Faida ya kujitibu kutokana na kitunguumaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Faida ya kujitibu kutokana na kitunguumaji

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Aug 12, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Faida ya kujitibu kutokana na kitunguumaji

  tiba inayopatikana katika Kitunguumaji

  Kitunguumaji ni aina ya mboga ya yungiyungi. Ni mboga yenye harufu kali inayochangamsha. Anaeikitumia kitunguu maji ajihadhari kukitumia baada ya kukihifadhi kikiwa kimekatwakatwa, kwasababu hufanya oksaidi (oxide) na huwa kiini chenye sumu. Kwa hivyo yatakiwa kitumiwe kikiwa fresh.

  Imethibitiswa kisayansi kuwa juisi yake huuwa vijidudu vya kinamasi na vya kifua-kikuu, huuwa baada tu ya kunusa moshi wake.

  Nchi mashuhuri duniani katika upandaji wa kitunguumaji ni Misri (Egypt). Razi amesema: "Kitunguu maji kikifanyiwa achari, ukali wake hupungua na hutia nguvu maida, na kitunguu kilichofanywa achari, hufungua mno hamu ya kula" Kwa ajili hiyo watu wa misri hula ktunguumaji kikiwa kimechomwa, hutia nguvu mwilini, huufanya uso kuwa mwekundu na huimarisha misuli.

  Ibn Baitar amesema: " Kitunguu maji hufungua hamu ya kula, hulainisha tumbo. Kikipikwa hukojoza na huzidisha nguvu za kiume kikichemshwa. Na kinachokata harufu ya kitunguumaji ni lozi (almond).

  Al-Antaky amesema kuhusu kitunguu maji: "Hufungua vizuizi mwilini, hutia nguvu za shahawa kwa mwanamke na mwanaume mbili (ya kula na na kujamii) hasa kikipikwa kwa nyama, pia huondoa homa manjano (jaundice) hukojoza na kumimina hedhi pamoja na kuvunja vijiwe tumboni".

  Katika gazeti moja huko Ufaransa liitwalo "Everything" (Kila kitu) limeelezea kuwa daktari mmoja aliwatibu wagonjwa kwa kuwapiga sindano (ya kitunguumaji) wagonjwa wengi waliokuwa na saratani (cancer) na akapata matokea mazuri.

  Viini vyenye athari nzuri katika kitunguu maji ni Vitamin C (antiseptic) inayozuia kukua kwa bakteria (bacteria) kwenye jeraha, ngozi n.k pia hutia nishati homoni (hormones) wa nguvu za kiume, kiini cha insulini (insuline, itumikayo kutibu wagonjwa wa kisukari). Kwa hivyo kitunguu maji ni katika dawa yenye kuwatibu wagonjwa wa kisukari, ndani yake mnapatikana salfa, chuma na vitamini zinazotia nguvu mishipa. Vilevile hupatikana viini vyenye kukojoza, kutoa safura na vyenye kutia nishati moyo pamoja na mzunguko wa damu mwilini.

  Pia imethibitishwa kuwa katika kitunguu maji muna vijiuasumu vyenye nguvu zaidi kuliko penesilini (penicillin) kwahivyo hupoza kifua kikuu, kaswende (syphillis) na kisonono (gonorrhea), na huua aina ya vijidudu vingi vya hatari.

  Pamoja na kuwa tunaamini kuwa maisha ya mwanaadam yote yamo katika mikono ya Allah S.W, lakini imethibitishwa kuwa wale watumiaji wa vitunguu maji zaidi huwa na umri mrefu pia huepukana na maradhi ya saratani na kifua kikuu. Mwandishi wa kitabu cha tiba zinazotokana na kitunguu maji yeye amekiita kitunguu maji ni " mpira wa dhahabu" kwakuwa ndani yake muna manufaa mengi yenye utajiri wa afya. Kutakasika ni kwa Allah mwenye kuneemesha peke yake.


  MARADHI YANAYOTIBIWA NA KITUNGUUMAJI


  Pumu:
  Changanya juisi ya kitunguu maji na asali halafu kunywa kiasi cha kikombe kimoja, asubuhi na jioni. Endelea hivyo kwa muda wa mwezi mmoja.

  Uvimbe wa pafu (Pneumonia):
  Weka kibandiko cha kitunguu maji juu ya kifua na mgongo pamoja na kufunga kwa kitambaa, fanya hivyo kila siku kabla ya kulala.

  Maradhi ya kinafsi:
  Chemsha kitunguu na maganda yake, baadae mgonjwa wa kinafsi ale, au chukua juisi ya kitunguu maji na juisi ya saladi (lettuce) na kijiko kimoja cha asali changanya vyote ndani ya blenda na baadae unywe.

  Saratani (Cancer):
  Kausha maganda ya kitunguumaji kwenye jua, yasage na kiasi cha magamba hayo chukua magamba ya muoka (muoki, maloni, oak) halafu yakande katika asali na chukua na uchanganye katika juisi ya karoti (carrot) na unywe kiasi ya kijiko kimoja kwa muda wa mwezi mzima mfululizo, na baadae uvute moshi wa kitunguu maji kabla ya kulala.

  Vidonda ya saratani:
  Chukua juisi ya kitunguumaji kiasi cha kikombe, chukua na kiota (kiwawi, nettle) kamua majani yake kiasi cha kijiko kimoja na ongezea juisi ya kitunguu na halafu chukua hina iponde ndani yake ili ipate kuwa marhamu inayopakwa katika vidonda; fanya hivo kila siku pamoja na kunywa juisi ya kitunguu maji iliyochanganywa na juisi ya kiota kijiko kimoja kidogo na baada ya hapo kunywa kikombe kimoja cha maziwa.

