Faida elfu 30 kwa siku

chiefnyumbanitu

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
906
426
Habari wana FJ,

Nimekua nikipata faida ya elfu 30 kwa siku katika biashara yangu ndogo ndogo lakini imekua ikipotea tu kwa matumizi madogo madogo ya hapa nyumbani mpaka nmewaza nifungue account benki au niweke akiba kwenye mitandao ya simu, sasa ombi langu kwenu kati ya benki na kuweka akiba kwenye makampuni ya simu, muonavyo ndugu zangu wapi kupo salama zaidi?

Sina mengi zaidi natanguliza shukrani kwenu.
 
Popote utakapoiweka itakatwa gharama za utunzaji. Aidha uwe unazurudisha kuongeza mtaji ili faida nayo iongezeke au laa ihifadhi M-PAWA kwa mwezi utapata riba asilimia kadhaa.
Lakini pia ni aina gani hiyo biashara nami niifanye.
Asante kwa ushauli. Nasubiri wengne pia nipate mawazo yao..

Biashara niifanyayo ni bidhaa za kichina kama bed shet,taulo, pazia, sofa set... n.k
 
Popote utakapoiweka itakatwa gharama za utunzaji. Aidha uwe unazurudisha kuongeza mtaji ili faida nayo iongezeke au laa ihifadhi M-PAWA kwa mwezi utapata riba asilimia kadhaa.
Lakini pia ni aina gani hiyo biashara nami niifanye.
Zipo benk ambazo unaweza kutunza hela na usikatwe makato yeyote (mfano Equity Bank) .Nakushauri ufungue akaunti benki
 
Ndugu, unaweza izalisha pesa yako zaidi endapo utapenda kujiajiri na Mobistock kwa mtaji ulionao wa kuanzia 10,000/= tu. Mobistock inakuwezesha wewe kuwa wakala ambaye utatoa huduma tofauti tofauti katika jamii kwa kutumia simu yako ya kila siku ya kiganjani. Huduma utakazoweza kuzifanya ni kuuza vocha zote za kurusha (Voda, Tigo, Airtel, Zantel, Smart na Halotel) utaweza kuwaungia wateja vifurushi vya muda wa maongezi vya Tigo na Zantel, utaweza kuwanunulia wateja vifurushi vya AZAM, DSTV, Smile na Startimes pia. Kwa kila muamala ufanyao hapo utalipwa kamisheni / faida papo kwa hapo.. hii inamaana pesa yako utakuwa unaizungusha na kukuletea faida kuliko kuweka benki ambapo kila kukicha itakuwa ikipungua kwa ajili ya makato mbali mbali.. Kujua zaidi juu ya Mobistock wasiliana 0755 572 777 / 0655 057 212
 
Ndugu, unaweza izalisha pesa yako zaidi endapo utapenda kujiajiri na Mobistock kwa mtaji ulionao wa kuanzia 10,000/= tu. Mobistock inakuwezesha wewe kuwa wakala ambaye utatoa huduma tofauti tofauti katika jamii kwa kutumia simu yako ya kila siku ya kiganjani. Huduma utakazoweza kuzifanya ni kuuza vocha zote za kurusha (voda, tigo, airtel, zantel, smart na halotel) utaweza kuwaungia wateja vifurushi vya muda wa maongezi vya tigo na zantel, utaweza kuwanunulia wateja vifurushi vya azam, dstv, smile na startimes pia. Kwa kila muamala ufanyao hapo utalipwa kamisheni / faida papo kwa hapo.. hii inamaana pesa yako utakuwa unaizungusha na kukuletea faida kuliko kuweka benki ambapo kila kukicha itakuwa ikipungua kwa ajili ya makato mbali mbali.. Kujua zaidi juu ya Mobistock wasiliana 0755 572 777 / 0655 057 212
Nmekupata vizuri sana.
 
Mhhhh..
 
We mzee wa kulialia kumbe wewe tajiri mkuu.
Maana mie kijana akiweza kuingiza faida ya elfu 30 tu basi ni tajiri,maana ni pesa nyingi sana na ukiweka nidhamu basi unatusua ile mbaya.Naeleza hivyo kwakua najua nilipotokea.

Nakushauri weka Bank kama fixed vile,ili ikae huko kwa muda mrefu Halafu wakati huo unafikiria biashara ya ziada ya kufanya,yaani biashara mpya.Wakati wewe unapiga roving zako,pesa ikifikia kiasi fulani basi unaanzisha biashara hata kama ndogo ya laki mbili au tatu,ukiona inalipabasi tafuta mtu umuweke ili uwe na biashara zaidi ya moja ila iwe tofauti na unayofanya.Licha ya kwamba unaweza kwanza kuboresha hiyo uliyonayo ila kama umefika kwenye level fulani unaanzisha mpya.

