Faida ya samaki (fish) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Faida ya samaki (fish)

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Jun 15, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  SAMAKI (FISH)

  • Huyayusha damu, huifanya kuwa nyepesi
  • Huilinda mishipa ya damu isiharibike
  • Huzuia damu kuganda
  • Hushusha shinikizo la damu
  • Hupunguza hatari ya kupatwa na mshituko wa moyo na kiharusi
  • Hutuoa ahueni kwa wenye ugonjwa wa kipandauso
  • Husaidia kuzuia uvumbe mwilini
  • Huendesha mfumo wa kinga ya mwili
  • Huzuia saratani
  • Hutoa ahueni kwa wenye pumu
  • Hupambana na dalili za awali za ugonjwa wa figo
  • Huongeza nishati ya ubongo
  KITUNGUU SAUMU (GARLIC)
  • Hupambana na maambukizi
  • Ina kemikali zenye uwezo wa kudhibiti saratani
  • Hufanya damu kuwa nyepesi
  • Hupunguza shinikizo la damu na kolestro
  • Huamsha mfumo wa kinga ya mwili
  • Huzuia na kutoa ahueni kwa kikohozi kilaini.
  • Huweza kutumika kama dawa ya kifua
  TANGAWIZI (GINGER)
  • Huzuia ugonjwa wa kutetemeka
  • Hufanya damu kuwa nyepesi
  ZABIBU (GRAPE)
  • Ina uwezo wa kufanya virusi visifanyekazi
  • Huzuia meno kuoza
  • Ina mchanganyiko wenye uwezo wa kuzuia saratani
  PILIPILI HOHO (GREEN CHILLIES)
  • Dawa nzuri ya mapafu
  • Hutumika kama dawa ya kifua
  • Huzuia na kuponya kikohozi kikali
  • Husaidia kuyeyusha mabonge ya damu
  • Hutoa maumivu
  • Huweza kumfanya mtu kuwa na furaha
  ASALI (HONEY)
  • Huua vijidudu (bacteria)
  • Huondoa wadudu kwenye vidonda na malengelenge
  • Huondoa dalili za maumivu
  • Hutoa ahueni kwa wagonjwa wa pumu
  • Hutuliza maumivu ya vidonda vya koo
  • Hutuliza mishipa ya damu, humpatia mtu usingizi
  • Hutoa ahueni kwa mtu anayeharisha
  MAZIWA (MILK)
  • Huzuia ugonjwa wa mifupa (osteoporosis)
  • Hupambana na maambukizi, hasa kuharisha
  • Hurekebisha kuchafuka kwa tumbo
  • Huzuia vidonda vya tumbo
  • Huzuia kuoza kwa meno
  • Huzuia mtu kupatwa na kikohozi
  • Huongeza nishati ya ubongo
  • Hushusha shinikizo la damu
  • Hushusha kiwango cha kolestro mwilini
  • Hudhibiti baadhi ya saratani
  UYOGA (MUSHROOM)
  • Hufanya damu kuwa nyepesi
  • Huzuia saratani
  • Hushusha kiwango cha kolestro
  • Huchangamsha mfumo wa kinga ya mwili
  • Hudhoofisha virusi
  SHAYIRI (OATS)
  • Dawa bora ya moyo
  • Hushusha kolestro mwilini
  • Hurekebisha sukari kwenye damu
  • Ina mchanganyiko wa virutubisho unaodhibiti saratani
  • Hupambana na kuvimba kwa ngozi
  • Ina uwezo sawa na dawa ya kumpatia mtu choo
  KITUNGUU MAJI (ONION)
  • Dawa kubwa ya magonjwa ya moyo
  • Huimarisha kolestro nzuri (HDL)
  • Huifanya damu kuwa nyepesi
  • Hushusha kiwango cha kolestro mbaya
  • Huzuia damu kuganda
  • Hurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu
  • Huua vijidudu
  • Huzuia saratani
   
 2. J

  JituParaTupu Member

  #2
  Jun 15, 2009
  Joined: Nov 20, 2008
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Mkuu,

  Kwa vile ambavyo ni lazima vipikwe ungetueleza na mapishi yake.
   
 3. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  MziziMkavu,
  Asante kwa dondoo nzuri za kuboreshsa afya zetu.
   
 4. Robweme

  Robweme Senior Member

  #4
  Jun 15, 2009
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 178
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jituparatu,
  Mapishi ya samaki ni yaleyale, ya kila siku we hujui kupika samaki au?.
  Nadhani kwa kumsaidia Dr.Ni vizuri samaki akapikwa katika hari ya kuto haribu viungo yake vya asili.Nina maana kuwa samaki akichemshwa kawaida kwa kitunguu na nyanya na akaliwa kama mchemzo inakuwa nzuri kuliko yule wa kukaanga na mafuta yetu mengine yasio na TBS.
  Siyo Daktari lakini nadhani mapishi mazuri ni yale ambayo unaweza ku manage kwa kutumia vitu asilia, au mafuta ya asili.
  Asante.
   
 5. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2009
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,806
  Likes Received: 1,053
  Trophy Points: 280
  vinatumiwaje? kupika au kutafuna?
   
 6. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...unaposema samaki, unazungumzia samaki wabichi tu ama hata wale ambao wamekaushwa na kukauka kama ubao??
   
Loading...