Ngamanya Kitangalala
JF-Expert Member
- Sep 24, 2012
- 501
- 1,214
Tangu kuanza kwa mchakato wa kampeni za uchaguzi mkuu wa October mwaka huu, nimepata bahati ya kufuatilia kampeni za baadhi ya wagombea wetu wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Kwa bahati mbaya kwenye baadhi ya mikutano ya kampeni ya baadhi ya wagombea, Kumekuwepo upotoshwaji mkubwa kuhusu ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa katika mkoa wa Geita, unaoendelea kujengwa katika wilaya ya Chato.
Binafsi naamini sisi kama watanzania tunawajibu mkubwa wa kupima na kutafakari kwa umakini mkubwa tuhuma mbalimbali zitolewazo na baadhi ya wagombea dhidi ya wagombea wengine katika mikutano mbalimbali ya kampeni inayoendelea kwenye maeneo kadhaa hapa nchini.
Nadhani ipo haja ya sisi Watanzania, kuelewa umuhimu na faida za kiuchumi ( Economics Benefits) kwa uwanja wa ndege wa kimataifa Chato.
Kwanini uwanja wa ndege Chato?
Ukisoma ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2015- 2020 , ilieleza umuhimu wa serikali kuchukua hatua za makusudi katika kukuza na kuendeleza sekta ya utalii nchini,ili ifikapo mwaka 2020, Tanzania iwe na uwezo wa kupokea watalii wasiopungua 2,000,000 kwa mwaka toka watalii 1,200,000 ilivyokuwa mwaka 2014,hasa ukizingatia kuwa kwa mujibu wa ripoti ya World Economic Forum ( WEF) iliyotolewa mwala 2014,ilionyesha Tanzania ni nchi ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya asili vya utalii baada ya Brazil.
Japokuwa kwenye ripoti nyingine ya 2019 kutoka World Economic forum ambayo utolewa kila baada ya miaka 5, imeonyesha Tanzania inashika nafasi ya 12 duniani na ya 1 kwa Afrika kwa kuwa na vivutio vingi vya asili vya utalii(Tumeshuka kwa nafasi 10)
Lakini pia ukisoma ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ya 2020-2025, latika ukurasa wa 111, imeeleza lengo la serikali la kutaka kukuza sekta ya utalii, na kufikia kupokea watalii 5,000,000 kwa mwaka, ifikapo mwaka 2025, na kuongeza mapato ya utalii kutoka dola za kimarelani 2.6 billion mwaka 2020 hadi kufikia dola za kimarekani 6.0 bilionimwaka 2025
Na ni kwa nini utalii?
Sekta ya utalii Tanzania,ni moja ya sekta muhimu kabisa katika uchumi wa nchi yetu, kwani sekta hiyo ndio inayoongoza katika kuingiza fedha nyingi za kigeni kuliko sekta nyingine yeyote ile hapa Tanzania,Asilimia 25 ya fedha zote za kigeni( foreign currency) zinatokana na sekta ya utalii, Kwa mfano katika mwaka wa fedha wa 2018/ 2019 sekta ya utalii, iliingizia taifa takribani dola za kimarekani 2.4 bilioni( Tsh trilioni 5.2) pia katika mwaka wa fedha wa 2019/2020 sekta ya utalii pekee, iliingiza takribani dola za kimarekani 2.6 billion ( Tsh trilioni 5.4 )
Lakini ukiangalia jumla ya thamani ya shughuli zote za kiuchumi hapa nchini, kwa maana ya pato ghafi la taifa( Gross Domestic product ), sekta ya utalii inachangia 17.6%, ya GDP
Lakini pia sekta ya utalii imetoa ajira za moja kwa moja takribani watu 6000 na ajira zisizo za moja kwa moja takribani watu 2,000,000
Sasa kwa Tanzania, ukanda pekee unaofanya vizuri katika utalii ni ukanda wa Kaskazini, ambapo unaopokea watalii wengi kuliko kanda zingine za utalii,kama, kanda za Kusini na Kanda ya Kaskazini magharibi, takribani 90% ya watalii wote wanaoingia hapa nchini wanaelekea ukanda wa Kaskazin
Sasa ili kufikia malengo ya kuongeza idadi ya watalii, serikali waliamua kufungua baadhi ya kanda zingine za utalii, kanda hizo ni Kanda ya Kusini( mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe,Songwe) ambapo Kitulo ilipandishwa hadhi na kuwa hifadhi ya Kitulo, na kanda ya Kaskazini magharibi yenye mikoa ya ( Geita, Mwanza, Kagera, Kigoma)
Serikali walifanya nini kwa kanda ya Kaskazini magharibi?
Hatua ya kwanza waliofanya, ilikuwa ni kuyapandisha hadhi mapori tengefu ya Burigi, Biharamulo, Kimisi ,Ibanda, Rumanyika & Kyerwa na kuwa hifadhi za taifa( National parks)
1. Burigi- Chato National Park
2. Ibanda-Kyerwa National Park
3. Rumanyika-Karagwe National Park
Sasa ili kuweza kuvutia watalii waweze kufika Kwa urahisi zaidi katika hifadhi hizo, serikali waliona ipo haja ya kujenga uwanja mkubwa wa kinataifa wa ndege ulio karibu na maeneo hayo, ambapo watalii wataweza kufika kwa urahisi zaidi kuliko ilivyo sasa, ambapo kimsingi kunapatikana hifadhi ya tatu kwa ukubwa hapa Tanzania, hifadhi ya Burigi- Chato yenye ukubwa wa kilometa za mraba 4,702, ikitanguliwa na hifadhi za Serengeti na Sellou
Kwa hiyo kwa kuzingatia umuhimu wa kukuza sekta ya utalii nchini, ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Chato una manufaa makubwa sana katika kukuza uchumi wetu
Ngamanya Kitangalala Mwaswala
kngamanya@yahoo.com