Faida 10 za kujisomea, ukiacha kuongeza Maarifa

Faida 10 za kujisomea, ukiacha kuongeza Maarifa

Makirita Amani

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2012
Posts
1,914
Reaction score
3,438
Naweza kusema sasa hivi nimekuwa mlevi wa kitu kimoja, kusoma. Na sio kusoma tu, bali kusoma vitu vizuri ambavyo vinanifanya kuwa tofauti, kufikiri tofauti na hata kupata maarifa zaidi.

Naweza kusema kwa kujivunia kwamba chochote ninachofanya sasa kinatokana na maarifa makubwa ninayoyapata kwa kusoma vitabu. Nasoma vitabu vingi na kwa sasa nasoma angalau vitabu viwili kwa wiki, wiki nyingine nasoma zaidi ya hapo ila nahakikisha kila wiki sishuki chini ya hapo.

Mwaka huu 2015 lengo langu ni kusoma vitabu visivyopungua 150, ukichanganya na vingine zaidi ya 200 nimesoma kwa miaka miwili iliyopita, maarifa yangu yataongezeka maradufu.

Leo siandiki haya kukuonesha kwamba nasoma sana ila nataka nikushirikishe faida kumi ninazozipata kwa kusoma, ukiacha kuongeza maarifa ambacho ndio kila mtu anafikiria.

1. Burudani
Kusoma ni burudani na ni burudani ambayo haina madhara yoyote kwenye mwili wako au maisha yako. Kuna baadhi ya vitabu unapovisoma unapata hisia nzuri za kiburudani na unaona uzuri na utamu wa maisha.

2. Kuhamasika

Tunaishi kwenye dunia ambayo inakatisha tamaa sana. Kila jambo ambalo unajaribu kufanya kuna watu watakuambia haiwezekani au kuna watu watajaribu kukuwekea vikwazo. Unapokuwa unasoma vitabu unapata hamasa kubwa sana ya kufanya kile unachotaka kufanya. Unaposoma maisha ya wengine na kuona jinsi walivyopitia magumu, unapata moyo kwamba inawezekana.

3. Mshauri (Mentor)

Ni muhimu sana kuwa na mshauri wako, ambaye anakuonesha wapi pa kupita ili uweze kupata kile unachotaka. Mara nyingi mshauri huyu inabidi awe ameshapitia unakopitia wewe. Katika mazingira yetu ya kitanzania ni vigumu sana kupata mtu wa aina hii, na hata ukimpata anaweza asipate muda mwingi wa kwenda na wewe sawa. Ila vitabu, vitabu ni mentor mzuri sana.

Unaweza kusoma maisha ya watu ambao wamefanikiwa kwenye kile unachofanya na wakakupa mwongozo mzuri sana.


4. Kuwa bora zaidi

Licha ya kuongeza tu maarifa, kusoma kuna kufanya unakowa bora zaidi katika kila eneo la maisha yako. Kabla sijajingea tabia ya kujisomea nilikuwa mtu wa kuhukumu, kukwazika, kuchukia, kubishana na mengine mengi. Lakini yote hayo nimeyaacha sasa, sina tena muda wa kuhukumu kwa sababu najua kila mtu ana matatizo yake, kila mtu anachagua maisha yake.

Sikwaziki tena wala kukasirishwa na mtu kwa sababu najua anayetaka kukukasirisha anataka na wewe uwe na matatizo kama aliyonayo yeye, nishakuwa mjanja, sinunui tena matatizo ya watu. Na kilicho bora zaidi sibishani, zamani nilikuwa nikiwa na wazo langu na mtu akalipinga, nabishana nae mpaka nihakikishe amekubaliana nami, lakini sasa sibishani tena, kwa sababu nimejifunza kama wazo lako ni sahihi huna haja ya kulipigania, maana mwisho wa siku ukweli utashinda. Na kama wazo lako sio sahihi pia huna haja ya kubishana maana hakuna atakayekusikiliza au kujali.


5. Kuishi maisha tofauti tofauti

Mtu anayesoma vitabu anaishi maisha zaidi ya 1000 kabla hajafa, mtu asiyesoma vitabu anaishi maisha mamoja tu mpaka anakufa. Sasa unafikiri ni yupi ambaye anakuwa na maisha mazuri kati ya hawa wawili?

