Faida na hasara za uchokonozi.

ndayilagije

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Posts
7,490
Reaction score
8,305
Naamini wanajamvi mpo kama kawaida pamoja na machungu mengi tunayopitia tunazidi kupambana na hali zetu.
Uchokonozi ni neno la kiswahili linaloshabihiana na upekepeke. Katika jamii yoyote ile wachokonozi hawakosekani. Karama yao kubwa ni kuona mapungufu kila mahali na kuyaanika hadharani. Ikumbukwe kuna mapungufu mengi katika kila kitu kinachotuzunguka,yapo yaliyodhahiri na ya siri,yaliyofichwa makusudi na yaliyojificha kwa bahati mbaya. Yote ni mapungufu tu.
Kwa kutambua hilo watu wakaja na msemo kuwa "Aso kasoro hakuna."ni kweli hakuna. Lakini nani anayefurahia kukosolewa? hayupo.
Binafsi namkubali sana mheshimiwa Tundu Lisu kama mchokonozi mahiri wa kizazi hiki.(Mungu amjalie ahueni).Yuko vizuri sana katika kuziona kasoro za mambo na kupaaza sauti yake bila kuogopa. Si kweli kuwa anasema yasiyokuwepo. Kwa karama hiyo inampa uhodari kama mwanasheria mzuri awezaye kuona mapungufu yaliyojificha au kufichwa.Ana jicho kali.
TL,mbunge,mwanasheria,raisi wa TLS,na vyeo kibao alivyo navyo nchi hii. Kwa upande mwingine amsha amsha yake huwa inafedhehesha hasa kama pungufu linakuwa ni la makusudi.Hivyo kumjengea uhasama kwa mkosolewa. Ni kwa sababu hiyo nikijua kuwa sistahili kumpa ushauri kwa maana Mimi ni mdogo mno,nadiriki kusema TL ni muhimu kuchokonoa na kisha kujinyamazia tu,muhimu kwake ameweka wazi kasoro inatosha. Itashugulikiwa namna gani asijali. Si kashaiweka peupe bwana.
Sasa ngondo huja pale anapotaka matokeo ya uchokonozi wake kutambuliwa..
Yote kwa yote dunia bila watu kama yeye haipendezi kwa kweli.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
 
WAZUNGU WABAYA SANA, KAMWE HAWATAFANIKIWA KUTUCHONGANISHA ILI WAPATE WAKUMSHIKA MKONO!
MADINI YETU MALI YETU.
SIASA ZETU WATU WETU WAACHE KUMWAGA DAMU ZETU ILI KUPANDIKIZA CHUKI.
 
Babu aliniasa ukitaka kufa muda siyo wako chungulia kila jambo fatialia maisha ya watu utapotea bila kujijua ni mengi sana nimeyaona na alisema usione watu wamekaa kimya kwa jamboi lolote siyo kwamba hawajui mwanangu chunga mdomo wako utanaswa na ndoano
 
Sikuhizi hatusikilizi babu zetu eti[emoji16][emoji16]Mange tu akisema basi.Bibi zetu ndo hatuwataki kabisa eti wanamacho mekundu.Tukifa haraka tunamlilia mzee Serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…