Faida ya TBL imeshuka mwaka 2018

Faida ya TBL imeshuka mwaka 2018

tatum

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2018
Posts
5,786
Reaction score
4,494
DoBER5AX0AQ6JCM.jpg

Faida ya Kampuni ya Bia #Tanzania (TBL) katika nusu ya kwanza ya mwaka 2018 imeshuka kwa asilimia 16 hadi TZS bilioni 64.5 kutoka TZS bilioni 77.13 katika kipindi kama hicho mwaka jana. Kushuka huko kumechangiwa na kuzuiwa kwa pombe za viroba, na mazingira magumu ya biashara.

Hizo sababu zilizotajwa hapo juu ndiyo hizo kweli au kuna sababu zingine?
 
Ni upepo tu wa biashara (boom, recession, depression, recovery),
Kutokana na muda wa kunywa bia kubadilika (saa 16:00 - 23:00) wanywaji wengi nao wamebadili tabia na maeneo ya kunyweaa...ni baa chache zimeendelea kuwa na wateja wengi hasa zile zenye WAHUDUMU MAKINI na WAWAJIBIKAJI.... nyinginezo zimebadilika matumizi na kuwa kumbi za ibada na BETTING rooms
 
Vipi kuhusu mishahara imepunguzwa au wafanyakazi ndio wamepunguzwa?
Maana makampuni hupenda ku~maximize profit na sio vinginevyo.
 
View attachment 879265
Faida ya Kampuni ya Bia #Tanzania (TBL) katika nusu ya kwanza ya mwaka 2018 imeshuka kwa asilimia 16 hadi TZS bilioni 64.5 kutoka TZS bilioni 77.13 katika kipindi kama hicho mwaka jana. Kushuka huko kumechangiwa na kuzuiwa kwa pombe za viroba, na mazingira magumu ya biashara.

Hizo sababu zilizotajwa hapo juu ndiyo hizo kweli au kuna sababu zingine?
jamani mbona mnatuchanganya kipindi jiwe alipokutana na wafanya biashara nadhani mwezi wa nne mwaka huu akasema ameongea na mtendaji mkuu wa tbl kuwa toka wamefungua kiwanda cha bia Tz miakaa hiyo hakuna miaka ambayo mauzo yao yamepanda kama kipindi hiki cha miaka mitatu!!!watu tuna bisha tukasema haiwezekani kwani hali halisi ya unywaji wa bia mtaani tunauona,nyumbu wakaja juu!!hivi huwa wanasema uongo ili iweje lakini??uchumi ni namba
 
Huku Mwanza bia zao zile ndogo ndogo zimepanda bei kutoka Tshs1,500/= sasa ni Tshs.1.700/= kwa chupa moja😡😡😡😡😡😡
 
Huku kaskazini Eagle buku buku tu ni mwendo huo na banana hakuna muda maalum gambe kuanzia kokoriko hadi muda wa mavyura kuamka.
 
Wakianza kutengeneza beer zile za Kilimanjaro kubwa zenye TASTES MURUA tutarudi tena,sio haya matakataka wanayotengeneza sasa.
Nimekuelewa Sana, Kilimanjaro ndogo ikoje asee nainywa tu nikiwa na arosto ila haivutiii km ile kubwa ya zamani
 
Back
Top Bottom