Fahamu zaidi juu ya ndege Bundi

Fahamu zaidi juu ya ndege Bundi

The Dictator

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
4,340
Reaction score
11,833
Katika moja ya kundi la viumbe hai walio wa ajabu zaidi; basi bundi hawezi kukosekana.

Bundi kama walivyo jamii nyingine ya ndege chimbuko lake ni yai. Mayai ya bundi huchukua mpaka siku thelathini mpaka kuja kutoa kifaranga. Katika utotoaji kifaranga wa bundi kawaida anaweza kuchukua mpaka masaa 48 tangu kutengeneza ufa katika ganda yai mpaka kujitotoa kabisa. Kifaranga atotolewapo huchukua mpaka siku tatu macho yake kufunguka na week 2 mpaka kupata uono wa kawaida.

Kifaranga kawaida anaweza kuanza kuifunza namna ya kuruka na kuwinda vitu vilivyo vidogo vidogo kama minyoo, panzi na kadhalika.

Bundi ni mmoja kati ya ndege hodari zaidi katika mawindo. Macho yake yaliyo na nguvu humsaidia katika kuona windo lake hata akiwa katika umbali mrefu au chini ya nyasi ama barafu. Macho ya bundi yanachukua asilimia 75% ya eneo lote la fuvu la kichwa chake ukilinganisha na ukubwa wa macho ya binadamu yanayochukua asilimia 5% ya sehemu yote ya fuvu la kichwa. Ni ajabu kwa kiumbe huyu pia kuwa na uwezo wa kugeuza kichwa chake pande zote kwa nyuzi 270° pasipo kuhusisha mwili mzima.

Hali hiyo inamlazimu kwa sababu ya jicho lake kutokuwa katika umbo la mduara kuruhusu kuzunguka kama ilivyo kwa viumbe wengine.Pia anauwezo mkubwa wa kuona wakati wa usiku zaidi kuliko mchana kutokana na ukubwa wa macho yake yenye nerves zenye kumuwezesha kuona zaidi usiku ambapo uwezo wake wa kuona usiku ni 2½ zaidi ya binadamu.

Pamoja na uoni hafifu wakati wa mchana bundi hulazimika kufanya mawindo yake mchana hasa wakati wa hali mbaya ya hewa kama baridi kwa sababu manyoya yake yasiyoweza kumlinda zaidi katika vipindi hivyo vya baridi au wakati wa mvua.

Nini kinamsaidia kujua windo lilipo? Bundi anauwezo mkubwa wa kusikia pamoja na sensi zilizo katika manyoya ya kichwani inayoweza kufahamu wapi windo linapatikana.

Pia, bundi anauwezo mkubwa wa kumfikia windo lake pasipo kutoa sauti yoyote ya mapigo ya mabawa wakati wa kupaa tofauti na ndege wote. Hiyo hutokana na ukubwa wa mabawa yake yanayozidi mwili na manyoya mepesi yanayomfanya awe na mapigo ya mabawa yasiyo na sauti na mwezo wa wastani ukilinganisha na ndege wengine wawindao kama falcon na eagle.

=====
MJUE VIZURI BUNDI..

BUNDI ni aina ya ndege ambaye hula nyama; hufanya mawindo yao wakati wa usiku na kupumzika wakati wa mchana. Pamekuwepo na imani kwa wengi kwamba bundi anaponekana nyumbani kwa mtu ni lazima kuna mtu atakufa katika nyumba hiyo. Hivyo imewapelekea watu wengi kuwa na hofu kubwa sana juu ya kiumbe hiki cha Mungu na hivyo kukihusianisha na nguvu za giza kwamba ni lazima ametumwa na mchawi ili kuchukua roho ya mtu. UKWELI UPO HIVI:

Bundi ana uwezo mkubwa sana wa kuvuta harufu ya mzoga kutoka mbali. Uwezo huu wa kunusa harufu unapita uwezo walionao binadamu. Hivyo inapotokea katika nyumba fulani kuna mgonjwa mahututi ambaye seli za mwili wake zimeshaanza kufa lakini mapigo ya moyo bado yanafanya kazi; Bundi huweza kunusa harufu ya seli hizo, harufu ambayo binadamu hawawezi kuihisi, na hivyo huvutiwa kuisogelea kwa ajili ya kujipatia chakula, ila hataweza kuingia ndani kwa kuhofia binadamu. Kwa kawaida binadamu hafi mara moja, bali hufa hatua kwa hatua. Zinaanza kwanza kufa seli za mwili, baadaye ogani mbalimbali za mwili. Ogani za mwisho kufa ni moyo ikifuatiwa na ubongo. Hivyo bundi anapoonekana kwenye nyumba yenye mgonjwa mahututi ni dalili kwamba mgonjwa huyo ameshaanza hatua za kufariki, na hivyo uwezekano wa mgonjwa huyo kufariki siku za karibuni ni mkubwa sana. Inapotokea kwamba mgonjwa amekufa baada ya bundi kuonekana, tafsiri sahihi siyo kwamba kifo kimesababishwa na bundi bali ni kwamba dalili za kifo cha mgonjwa huyo zimetambuliwa na bundi. Hivyo cha kufanya siyo kumtafuta mchawi bali ni kuzidi kumkabidhi mgonjwa huyo katika huruma ya Mungu kwa njia ya sala.

