Fahamu yaliyojiri ziara ya dc Hapi Kinondoni leo

Fahamu yaliyojiri ziara ya dc Hapi Kinondoni leo

Egnecious

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2015
Posts
899
Reaction score
999
FAHAMU YALIYOJIRI ZIARA YA DC HAPI KINONDONI LEO TAR 28/9/2017

BUNJU A BARABARANI

*Mkuu wa wilaya alisimama kuzungumza na wafanyabiashara wa barabarani ambapo waliomba eneo/nafasi sokoni ili waondoke barabarani wanakofanyia biashara.

*Wafanyabiashara waeleza juu ya eneo la kiwanja cha soko kinachodaiwa kupewa mtu binafsi na kujenga shule binafsi.

*DC Hapi ameagiza Mkurugenzi kumpatia taarifa juu ya kiwanja hicho na kumtaka mmiliki wake kufika kwake akiwa na nyaraka zote za umiliki.
*Aidha DC amewataka wafa
Wafanyabiashara hao kwenda kwenye soko la Bunju B ambako kuna nafasi.

BUNJU B SOKONI

*DC Hapi amezindua choo cha kisasa cha soko kilichojengwa na manispaa ya Kinondoni kama sehemu ya uboreshaji wa soko hilo.

*Choo hicho kina matundu 12, 7 ya wanawake, 5 wanaume, mabafu mawili, vyumba viwili vya walemavu na sehemu 7 za haja ndogo kwa wanaume (urinals).

*DC amekagua ujenzi wa machinjio ya kisasa unaoendelea sokoni hapo itakayokua na uwezo wa kuandaa kuku zaidi ya 1500 kwa siku.

*Maboresho yaliyofanyika sokoni hapo ni kujengwa Choo, machinjio, huduma ya maji na umeme na kuhakikisha daladala zinapita sehemu iliyotengwa sokoni.

BUNJU B MKUTANO

*DC Hapi amefanya mkutano wa hadhara kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.

*Mkuu wa wilaya amewataka wafanyabiashara wanaofanya biashara barabarani kinyume cha sheria kuhamia sokoni ndani ya siku 14, kwani hoja zao zote walizotoa zimefanyiwa kazi na maboresho yamefanyika na yanaendelea kufanyika sokoni.

*DC Hapi amemtaka Mkurugenzi wa manispaa, RPC, uongozi wa soko na wafanyabiashara hao kukaa pamoja na kutekeleza agizo hilo kwa wakati.
IMG-20170928-WA0023.jpg

IMG_20170928_195740_064.jpg
 
Asimama kuongea Kama Nani? Copy and paste hizi za viongozi zitatuponza
 
Hii I'd inakawaida ya kujipigia promo
 
Wakati anasoma Udsm alijulikana kama Salum sasa hapi alipata wapi? Na alikuwa kada na mnazi wa ccm na muongozaji mkubwa wa migomo pale rev. Square kama sikosei
 
Back
Top Bottom