Kitabu kinaweza kukutoa hapa na kukupeleka kwenye mapiramidi ya misri, kikakupeleka marekani, kikakupeleka china na kadhalika.


6. Kuandika

Moja ya faida kubwa ninazopata kwa kusoma vitabu ni kuandika. Ndio huwezi kuandika kama husomi, nazungumzia kitu ambacho kinaweza kuwasaidia wengine. Huwa naandika kila siku, zamani ilikuwa maneno 1000 ninapoamka asubuhi lakini sasa ni zaidi ya maneno 2000.

Fikiria pale unapohitaji kuandika kila siku, jumatatu mpaka jumatatu, mwaka mzima, ni kazi ngumu eh? Kuna siku naweza kuamka sijisikii kabisa kuandika, nachukua kitabu na kuanza kusoma, nusu saa baadae nakuwa nimepata mawazo zaidi ya matano ya kitu ninachotaka kuandika.

Mara nyingi mawazo hayo hayatoki kwenye kitabu hiko ninachosoma, ila kile kitendo cha kukaa na kuanza kusoma ni kama milango ya akili inafunguka na kuanza kumwaga mawazo mazuri. Napenda sana hii hali.


7. Kutunza muda

Unapoanza kujijengea tabia ya kujisomea, moja kwa moja unaanza kujijengea tabia ya kutunza muda. Hutapoteza tu muda na kuona huna cha kufanya kwa sababu muda wote una kitabu cha kusoma. Na pale ambapo una kitu cha kukusukuma umalize kitabu haraka kila dakika chache utakazopata utazitumia vizuri kusoma.

8. Kupunguza gharama

Unapojijengea tabia ya kujisomea, muda wako mwingi unautumia kusoma hivyo hutapata mawazo ya nifanye nini sasa na kujikuta umeenda kufanya jambo ambalo linakuingiza kwenye gharama ambazo sio za msingi. Naweza kuhitaji kubadili mazingira nikachagua kwenda kwenye hoteli kubwa, nikiwa na kitabu nasoma, naagiza maji ya kunywa.

Natulia na kusoma hata kwa masaa mawili bila ya kufanya kingine chochote. Ila ukienda kwenye hoteli ya aina hii na huna kitu cha muhimu cha kufanya, utajikuta unatumia gharama kubwa sana.


9. Kuepuka umbea na majungu

Angalau watanzania tumebobea kwa hili. Kama unapenda kufuatilia umbea na majungu sikulaumu kwa sababu kama huna kingine cha kufanya utafanya nini sasa? Yaani umeamka asubuhi huna ratiba yoyote ya siku zaidi ya kwenda kazini kama ulivyoenda jana.

Utaanza kuangalia nini kinaendelea, Diamond ana mpenzi gani mpya, kampa mimba nani, kavaa viatu vya shilingi ngapi au valentine alitumia kiasi gani cha fedha. Sawa, sikukatazi kufuatilia, ni burudani, lakini kabla ya kuipa burudani hii kipaumbele je maisha yako umeyapa kipaumbele?


10. Kuongeza kipato

Hii ipo karibu sana na kupata maarifa maana maarifa ndio yanafanya kipato chako kuongezeka. Lakini nimetaka niiweke yenyewe ili kuonesha msisitizo zaidi. Zaidi ya mwaka mmoja uliopita, nilisoma kitabu cha Robin Sharma, na moja ya vitu alivyoshauri ni hiki; KUONGEZA KIPATO CHAKO MARA MBILI, ONGEZA KUSOMA KWAKO MARA TATU.

Nikasema nafanyia kazi hilo, kadiri ninavyojisomea ndivyo kipato changu kinaongezeka, mpaka wakati mwingine nashangaa nilichelewa wapi sikuanza mapema kama miaka kumi iliyopita.


Hizo ndio faida kumi za kujijengea tabia ya kujisomea. Anza kujisomea leo, na utaanza kunufaika na hayo na mengine mengi ambayo sijayaandika hapa. Nina uhakika na haya ninayokuambia hapa, hebu anza kufanya na lazima utaona mabadiliko.