Hofu ya bundi kama kiumbe chenye nguvu za giza ipo zaidi Afrika. Ulaya hawana hofu hiyo. Wao humtazama bundi kama kiumbe cha Mungu, kiumbe cha ajabu, na hivyo huvutika kukaribia kwa njia ya utalii, utafiti na hata ufugaji. Zipo mbuga za wanyama zinazofuga bundi. Sifa mojawapo ya bundi inayowavutia watalii wengi kumtazama ni ule uwezo wake wa kugeuza shingo kutoka mbele mpaka nyuma pasipo kuhitaji kugeuka kwa kiwiliwili chake.

Hivyo hatupaswi kuwaogopa, kuwachukia bundi ama kuongea vibaya juu yao. Hao ni viumbe vya Mungu kama walivyo njiwa, kondoo, v n.k. Wao ni kazi ya Mungu. Hivyo kuongea vibaya juu ya bundi ni kuongea vibaya juu ya kazi ya Mungu na hiyo kumpa shetani nafasi ili hofu izidi kutawala miongoni mwa watu. Kwa hiyo tunapowaona bundi tuna wajibu wa kumpa Mungu SIFA NA UTUKUFU!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda ndiye ndege anaetisha zaidi duniani.sitaisahau siku ile nimemuona bundi juu ya mti.nikachuma kakao na kumrushia mara kadhaa lakini hakuruka.nikajua amelala.nikapanda juu ya mti kumfuata nimpige na fimbo lakini kilichonikuta sitasahau kwani nilipomsogelea alifumbua macho nikastuka sana na kujiachia na kudondoka.nikavunjika mguu na mkono.bundi anatisha.namwogopa sana.bundi wa kyela wana aina mbili za kulia.nduuuuuuu na pisupinsulu unkukuu.wa kike ana sauti nyembamba huku dume anatoa base.bundi hawalii hovyo na akilia mara nyingi kuna tokea msiba.au mkila chakula kitamu kama nyama anatokea.bundi hapendi matusi hivyo ukimtukana anakimbia.pia anaogopa sana moto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mtu mmoja wizara ya pesa alikua anajitia mnoko na mfitini sana. Basi kuna mtu kachukua bundi hai. Kamvunja miguu na mabawa akiwa hai na kumfunga kitambaa chekundu mguuni na kilemba cheusi kichwani halafu kwa siri kubwa akavitumbukiza kwenye droo ya mnoko. Mbona palichimbika bila jembe mpaka mnoko akahamishwa idara.
 
Walimkomesha

Haha umenifurahisha sana hapo kwenye milio yao.

Ilikuwa usiku ulipotaka kumpiga?

Bundi wote madume na majike yote yanasauti base sema jike si base sana ila ya liyo na sauti unayosema pisupinsululu hao yawezekana bado wadogo kiumri na hawajafikia umri wa kua matured vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inamaana wewe humjui bundi? Hebu Google OWL. Kumbuka sura iNatisha UNaweza kuweweseka usiku
Labda yawezekana hamjui sishangai. Kuhusu sura ile si kwamba anatisha ila kwa jinsi umbo la kichwa chake na manyoya yaliyozunguka kichwa/uso (unaotisha) vinamsaidia yeye kwa namna moja au nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mtu mmoja wizara ya pesa alikua anajitia mnoko na mfitini sana. Basi kuna mtu kachukua bundi hai. Kamvunja miguu na mabawa akiwa hai na kumfunga kitambaa chekundu mguuni na kilemba cheusi kichwani halafu kwa siri kubwa akavitumbukiza kwenye droo ya mnoko. Mbona palichimbika bila jembe mpaka mnoko akahamishwa idara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Picha ya kusapoti uzi
Huyo bwana mdogo
images%20(2).jpeg
images%20(1).jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeanza kumchukia sana Bundi ilibidi siku ile aondoke na kiti yeye akaleta uzembe eti
 
Back
Top Bottom