Faida na manufaa ya kucheka kwa binadamu

Mkuu huyu anajitahidi sana katika kutufahamisha mambo mbali mbali ya kula vyakula bora ili kuweza kukinga afya zetu.

Napenda zaidi madawa yake fulani ya asili..
hata siku moja sijawahi ona akimwambia mtu kanunue Asprin au Klorokwin..
yeye atachanganya vitunguu saumu sijui malimao, asali na nanilii lohhhh dawa tayari..

Nampa heshma yake kwa kweli..
 
Kwa hiyo MziziMkavu, mie pia nacheka kila wakati hata usingizini hadi meno yanapauka. Ina maana sihitaji gym eeh?
Asante manake nakomboa mapene na wakati.
 
Napenda zaidi madawa yake fulani ya asili..
hata siku moja sijawahi ona akimwambia mtu kanunue Asprin au Klorokwin..
yeye atachanganya vitunguu saumu sijui malimao, asali na nanilii lohhhh dawa tayari..

Nampa heshma yake kwa kweli..
:lol::lol::lol: Unanifurahisha naandika hapa kwenye keyboard huku ninacheka kwa maneno yako kusema ukweli Madawa ya kizungu yaani Asprin,Klorokwin na Madawa mengineyo mingi

tu ni yana madhara kwa mwili wa binadamu kwa kizungu tunaweza kusema kuwa madawa ya kizungu ya
Side effects sio kama hayatibu la hasha yanatibu kwa haraka na yanakupa madhara mengineyo katika mwili . ukitaka kutumia Madawa

ya kizungu lazima utumie pamoja na Dawa za Vitamins ili kukinga hizo Side effects lakini pia hata hizo Dawa za Vitamins zina madhara ndani yake. Lakini ukitumia Madawa Asilia kwa mfano Asali,Mdalasini,Kitunguu Maji,kitunguu Saumu,Pilipili

hoho,Tangawizi na kadhalika hazina madhara kwa binadamu hata kidogo. Ila unatakiwa utumie kwa kipimo chake. Mimi nilikuwa na Rafiki yangu Babu Mmoja Mnyamwezi Mtu wa Tabaora mnamo Mwak 1980 kabla sijasafiri nje ya nchi, hapo Dar

nilimshangaa Mzee huyo wa kinyamwezi ana umri wa miaka 90 ana wake 3 na ana nguvu za kiume. Nikamuuliza eti Babu mbona una wake 3 unazo nguvu za kiume?alicheka sana huyo Babu alikuwa ni Mganga wa kienyeji,akanipa Siri ya

mafanikio yake kwanini ana nguvu za kiume akaniambia kuwa nyie vijana mnatumia sana mafuta ya kupikia ,sindano za Hospitalini,Mchuzi wa nazi Sukari nyingi yaani vitu vya vyakula vya sukari nyingi na Bamia ya mrenda ndio maana mnakosa nguvu za

kium
e,hivyo akaniusia usitumie vitu hivyo kwa wingi utakuwa na matatizo ya nguvu za kiume. Mimi tangu siku hiyo nikashika hiyo miiko yake huyo babu wa kinyamwezi akanifundisha madawa mengi tu. Nakuacha hapo kwa leo mkuu Afrodenzi.

Kwa hiyo MziziMkavu, mie pia nacheka kila wakati hata usingizini hadi meno yanapauka. Ina maana sihitaji gym eeh?
Asante manake nakomboa mapene na wakati.
Na mimi pia unanifurahisha sana nikiangalia hiyo Avatar yako sijuwi shemeji yangu yaani mpenzi wako au mume wako akikukasirikia si utamuuwa kwa hiyo silaha yako bibie King'asti? avatar yako inanivutia lakini pia inanitia woga kidogo hahahahahahahha:lol::lol::lol:
 
Kwa hiyo MziziMkavu, mie pia nacheka kila wakati hata usingizini hadi meno yanapauka. Ina maana sihitaji gym eeh?
Asante manake nakomboa mapene na wakati.
1374166_593677714026031_249672990_n.jpg
 
Matibabu kwa kucheka- Zimbabwe



100505122746_vichekozimbabwe_466x262_nocredit.jpg

Vicheko Zimbabwe


Wanawake wawili wana mpango wa kuanzisha klabu za kucheka Zimbabwe, nchi inayokabiliwa na changamoto kubwa za kiuchumi duniani.
Shilpa Shah na Celina Stockill wanaamini watasaidia watu kukabiliana na majaribu ya maisha ya Zimbabwe.
Hivi karibuni waliandaa warsha katika tamasha la kimataifa la sanaa mjini Harare, huku wakiwapa mafunzo ya kushawishi watu kucheka.
Bi Shah ambaye ni mkufunzi wa kucheka amesema, "Ukicheka-unabadilika; na wewe ukibadilika- dunia nayo hubadilika."
"Kwahiyo ni amani duniani, vicheko kwa Zimbabwe, kwahiyo tufurahishane na kueneza furaha."
Katika warsha zao, Bi Shah na Bi Stockhill hushawishi watu kushikana mikono, kila mmoja akiweka sura yake imchekeshe mwenziwe, na kulala sakafuni na kupiga miguu yao hewani.
Pia huwaambia wabirue mifuko yao ya susruali ambayo haina kitu na kila mmoja aanze kumcheka mwenziwe kwasbabu hana fedha, na kunyoosheana kidole huku wakichekana.
Mtu mmoja katika warsha hiyo amesema, “ Tunahitaji kucheka zaidi, hasa katika hali hii tuliyonayo Zimbabwe- ukiwa masikini, ni muhimu ujifunze kucheka.”
Mwaka jana serikali ya umoja ilisaidia kuzuia kuporomoka kwa uchumi wa Zimbabwe- uchumi uliyosababisha dola ya nchi hiyo kupoteza thamani yake- kwa kuruhusu utumiaji wa fedha za kigeni.
Lakini hii inamaanisha wale wasio na uwezo wanapata tabu zaidi.
‘Hakuna ucheshi’