  Mvilio wa damu (Bruise):
  Changanya juisi ya kitunguu maji pamoja na kiasi cha mafuta ya kafuri, sugua mahala pa mvilio asubuhi na jioni.

  Majipu:
  Saga kitunguu maji na kikange katika mafuta ya zaituni bila ya kuwa rangi ya manjano, paka kama marhamu na funga bendeji juu yake. Kila siku ukibadilisha pamoja na kusafisha utokaji wa usaha umalizike, halafu utakuwa ukitumia habasouda.

  Chunusi:
  Chukua kitunguu maji kisha ukisage, halafu ukikande katika unga wa ngano nzima, changanya na yai pamoja na mafuta ya simsim(ufuta) na upake usoni asubuhi na jioni pamoja na kula kitunguu kwa sana.

  Ukurutu (Eczema):
  Chukua juisi ya kitunguu na nanaa (mint) vipimo sawa, tengeneza kama krimu (cream) na ujipake baadae pangusa ukurutu kwa maji ya siki nyepesi, rudia kila siku pamoja na kujiepusha na kila kinachochea hisia. Kula matunda, mboga na asali kwa wingi.

  Saratani ya ngozi:
  Chukua juisi ya kitunguu maji, uwatu uliosagwa na salfa manjano kiasi cha robo kijiko kidogo; tengeneza marhamu jipake kila siku. Baada ya kuosha jioni jipake mafuta ya zetuni endelea hivyo kwa muda wa wiki.

  Mgonjwa wa figo na vijiwe:
  Chukua kitunguu bila kukichambua, tia mbegu ya tende baada ya kuichoma kama vile buni na kuisaga; halafu kila siku kula kimoja kula kimoja kwa muda wa wiki.

  Kikohozi kwa wakubwa na wadogo:
  Saga kitunguu kitie ndani ya kikombe cha asali; iwache kwa muda wa masaa matatu (3) kisha uisafishe. Kula kiasi cha kijiko kimoja kila baada ya chakula.

  Kisukari (Diabetes):
  Kila siku kula kitunguu. Sukari itashuka na baadae kula mzizi wa kabichi (cabbage).

  Maradhi ya macho:
  Chukua maji ya kitunguu na asali vipimo sawa halafu ujipake jichoni (kama unavyojipaka wanja) , (dawa hii naamini ni dawa bora kwa maradhi ya macho yote nakuambuka marehemu bibi yangu alikuwa akiwatibu wagonjwa wenye mtoto wa jicho kwa kutumia dawa hii) jipakae jichoni kwa kutumia glassrod au kama huna kifaa hicho unaweza kutumia nyoya la kuku au ndege yoyote.

  Kikohozi:
  Chemsha maji ya kitunguu maji na asali kunywa kijiko kimoja kila baada ya kula na weka kibandiko cha kitunguu maji juu ya kifua na majani yake kwa bendeji kabla ya kulala.

  Kufungua choo:
  Chambua kitunguu, tia katika maziwa na kunywa.

  Kutia nguvu na nishati:
  Choma kitunguu pamoja na maganda yake halafu kichambue na ukikande katika asali na samli, weka katika mkate wa ngano nzima kama vile sandwich. Kula wakati wa chakula cha asubuhi na unywe maziwa nusu lita.

  Kupunguza uzito:
  Kwa anaetaka kufurahi mwili wake uwe mzuri na mwepesi, kuyayusha mafuta na kuondoa kitambi na mwili tepwetepwe miongoni mwa wanaume na wanawake basi afwate hivi:
  1. Kila siku kunywa maji ya kitunguu maji kiasi cha kijiko kimoja kidogo unaweza kuchanganya katika juisi ya matunda ukanywa.
  2. Soma sana katika masaa ya mwisho wa usiku na kukizingatia ukisomacho (ukisoma Quraan utapata faida 2 kwa wakati mmoja, moja ya hapa duniani na moja ya huko tunapokwenda akhera) pia usile chakula cha usiku isipokuwa maziwa ya mgando kikombe kimoja, au matunda.
  3. Tembea sana na kufanya mazoezi kwa wingi.

  Inshallah leo nitakomea hapa. Mola atujaalie afya njema. Amin
   
 2. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Dah,asante sana mzizi,...nimeikopi na kuweka kwenye ms word ntaipita kesho vizuri zaidi
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Na wewe pia asante Kitunguu maji kina Faida nyingi hizo nilizosema ni chache tu
   
 4. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,693
  Likes Received: 411
  Trophy Points: 180
  Shukrani kwa darasa hili,ila naomba kufahamishwa hiyo juisi ya kitunguu naitengeneza vipi? Pia nilikuwa naomba darasa la faida ya asali na matunda/viungo vifuatavyo parachichi/tangawizi na vituu swaumu
   
 5. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,090
  Likes Received: 6,555
  Trophy Points: 280
  Asante sana Mkuu, nimeitunza kwenye faili langu la tiba, nawashangaa wana jf ambao hawapitii humu wanakosa mengi sana.
   
 6. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  tunashukuru mkuu tumekusoma maana shule haziishi tumesha kupata
   
 7. Salanga

  Salanga JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu lakini kama hamna mafuta ya ufuta kuna kitu mbadala katka kutibu chunusi?
   
 8. mchakachuaji192

  mchakachuaji192 JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Shukrani kwako mzizi mkavu
   
Loading...