA HASA HUYU MWENYE PREFERENCE SHARES ATALIPWA KWA MAANA YA KUA MALIPO YAKE YAKO FIXED KULINGANA NA HISA ANAZOZIMILIKI LAKINI KWENYE UPANDE WA PILI WA HAWA WENYE ORDINARY SHARES,WAO WATAPATA GAWIO ENDAPO TU FAIDA ITABAKIA BAADA YA KUNDI LA PREFERENCE SHAREHOLDERS KUPATA MGAWO WAO NA KAMA KUNA HASARA BASI HAWA ORDINARY SHAREHOLDERS HAWATAPATA HATA SENTI KAMA GAWIO KWENYE HICHO KIPINDI HUSIKA.SASA VODACOM MNATAKIWA MUACHE MANENO MEEEEEEEEEEEENGI,TOENI ELIMU KWA KINA KUANZIA HASARA ZA HII BIASHARA NA FAIDA ZAKE BILA KUFICHA KITU CHOCHOTE ILI TU MUWAVUTIE WATU WANUNUE HISA ZENU NA NYIE KUPATA MTAJI MLIOKUSUDIA.KUMBUKEN WATAKAO NUNUA NI WATEJA WENU NA WENGI WAO WANASHAUKU YA KUNUNUA HISA KWA KUANGALIA UPANDE WA FAIDA TU BILA KUJUA UPANDE MWINGINE WA CHANGAMOTO ZA HII BIASHARA NA HIVYO KULETA MKANGANYIKO ENDAPO WANAHISA WAKIKOSA KILE WALICHOKITARAJIA(FAIDA).SAS ELIMU YENU INATAKIWA ILENGE
1. KUELIMISHA UMA JUU YA KUNDI LIPI LA HISA AMBALO NYIE MNAUZA(PREFERENCE SHARES,ORDINARY SHARES etc.)
2. CHANGAMOTO ZIPI(RISKS ASSOCIATED WITH THE BUSINESS) ZINATARAJIWA KUTOKEA KATIKA BIASHARA HUSIKA.
3. FAIDA AMBAZO MMILIKI WA HISA ZENU ANATARAJIA KUZIPATA MBALI NA GAWIO.
NA MASWAL MENGINE MENGI,NAAMIN MKIFANIKIWA KUTOA ELIMU HII BILA SHAKA SOKO LENU LITAKUA NA KUPANUKA MARADUFU ZAIDI YA SASA KWA SABABU MNA UTHUBUTU WA KUJA NA BIDHAA MPYA ILI MJITOFAUTISHE NA WASHINDANI WENU WA SASA HASA KATIKA BIASHARA YA DATA AMBAYO HIVI SASA IMEONGEZEKA MATUMIZ YAKE KUTOKANA NA UPATIKANAJI WA TECHNOLOGICAL DEVICES KAMA SMARTPHONES KWA URAHIS NA KWA BEI RAFIKI KWA WATANZANIA WENGI.
 
umeshindwa kuanisha hizo faida..kwanini usingeliacha tuu?
Watu wanatakiwa kujua faida ikipatikana hugaiwa kulinganana na idadi ya hisa uzomiliki...mwenye hisa 1000 hawezi pata sawa na mwenye hisa 100.
Halafu kama kampuni ikipata hasara hakuna gawio bali wote mwaka huo mtakuwa mmepata hasara.....
Pia gawio hutolewa mwisho wa mwaka.....
Alafu kama kampuni imepata hasara wanatoa katika HISA zilizopo au inakuwaje.
Mfano:-
Wamepata hasara ya 10% ya izo 100 HISA kwa Tshs 850.
HISA 100x850=Tshs 85,000
10%x100x850=Tshs 8,500
Kwa iyo apo Ukitoa zinakuwa na thamani ya Tshs (85,000-8,500) =Tshs 76,500
 
