Fahamu vitimbi vya majini na hila zao

Fahamu vitimbi vya majini na hila zao

Joined
Aug 26, 2018
Posts
5
Reaction score
2
A,aleykum warahmatullah wabarakatu naam kwa wale wafuatiliaji wa darsa zangu nadhani hawatakuwa na ugeni na namna ambavyo ninavyowachambua Majini na Wachawi lakini pia habari kuhusu Nyota,Ndoto n.k leo naendelea kuzungumzia vitimbwi vya majini na hila zao

KUNA AINA NGAPI ZA MAJINI
Kimsingi kuna aina 2 za majini

(1)MAJINI WAOVU hawa ni wale ambao wamekiuka njia za mola wao na wakafanya mambo ambayo hayampendezi mola wao mfano kuwasababishia watu madhara mbali mbali,kuwatia maradhi,kuwavunjia ndoa,Kuwaharibia kazi au biashara, Kuwafunga watu vizazi n.k kiufupi hawa ni wale wanaoitwa MASHEITWANI WA KIJINI NA HAWA NDIO TUTAKAOANZA KUWAZUNGUMZIA


(2)MAJINI WEMA hawa ni wale ambao hawakai katika viwili wili vya watu na wala hawafanyi shughuli yoyote yenye kuhusiana na uchawi bali hawa hufanya ibada kwa mujibu wa namna ambavyo mola wao na wetu alivyowaamrisha na alivyotuamrisha.

TUNAUPATA WAPI UKWELI KUHUSU KUWEPO KWA MAJINI Swali hili linajibwa na ALLAH mwenyewe katika kitabu chake kitukufu qur-an (46:29)
(Wakumbushe tulipokuletea kundi la majini kuja kwako kusikiliza qur-an)

Lakini pia qur-an inaendelea kutueleza (Siku ya qiyama wataambiwa)Enyi makundi ya majini na wanadamu Je mitume hawakuwafikia miongoni mwenu kuwabainishia aya zangu na kuwaonyesha mkusanyo wa siku yenu hii ya leo?(6:130)
Aya hizi zinatosha kutueleza ama kutudhibitishia uwepo wa majini na zipo nyingi sana na panapo majaliwa yake KARIMA tutaendelea kuziona katika masomo yajayo

JE SHETANI NI NANI?

Wanazuoni wanakubaliana na kutuambia kwamba SHETANI ni tabia ya maasi atakayokuwa nayo jini au binadamu huyu ataitwa SHETANI

JE SHETANI KAZI YAKE NINI?MALENGO YAKE NI YAPI KWA BINADAMU endelea kuwa nami ili ujue anamuingiaje binadamu anampotezaje na anawezaje Jinni huyu kishetani kuzungumza kwa kutumia kinywa cha binadamu

KWA MASWALI ZAIDI WHAT UP 0757144465 Piga simu tuzungumze kwa no 0656228832 wakazi wa unguja Zanzibar sasa napatikani KIDMNI kwa KANDURU. Karibuni kwa ajili ya dua na visomo mbalimbali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
jini pesa nalitafuta sana ila naskia linataka kafara ni kweli shehe??
 
Majini ni usanii tu, naamini majini kweli wapo kwa mujibu wa Quran, ila siamini majini kuwaingia watu hasa wanawake na watu wa pwani. Huku mikoani kwetu ishu hizi ni chache sana, tena kwa wanawake. Hebu sheikh niambie kwanini majini wanawaingia watu wa pwani hasa wa jinsia ya ke?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe kuna majini wazuri wanaoswali na kumuomba Allah!

Shetani umesema ni tabia ya maasi anayokuwanayo jini au binadamu, kwa hiyo shetani sio kiumbe?
 
Hivi kwanini hili swala la majini kuwaingia watu haswa mabinti/ wakina mama lipo pwani sana au wanafwata bahari shekhe ebu tufafanulie.
 
Back
Top Bottom