KARIBU KWENYE KUNDI LA KUJISOMEA;

Kama unataka kujijengea tabia ya kujisomea na ungependa kupata kitu cha kukusukuma uweze kusoma nakukaribisha kwenye kundi la kusoma vitabu. Kundi hili linaitwa VORACIOUS READERS, katika kundi hili tunasoma vitabu viwili kwa wiki na ni muhimu kila mwanachama kusoma na kujadili angalau kitabu kimoja. Kupata maelezo zaidi ya kundi hili bonyeza maandishi haya.

MUHIMU; Usitake kujiunga na kundi hili kwa sababu tu umehamasika, ni muhimu sana utenge muda wa kujisomea na usome kweli, usipofanya hivyo unaondoka kwenye kundi.

NAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA KUBORESHA MAISHA YAKO.

TUPO PAMOJA.
 
mkuu mmi napenda na nataman sana kujua mambo mapya kwa kujisomea ILA tatiz langu ni mvivu af pia na stress za maisha zinanfanya nisahau swala la kujisomea....Naomb angalau technique mbil tatu apo mkuu.
 
Umeongea kweli tupu!

Ni jana tu nakatiza maeneo ya ubungo terminal nikajikuta bajeti yangu imefanyiwa ambush na kiu ya kununua vitabu. Napenda kusoma vitabu, nafurahia kusoma vitabu! Kusoma vitabu tofauti tofauti ni sawa sawa na kuipa ubongo wako chakula kizuri chenye lishe! Ni kama kufanya mazoezi ya viungo kwa ajili ya kuipa mwili wako afya njema, vivyo kwa ubongo pia chakula chake kikuu ni kusoma na kuandika!

Someni vitabu tofauti tofauti mtajikuta mnainjoi maisha pamoja na magumu yake!
 
mkuu mmi napenda na nataman sana kujua mambo mapya kwa kujisomea ILA tatiz langu ni mvivu af pia na stress za maisha zinanfanya nisahau swala la kujisomea....Naomb angalau technique mbil tatu apo mkuu.

Uvivu
Anza taratibu taratibu mwishowe utaanza kuinjoi na kuendelea vema. Jiunge na lile group la jamaa ili upate hamasa

Stress
Suluhisho kuu la stress ni kusoma ili upate maarifa. Stress zipo kwa sababu ya kutoielewa dunia vizuri, huna utambuzi. Kusoma kunakusaidia sana ku handle viji ishu ndogo ndogo kama stress za kimaisha!
 
napenda sana kusoma novel lakini siwezi kutulia kwa hata dakika tano kuisoma.... lakini cha ajabu kama ni story ya mambo ya mapenzi huwa naweza kuisoma hata masaa kadhaa...
 
Umeongea kweli tupu!

Ni jana tu nakatiza maeneo ya ubungo terminal nikajikuta bajeti yangu imefanyiwa ambush na kiu ya kununua vitabu. Napenda kusoma vitabu, nafurahia kusoma vitabu! Kusoma vitabu tofauti tofauti ni sawa sawa na kuipa ubongo wako chakula kizuri chenye lishe! Ni kama kufanya mazoezi ya viungo kwa ajili ya kuipa mwili wako afya njema, vivyo kwa ubongo pia chakula chake kikuu ni kusoma na kuandika!

Someni vitabu tofauti tofauti mtajikuta mnainjoi maisha pamoja na magumu yake!

Ni kweli kabisa mkuu.
 
napenda sana kusoma novel lakini siwezi kutulia kwa hata dakika tano kuisoma.... lakini cha ajabu kama ni story ya mambo ya mapenzi huwa naweza kuisoma hata masaa kadhaa...

Unahitaji kujijengea nidhamu, unahitaji kuona umuhimu wa kusoma vitabu.
Halafu anza kidogo, soma vitabu ambavyo ni rahisi ila kuna kitu unajifunza.
Panga muda maalumu wa kujisomea, kwa mfano weka utaratibu kwamba unapoamka asubuhi, kitu cha kwanza kabisa unasoma kwa nusu saa. Anza kufanya hivyo, amka mapema zaidi ya ulivyozoea na tumia muda huo kusoma. Anza hata na dakika 20 halafu endelea kuongeza.
Ukifanya hivi bila kuacha utaona mabadiliko makubwa sana.
 
napenda sana kusoma novel lakini siwezi kutulia kwa hata dakika tano kuisoma.... lakini cha ajabu kama ni story ya mambo ya mapenzi huwa naweza kuisoma hata masaa kadhaa...