Hapo akili yako itatanuka,na hata soko la upande mmoja likifa basi upande mwingine upo vizuri unawezakukaza huko
Mie miaka ya 2003 nilikuwa na banda la sim zile za kupigisha,wakati huo sim ya mkononi aisee watu kibaoo hawana,nilipiga hela balaa,na 2004 nikaoa harusi kubwa ile mbaya,maana pesa ilikuwepo,we unauza kadi zote na unapigisha sim bonge la foleni.Then baada ya kupata pesa nikamuita mdogo wangu nikawa nauza Tv na Deck natoa Zanzibar naleta Dar,nilipga hela balaa mkuu,kisha nikaanza kupeleka Mwanza.

Nilivyokuwa imara nikaanza kupeleka Burundi,ila huko nilienda round moja tu,ile round ya pili nilipeka Tv kama 200 na deck 300,basi mie na wenzangu wote tulitekwa,wakatupa kichapo cha maana,huku na silaha,wakahamisha mali zoote wakakimbia,tulikaa siku kadhaa kwenye maji ndio tukaokolewa na patrol,maana hata mashine walichukua,siisahau siku hii,sijaenda teeena na wala sifikirii kwenda

Kisha,nikaingia kwenye biashara ya kutoa Mashuka ya Kigoma kuuza hapa Zanzibar,piga hela tena hapo,leo imechupia kwenye Carry na Bodaboda,na Spices kwenda Commorro,at the same time pesa ikifika kiasi fulani naanzisha jingine,nina Idea binafsi kwenye Kitambu changu zinafikia biashara 47,na zote nimeishafanya research kwa level fulani na zaidi nashkuru saana wana JF woote na mbarikiwe saana,mambo mengi na ujasiri nimeupata humu,lazima nikiri hilo.Jukwaa hili ni msaada saana kwangu,kule kwenye Siasa tunatukananaaeee tukija humu letu lazima liwe moja.

Ni habari ndefu kiasi mkuu
Lengo nio kukuonyesha kwamba biashara zinatabia ya kubadilika sana tofauti na unavyofikiria mkuu,sasa lazima akili uifungue kwa kuwa na biashara zaidi ya aina moja.
Nisikuchoshe mzee wa kulialia
 
Tunza M-Pawa(Vodacom), au Tigo-Pesa.
1.Uzuri wa M-Pawa unaweza kukopa hadi laki tano(500,000/=) pale unapohitaji.
2.Uzuri wa Tigo-Pesa unapata gawio kila baada ya miezi mitatu, Mimi huwa nakula Gawio langu kila baada ya miezi mitatu, Jana tu nimepokea Gawio langu.
 
Habari wana FJ,

Nimekua nikipata faida ya elfu 30 kwa siku katika biashara yangu ndogo ndogo lakini imekua ikipotea tu kwa matumizi madogo madogo ya hapa nyumbani mpaka nmewaza nifungue account benki au niweke akiba kwenye mitandao ya simu, sasa ombi langu kwenu kati ya benki na kuweka akiba kwenye makampuni ya simu, muonavyo ndugu zangu wapi kupo salama zaidi?

Sina mengi zaidi natanguliza shukrani kwenu.
Weka benki, ni more secure kuliko kwenye simu. Uwe makini tu kufuatilia balance yako maana kuna wafanyakazi benki ambao sio waaminifu. Ila wakiiba na kama wewe una data kamili kuhusiana na balance yako hupati hasara ila benki ndiyo itakuwa imekula hasara.
 
Habari wana FJ,

Nimekua nikipata faida ya elfu 30 kwa siku katika biashara yangu ndogo ndogo lakini imekua ikipotea tu kwa matumizi madogo madogo ya hapa nyumbani mpaka nmewaza nifungue account benki au niweke akiba kwenye mitandao ya simu, sasa ombi langu kwenu kati ya benki na kuweka akiba kwenye makampuni ya simu, muonavyo ndugu zangu wapi kupo salama zaidi?

Sina mengi zaidi natanguliza shukrani kwenu.
Pesa inayotunzwa bila kuzungushwa haina faida bali inaleta hasara nakushauri usiitunze ongeza mtaji au buni biashara nyingine kwaiyo pesa ili mradi iwe inazunguka inaingiza faida
 
Back
Top Bottom