MKUU HIO 10% SIO HASARA KWA KAMPUNI,HIO NI BEI YA HISA KATIKA SOKO LA HISA MAANA HUA INAPANDA NA PIA HUA INASHUKA BEI KWA MAANA KUA UNAWEZA KUNUNUA HIZO HISA 100 LEO KWA (100 × 850 = 85,000/=)LAKINI BAADA YA MUDA FULANI BEI YA HISA SOKONI IKAPANDA HADI KUFIKIA 900 MAANA YAKE HAPA UKIUZA HISA ZAKO WEW UTAPATA FAIDA YA TSHS 50 KWA KILA HISA ILA PIA BEI YA HISA INAWEZA KUPUNGUA LABDA IKAWA 800 KWA HISA MAANA YAKE NI KUA UKIUZA HISA ZAKO KIPINDI HIKI UTAPATA HASARA YA TSHS.50 KWA HISA SASA HAYA MABADILIKO YA BEI YA HISA HAYAATHIRI GAWIO LAKO MWISHO WA MWAKA...GAWIO LAKO LITAASHIRIWA NA VARIABLES MBILI TU
1.FAIDA AU HASARA KATIKA BIASHARA ZA KAMPUNI AMBAZO ZITAASHIRI MAPATO YA KAMPUNI
2. AINA YA HISA UNAZOMILIKI.
SASA HAPA KWA MFANO MAPATO YA KAMPUNI BAADA YA KUFANYA BIASHARA KWA MWAKA MZIMA YAKIWA MADOGO KULIKO MATUMIZI MAANA YAKE KAMPUNI ITAKUA IMEPATA HASARA SASA KWENYE HALI HII WENYE HISA ZA AINA FULANI(PRERERENCE SHARES) WAO HAWATAATHIRIKA NA HASARA HII MAANA WAO GAWIO LAO LIKO FIXED KAMA SEHEMU YA EXPENSES ZA KAMPUNI YAN WAO WATAPATA GAWIO KAMA MTU ANAVYOPOKEA MSHAHARA VILE LAKINI WALE WENYE ORDINARY SHARES KWA SABABU KAMPUNI IMEPATA HASARA BASI HAWATAPATA GAWIO.
 
Hizi Hisa Vodacom mbona wanatangaza wenyewe tu au kampuni zingine za simu bado kutangaza!?
Nami nitaenda kuwekeza na Vodacom hakuna namna kamata fursa twenzetu.
 
Mbali na kuzungumzia suala la hisa leo, wajasiriamali wanashauriwa kusoma baadhi ya vitabu ambavyo waandishi wameandika mada mbalimbali za ujasiriamali ikiwamo uwekezaji katika hisa.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 84 ya Watanzania wakiwamo wasomi na wengine ambao hawajabahatika kusoma hawajui au hawana elimu kuhusu kuwekeza katika hisa.

Hali hiyo inatokana na ukweli kwamba mada hii haijawekwa katika mitaala mbalimbali ya elimu. Kama ipo basi wale wanaostahili kuifundisha ama hawana uelewa mpana na uzoefu wa kuwawezesha wanafunzi wao kufahamu umuhimu wake katika medani za kiuchumi.

Hisa inaelezeka kwa namna mbalimbali, kwa ujumla wake hisa ni mali, rasilimali, kitegauchumi, hati miliki, biashara, dhamana ya mkopo, ni akiba, ni fedha iliyohifadhiwa, na ni mtaji.

Katika mtazamo wa kibiashara, hisa ni uwekezaji wa mtaji au fedha ambayo imewekezwa na mfanyakazi, mkulima, mfanyabiashara au mtu mwingine ambaye ameamua kununua hisa kutoka katika kampuni fulani kwa lengo la kupata faida kupitia gawio na ongezeko la bei ya hisa husika.

Uwekezaji katika hisa kama biashara nyingine unahitaji umakini na upembuzi yakinifu. Kufanya upembuzi wa wapi uwekeze fedha zako na wapi ununue hisa kwa msingi wa kupata faida.

Mjasiriamali au watu wengine wanaweza kufanya upembuzi yakinifu, lakini kama watu makundi niliyoyataja hapo juu wana uelewa wa kutosha na mbinu za kusoma taarifa mbalimbali za kampuni ambayo unakusudia kununua hisa. Kwa mfano, unapaswa kufanya upepenuzi yakinifu wa taarifa za fedha na hali halisi ya kampuni husika.

Uwekezaji katika hisa unachangamoto zake ikiwzmo kushuka kwa bei ya hisa, kukosa gawio, mfumuko wa bei, viwango vya riba, kukosa wanunuzi kutokana na ukwasi na hitilafu mbalimbali.

Kwa hali ya kawaida uwekezaji katika hisa una faida nyingi kuliko changamoto kwa mfano, kupata gawio baada ya kampuni kutengeneza faida, ongezeko la thamani ya hisa, punguzo la kodi ya zuio kwenye gawio.

Katika masuala ya hisa, hakuna kodi kwenye ongezeko la thamani, urahisi wa kuuza na kununua hisa, na ukiwekeza katika hisa unapata muda wa kufanya shughuli nyingine. Kwa upande mwingine hisa ni dhamana ya kupata mkopo, hisa ni urithi mzuri, ukijiwekea utaratibu wa kutenga asilimia fulani ya pato lako kutoka kwenye mshahara ama biashara kwa ajili ya kununua hisa ni uamuzi mzuri, na hisa pia ni utajiri.

Nawashauri na kuwakaribisha kuwekeza na Vodacom
Tembelea ofisi za Vodacom kwa Maelezo zaidi.
[HASHTAG]#WekezaNaVodacom[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Tanzania[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom