Fahamu zaidi kuhusu gari aina ya kuhusu Nissan Juke

g1986

Member
Jul 10, 2016
60
19
Habari za wakati huu naomba kuuliza kwa yeyote ambaye anajua au analitumia gari aina ya Nissan Juke upatikanaji wake kwa hapa ndani na bei za hiyo gar?

1591788055537.png

Nissan Juke

UFAFANUZI ULIOTOLEWA NA WADAU
Hio machine iko poa kabisa mzee baba,ingawa wabongo watakwambia ni jini mafuta mzee baba.

Na hizi ndinga foleni za dar ndo zinafanya yaonekane yanakula wese lkn ukiwa nalo mikoani huko hakuna foleni unapiga nalo misele kawaida tu mkuu.

Progress ina engine kama 4 hivi:

1.1JZ-GE hii ina cc 2500

2.JZ-GE hii ina cc 3000

Hizi ulaji wake ni kama vile brevis,cresta,mark 2/Verossa zenye engine kama hizo hapo juu,CC 2500 zinatosha kabisa kwa misele/safari/mbio.

CC 3000 kula wese inakula heavy kiaina.

Na hizo hapo juu ndizo engine common hapa bongo.

3.1JZ-FSE hii ni cc 2500

4.2JZ-FSE hii ni cc 3000

Hii engine ya 3&4 zenyewe zinatumia technology ya D4 ambayo wanalalamika zinabagua mafuta(ukiweka mafuta machafu tu inaanza kuzingua),sijawahi kutumia hizo gari yenye D4 so hayo malalamiko hua nayasikia tu kwa mafundi,lk pia wabongo ukitaka kuuza gari yako ukawaambia tu hii ina D4 jua imekula kwako maana wameshalibatiza jina baya.

Khs service parts zinaingilia na hayo magari mengine kwa hio ni zinapatikana tu,kwny body parts kama taa hapo ndipo sina uhakika kama ziko nyingi huko madukani.

Inshort mimi napenda hayo magari yanayoitwa jini mafuta,kwa hio kama mimi ningekua wewe ningelinunua bila kujiuliza mara 2.
---
NISSAN JUKE


Nissan juke ni moja kati ya brand ,asikwambie mtu nigari matata sana ...huku likiwa na umbo la chura ....yaaani ukiliona mpk unaona kuna watu wanafaidi katika dunia hiii kwa maswala ya usafiri

Gari hili linakuja na machaguo mawili ya injini ambayo ni cc 1500 , na cc 1600 huku ikiwa na umbo la hatback

Gari hili likeundwa kwa mfumo mzuri sana umbo lake linapelekea kukata upepeo vizuri na gari kuwa na speed nzuri huku gari hili likishindana na mahasimu wake kama SUBARU XV,MITSUBISHI ASX,HONDA HR-V NA NISSAN DUALIS

Gari hili linakuja na injini ya cc 1500 HR15DE na injini yabpili ni 1600L MR 16DDT Huku ikiwa na nyongeza ya turbo kwa nini liteseke sasa barabarani likifungua turbo unakuwa unasikia ka mluzi ka turbo kwa mbali yaaani hapo linatambaaa hakuna mfano

Transmition yake sasa automatic CVT na manual speed huku nisani wakijitahidi kulipa machaguo mawili kwenye kutembea 2Wd na 4WD...kama unaishi maeneo ya mjini chukua 2WD, na kama unaish maeneo ya milimani na sehemu nyingine zenye tope sana na bara bara za tope chukua 4WD hutajutia kbs

Njooo sasa kwenye grade za gari hili

* * Nissan Juke 15RS – Toleo hili linakuja na injini ya cc 1500( 1.5L )engine, 2WD, manual AC, key start, manual seats, 16-Inch steel rims na no ESC

** Nissan Juke 15RX – Toleo hili linakuja na maboresho kwa ndani ambayo ni injinj ileile cc 1500( 1.5L) engine, 2WD, automatic AC, smart start, manual seats, 17-Inch alloy rims na no ESC

** Nissan Juke 16GT – Hili ni toleo ambalo ni luxury grade linakuja na injini ya cc 1600(1.6L) engine, 2WD, automatic AC, smart start, electric seats, 17-Inch alloy rims na ESC

** Nissan Juke 16GT FOUR – Hili ni toleo linalokuja nlinafanan 16GT lakini utofauti ni kwenye 4WD

Hebu tuangali vitu vya kiusalama katika gari hili ....

ABS, Curtain Airbags, Electronic Stability Control, SRS Airbags

Exterior Features: Alloy Rims, Fog Light

Interior Features: Bluetooth Connectivity, CD/DVD Player, Reverse Camera

Upande wa mafuta je??

Kwanza tank lake lina beba lita 52

Upande wa kutumia mafuta kiukweli lipo vizuri na linastahili pongezi
2013 Nissan Juke

*Nissan Juke 1.5L inatumia km 15.9 kwa lita 1
*Nissan Juke 1.6L inatumia km 13.5 kwa lita 1

Nissan Juke Acceleration

*Nissan Juke 1.5L accelerates inatoka 0-100 km/h kwa sec 11.8

*Nissan Juke 1.6L accelerates inatoka 0-100 km/h kwa sec 9.5

GROUND CLEARENCE
Hapo nisan wametisha kabisa yaani wanajua waafrika wanataka nini linakuja na ground clearence ya 7.0 inch yaaani liko juu mno popote pale unakatiza hata viguguti ,mabanda ya papa,msamvu ,pongwe ,bariadi ,ngasamo ,rombo ,marangu bila shida yaani hapa nawapa

Spare zake
Kuhusu spare ondoa shaka kbs maana spare zake nyingi zinaingiliana na. matoleo mengine ya nissan na hivyo kufanya spare kuwa na bei ya kawaida sana ......

Changamoto
1.bei yake ni mkasi imechangamka sana
2.Upande wa matatizo ya injini anaihitajika fundi mzoefu sio wale wa chini ya muembe mafundi nyundo
3.baadhi sio zote spare bei iko juu
4.Gari za nissan zinahitaji intesive care kama unafuga kuku wa kisasa
kibao

Mwisho

Maneno yangu sio sheria ,kiufupi tu kama uko vizuri mfukon nenda kamchuke mnyama juke aisee hata kuangusha ni gari imara sana tena na liko vizuri sana limetengenezwa kwa kuzingatia mazingira ya Afrika
 
Back
Top Bottom