Hali ya watu katika warsha hiyo ilibadilika haraka toka wakati walipokuwa kimya hadi pakalipuka furaha.
Bi Shah amesema, “ Siyo lazima uwe na sababu kucheka; siyo lazima uwe na furaha ndio ucheke.”
“Na si lazima uwe mcheshi kucheka.”
100505123323_zimbabwevicheko_226x170_nocredit.jpg
Celina Stockhill na Shilpa Shah


Bi Stockhill anasema kucheka kuna faida nyingi za kiafya, na ana imani nzito kuwa watu wanuiwe kucheka kwa dakika 10 kwa siku.
“Kuna faida tatu- za hisia, kimwili na kiakili. Tunatoa msongo wa mawazo kwa kucheka, kuushughulisha mfumo wa limfu na ni nzuri sana kwa moyo wako.”
“Inasaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na mfumo wako wa uzazi.”
“Tunahitaji kutumia kiwambo kucheka, kucheka kupitia tumbo. Najiangalia kwenye kioo na kucheka kwa takriban dakika 10 hadi 15.”
Wakufunzi hao walio wachangamfu, wakweli na kutaka dunia iwe bora, wana mpango wa kuanza mtandao wa klabu mbalimbali za kucheka nchini Zimbabwe.
Bi Stockhill amesema, “Tumezoweshwa kucheka kwa mambo kadhaa lakini mafunzo haya yanampa mtu fursa ya kucheka bila sababu yeyote na katika eneo salama.”

BBC Swahili - Habari - Matibabu kwa kucheka- Zimbabwe


 
Je wajua kicheko ni Tiba ya Ukweli?




Utafiti umeonyesha kwamba faida ya kucheka ni kubwa na inayofaa kwa afya ya mwili na akili. Watafiti hadi sasa wamedokeza kuwa kicheko husaidia kupunguza maumivu,

kuleta furaha zaidi, na hata kuongeza kinga. Kicheko kwa hiyo, ni dawa isiyo na gharama ambayo kila mmoja anaweza kuipata. Kinachotakiwa ni kujenga mazoea ya kufurahi na kujitahidi kuwa na hisia ya ucheshi mara kwa mara.

Faida za kicheko:


1.
Homoni:
Kicheko hupunguza kiwango cha homoni zinazoleta msongo(stress) kama cortisol na epinephrine dopamine (Adrenaline). Pia huongeza kiwango cha homoni ya kuimarisha afya kama endorphins na neurotransmitters. Kicheko husababisha kuongezeka kwa idadi ya seli za kinga (antibody); pia huzalisha na huongeza ufanisi wa seli T. Yote hii ina maana kuwa mfumo wa kinga mwilini huimarika, na hupunguza uwezekano wa msongo wa mawazo(Stress).


2. Mwili kujiachia(Physical release):
Baada ya kicheko akili na mwili hupata hisia nzuri, ni kama unajiachia


3. Utendaji wa ndani
Kicheko hutoa mazoezi ya kiwambo (diaphragm), husaidia mabega (works out the shoulders) na kufanya misuli kushirikiana zaidi;lakini pia husaidia moyo(provides a good workout for the heart). Kicheko pia huondoa hasira, hatia, dhiki na hisia hasi.

4.
Kijamii
Kicheko hutuunganisha na wengine. Kucheka hujenga mahusiano mema na huleta kuaminiana.Furaha na faida ya kicheko huongezeka maradufu ikiwa watu wengi wanacheka pamoja.Kicheko ni njia nzuri ya kufahamiana na kushirikiana.

Unaweza je kucheka:

Kicheko ni moja ya tiba mbadala ya bure, urahisi na yenye manufaa kwa njia nyingi. Unaweza kupata zaidi kicheko katika maisha yako kwa mikakati ya ifuatayo:

1. Angalia vipindi vya TV vya kuchekesha pamoja na filamu za ucheshi.

2. Cheka na marafiki kazini,shuleni na hata nyumbani.Fanya kicheko kuwa tabia yako.

3. Acha kulalamika kuhusu maisha, jaribu kucheka . Kama jambo fulani linakuchanganya ni vizuri kuangalia nyuma juu yake na kucheka. Usikubali kusongwa na mawazo,zungumza na wenzako lakini juu ya yote angalia,soma au kumbuka mambo yatakayokuchekesha !
 
Back
Top Bottom