Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,113
- 34,953

Walenga walisema adhabu ya kaburi aijuaye maiti na ukiona aisifiaye mvua ujue imenyea. Misemo hii ni kweli kabisa kwani pilipili iliyo shamba haiwezi kukuwasha wewe mtu uliye mjini. Kuna siku za nyuma niliwahi kuandika makala nikielezea umuhimu wa teknolojia, nilizungumzia mambo mengi sana likiwemo la kurahisisha maisha na sio kuongeza ugumu.
Tekinolojia inayofanya maisha yawe magumu sio teknolojia inayokubalika katika ulimwengu wa leo, na tegemea kukimbiwa kama ukoma. Kuna usemi unaosema "IT Doesn't Matter" akimaanisha teknolojia ya mawasiliano sio kitu, hapa hawamaanishi kuwa teknolojia ni boya, bali kuwa na teknolojia sio kitu kigeni, kitu kigeni ni manufaa yake.
Katika miaka miwili ya karibuni tumeona mabadiriko makubwa kwenye uliwengu wa vifungulia tovuti (browsers), browsers ni programu zinazotumika kufungulia tovuti, mfano wake ni Mozilla Firefox, Internet Exproler na hii mpyampya kidogo Google Chrome. Browser hizi zimejitahidi sana kumfanya mtumiaji awe na uwezo wa kufanya mambo mengi kwa haraka zaidi bila ya kirudiarudia hivyo inaokoa muda (haswaa kwa wale wenye internet zenye spidi hohehae).
Ulimwengu wa sasa, tunaenda katika mfumo wa pamoja (Unified System) ambapo kila kitu kinapatikanika kwa pamoja, hii ndio sababu ya kuja kwa mfumo wa mawingi wa kompyuta (cloud computing), mfumo huu hukuwezesha kutumia hazina zilizo kwenye internet bila kujali zitokazo, ingawa mfumo huu sio mpya tena, ila utekelezaji wake bado unasuasua kutokana na sababu nyingi ndani yake, leo sitokugusia kwa sana kuhusu mfumo kwani sio langu.
Katika ulimwengu wa kompyuta na Internet kuna kitu kinaitwa SEO (Search Engine Optimization), SEO huwawezesha watu kukupata kwa kutumia vitafuto, vitafuto hivi ni kama Google, Baidu, Bing nk.
Katika siku za karibuni, vitafuto hivi vimefanya mabadiriko makubwa katika mpangilio wake, yaani nani atatokea kwanza kwenye matokeo ya mtafuto, kwa mfano ukienda kwenye google na kutafuta, habari za Tanzania, je ni tovuti ipi itakuja ya kwanza? Ingawa vitafuto hivi hutumia njia tata
kukokotoa nani anakuwa wa kwanza, ila ndani ya mkokotoo huo, moja ya vitu vinavyopewa kipaumbele ni upekee wa taarifa (sio za kukopi na kupaste) na ukubalikaji (je watu wangapi wanazungumza juu yako)? Hivyo basi kama utafanikiwa kushika sehemu hizi, inamaana mtu akienda Google na kutafuta kitu moja kwa moja analetwa kwenye tovuti yako.
Kwa nini nimeamua kuongea hivi? Siku za karibuni kumezuka mtindo kwenye tovuti nyingi za Kitanzania ambapo huwazuia watu kubofya mbofyo wa kulia 9right click), wao wakifikiria kuwa kwa kuwaruhusu watu wabofwe kutapoteza watembeleaji, nimewahi kuongea na baadhi ya wamiliki wa
mitandao maarufu nchini juu ya hili, wote walisema, watu wengi hukopi na kuhamishia kwenye tovuti zao bila kuonesha chanzo cha habari hivyo kumfanya msoaji ashindwe kujua nani ndiye chanzo cha habari. Hii inadhihirisha umimi na uchoyo tulionao. Pia inaonesha wengi wao wasivyofahamu umuhimu au faida ya hao wakopiji. Kama ningekuwa mimi, ningechekelea badala ya kulalama ingawa ni uungwana kuonesha chanzo.
Faida inayotokana na ukopiji wa habari ni kusambaa kwake, pia kwenye mitambo ya vitafuto (SE) yao itakopi asili kuwa ni wewe hivyo kokote ile habari inapoenda, wewe ndiye utakuwa chanzo labda kama mkopiji ana ufahamu na muda wa kutosha kuweza kucheza na hii mitambo kitu ambacho si kweli kwa asilimia kubwa kama si yote ya hawa wakopiji.
Sasa kitendo cha mwenye tovuti au blog kuzuia watu kukopi kwa kubana right click sio tu kutazuia watu kusambaza habari yake (kwa wale wema walio tayari kuonesha chanzo na walio tayari) bali pia inaweza kukufanya kupoteza masomaji na watu wengi kuishia kusoma vichwa vya habari na kuondoka hivyo kuongeza idadi ya watimkaji (Bounce rate) hivyo kushusha chati yako kwenye mitambo ya utafutaji. Binafsi ni mmoja wa hao watu,
mara nyingi huwa ninapenda kufungua habari nyingi kwa kutumia tab halafu ninaanza kuzisoma moja moja, ila ninapoenda kwenye tovuti inayonizuia kufanya hivyo, huwa ninafanya mambo mawili; moja ni kutimka (kama kuna njia mbadala), pili ni kuondoa hiki kizuizi na kusoma makala bila utata (ila hii ni nadra sana kwakuwa tovuti hizi nyingi ni za habari tena za kawaida)
Ila kabla sijamaliza, pia ningependa kutoa wito kwa wale wanaokopi, kutambua kazi za watu, kwani kuna baadhi ya habari / makala watu wamekaa chini na kuumiza kichwa kuziandaa, hivyo inapendeza kuonesha unavyojari kwa kurudisha linki kwa kuonesha inapotoka. Kwa njia hii sio tu itaongeza molale wa mwandishi kwa kuona ukubalikaji wake kwa jamii bali pia ni moja ya njia ya kumsapoti mwandishi kwa mchango wake.
Pia kwa wale wanaohofia kuibiwa kwa kazi zao, wanaweza kutumia alama thabiti (watermark) ainayoandika neno au picha fulani juu ya picha na kuonesha asili yake, kwa mtindo huu unaweza kuzuia wezi au watu wasio wataarabu.
Na M Nyoni
mnyoni@dudumizi.com
Chief Business Development officer - Dudumizi Solutions