Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,002
- 5,534
Kitindamlo au dessert ni chakula kinacholiwa mwishoni mwa mlo. Mara nyingi huwa ni chakula chepesi na chenye sukari kama matunda.
Binafsi, napenda sana sukari na siku nikiamua kupika lazima kuwe na dessert mezani. Lakini si kwa mapenzi tu, pia najua faida za kitindamlo.
Faida za Kitindamlo:
1. Ni njia nzuri ya kujumuisha matunda kwenye mlo wako
Matunda ni dessert nzuri sana na kwa wavivu wa kula matunda, kuandaa dessert ya matunda inasaidia. Unapata nutrients zako za kutosha.
2. Inasaidia kwa wanaofanya 'diet'
Unapofanya diet unapata hamu sana ya kula vitu vya sukari kama icecream na keki, usipoangalia unaweza kukatisha diet. Unapovifanya hivi kuwa dessert yako na kula kwa kiasi kidogo, unasaidia kukata cravings na kuhakikisha unafuatisha diet yako ipasavyo.
3. Huongeza furaha
Kitindamlo ndio muda wa wewe kula ukipendacho. Vitindamlo kwakweli huwa vitamu na hukupa furaha. Kila siku ukiweka kitindamlo kwenye hata moja ya milo yako, una uhakika wa kulala happy.
Kuna vitindamlo vya aina mbalimbali. Unaweza ukapika mwenyewe au ukanunua. Naomba next tym kisikosekane mezani kwako.