KIMOMWEMOTORS
JF-Expert Member
- May 17, 2018
- 358
- 670
Toyota ni moja ya Makampuni makubwa zaidi ya uzalishaji magari Duniani na wamejikita zaidi katika utengenezaji wa magari yenye uwezo mkubwa na imara lakini bila kuyasahau ya wastani yenye uwezo wa kawaida na ubora wa.
Kwa ufupi, zifuatazo ni baadhi ya tofauti za Magari haya mawili yaani Toyota Vanguard na Rav 4 model za kuanzia 2009 mpaka 2014
1. Injini
Ni ngumu kuzitofautisha injini hizi mbili kwa kua zote zina mwendo na uwezo mzuri. Rav 4 ina injini ya 2.5L ambayo ni Cylinder/Piston 4. Gari hiyo ina injini yenye Cc 2400 ikiwa na 4WD au AWD.
Wakati Vanguard ina injini za Cc 2400 mpaka 3500 na unaweza kuitumia kwa 4WD na 2WD
2. Magumizi ya Mafuta
Hakuna tofauti kubwa kwenye matumizi ya mafuta haswa kwa hizi za Cc 2400 kwa Cc 2400 kwa kua zote huenda kati ya kilomita 12 mpaka 13 kwa lita moja ya Petrol
3. Idadi ya Viti
Idadi ya viti ni moja ya vitu vya kuzingatia unapofikiria kuchagua gari za muundo huu. Rav 4 ina viti 5 wakati vanguard ina viti 7 jambo linalopelekea nafasi ya mizigo kua ndogo huku nafasi ya mizigo katika Rav 4 ikiwa ni kubwa zaidi
4. Uwezo wa Gari
Vanguard inaonekana kua Imara na yenye nguvu zaidi kuliko Rav 4. Nguvu ya Rav 4 kwa kawaida haizidi HP 170 wakati ya Vanguard ni mpaka HP 270 jambo linaloifanya itawale zaidi barabarani
5. Gharama za Uagizaji
Uzoefu katika hizi gari mbili unaonesha kua zinatofautiana kati ya milioni 1 mpaka milioni 3 kutegemea na mwaka kwa kua zina ushuru tofauti. Mara nyingi Rav 4 huagizwa kwa jumla ya gharama za Tsh 23.5 wakati Vanguard huanzia 25.5m
Hitimisho
Kwa kua sasa unajua machache kuhusu gari hizi mbili yaani Rav 4 ya 2009 mpaka 2014 na Vanguard, na kwa kua zote zinaonekana kua sawa kwenye baadhi ya vitu huku zikitofautiana kwenye mambo machache, sasa kazi ni kwako kuamua kuchagua aina ya gari unayoipenda zaidi kulingana na maelezo hayo.