Si mbaya unaweza kupiga bao kwenye hiyo Nyanja ya utunzi wa mikasa ya mapenzi baadae na ukauza kwa bongo movies n.k.. ongeza bidii hukohuko tu zipo novel nyingi za mapenzi
 
Thanks to Makirita"In every way, in every day I'm getting better and better". In addition to reading pdf based book, three books simultaneously (entrepreneuship, relationship, and religious), currently I'm listening already red books in form of audio.
Listerning audio book, after reading it, it's an enjoyment, fast to remember, save time, multasking .....
I had tried several time to download them, fortunately I can to it, regardless of weak network connection.
Thanks to Makirita Amini, thanks to Google, thank to Youtube. Knowledge is power.
 
Thanks to Makirita"In every way, in every day I'm getting better and better". In addition to reading pdf based book, three books simultaneously (entrepreneuship, relationship, and religious), currently I'm listening already red books in form of audio.
Listerning audio book, after reading it, it's an enjoyment, fast to remember, save time, multasking .....
I had tried several time to download them, fortunately I can to it, regardless of weak network connection.
Thanks to Makirita Amini, thanks to Google, thank to Youtube. Knowledge is power.

Great. Keep learning, keep acquiring knowledge and apply it to improve your work/business and life in general. Also share the knowledge to others so that they can also benefit,
If you want more audio books you can contact me i have a lot of them.
All the best.
 
Mimi napenda kusoma bya kingereza,vinaboost misamiati na kuelimisha..facebook,tweeter,watsup ni tatizo kwa ulimwengu wa bitabu
 
Kwangu binafsi hakuna kitu nachopenda kwenye kusoma kama kuelewa point of view ya mwandishi sio tu kile alichoandika hila kwanini anaona kwa namna yake maana kama binadamu anaweza kuandika kwa hisia za ushabiki, experience yake or just purely criticizing the subject.

Nilichojifunza kumpata mwandishi na kueshimu kazi za watu inabidi urudi nyuma sana kuzitambua basics of reasoning on many fields, kwa sasa naweza sema nilipofikia kuna watu nikiwasikia wanadadavua mambo iwe kwenye maandishi ya vitabu au kwenye audio yaani una appreciate their skills and their level of intelligence (ni jana tu wakati napitia thread ya umiliki wa daladala kwenye jukwaa la biashara kuna mtu katoa advise mpaka unasikia raha the level of education and skills kwenye maandishi yake) na unajua kabisa huyu mtu kaenda shule hila mistari yake ya ku-reason hipo very deep, na kuna wengine ukiwasikia wanakufanya ujione bado sana.

Naamini ukifikia level fulani sio tu ukisikia fulani ana Phd basi udhanie ndio mjuaji kila kitu its rather what has impressed you on his work. Hiyo ndio faraja ya kusoma kwa upande wangu.
 
Great. Keep learning, keep acquiring knowledge and apply it to improve your work/business and life in general. Also share the knowledge to others so that they can also benefit,
If you want more audio books you can contact me i have a lot of them.
All the best.

From our last chat, I need more audio books as possible, budgeting for those memory card plus transportation pose a challenge.
 
Eric Cartman;

Ni kweli unachosema.
Na faida kubwa ya kusoma sio kukariri kila neno bali jinsi unavyosoma mtazamo wako unabadilika. Jinsi unavyoelewa na kujadili mambo kunabadilika na hata picha nzima ya dunia kwako inabadilika.
 
Last edited by a moderator:
You have trully inspired me, i am going to start doing this, what do you recommend to start with?
 
Ni kweli unachosema.
Na faida kubwa ya kusoma sio kukariri kila neno bali jinsi unavyosoma mtazamo wako unabadilika. Jinsi unavyoelewa na kujadili mambo kunabadilika na hata picha nzima ya dunia kwako inabadilika.

Hii ni kweli kabisa.

Mwanzoni nilivyokuwa sijaanza kujisomea nilikuwa naiona dunia katika mrengo tofauti sana baada ya kusoma ninaiona dunia tofauti sana hata nikiwa na argue na mtu naona kabiaa the guy is too shallow.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom