Fahamu njia nzuri za kuondoa magadi (salts) shambani

Lasway.Jr

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
230
402
286527-saline-soil.jpg

FAHAMU NJIA NZURI YA KUONDOA MAGADI(SALTS) SHAMBANI
Katika mashamba mengi tatizo la udongo na ardhi kwa ujumla kujaa chumvi au magadi limekuwa tatizo kubwa kwa wakulima wengi kwani magadi au chumvi huleta madhara makubwa sana kwa mazao na hata mazao mengine hufa kabisa pale yanapooteshwa kwenye udongo wenye magadi mfano wa mashamba yalioadhirika ni Ndungu irrigation scheme,kitivo irrigation scheme, Dakawa,Kiroka na Mkindo irrigation scheme (Morogoro), Kinyasugwe scheme (Dodoma) pia baadhi ya maeneo ya Lower moshi,Mawala,Kikavu chini, na hivyo kufanya mashamba yalio na tatizo hilo yasitumike katika uzalishaji,makala hii itakusaidia kujua namna ya kurudisha ardhi ya shamba lako katika hali nzuri na kuzuia uwezekano wa magadi kuongezeka katika shamba lako na hii itaongeza uzalishaji kwani utaweza kuotesha mazao mengi na ya aina mbalimbali kama udongo wako utakuwa na hali nzuri ya kuupatia mmea wako maji na madini or (nutrients) za kuuwezesha kukua vizuri na kuzaa sana

AINA ZA MAGADI ZILIZOPO KWENYE UDONGO
Kuna aina nyingi za chumvichumvi zilizopo ardhini na huwa katika viwango tofauti kulingana eneo moja na lingine na tofauti hii husababishwa na asili ya udongo wa mahali husika chumvi hizi ni kama Sodium ambayo hupatikana kwenye chumvi ya kawaida(NaCl), Potasium, Boron,Magnesium, Calcium, Phosphorous madini mengine ni muhimu katika ukuaji wa mmea lakini kwa kiwango kinachotakiwa na huwa ni sumu endapo yatazidi kiwango chake

NAMNA AMBAVYO MAGADI HUDHOOFISHA MIMEA
Madhara yatokanayo ma magadi ni makubwa sana na huleta hasara kwa wakulima wengi sana, kitaalamu magadi huzuia mizizi ya mimea kufyonza maji kwenye udongo na kuufanya mmea kushindwa kukua kwani maji ni muhimu katika mfumo wa mimea kujitengenezea chakula chake hata kama utamwagilia maji ya kutosha katika shamba lenye magadi bado mimea haitaweza kupata maji hayo (salts induce water stress to crops through matrix forces build up between the soil particles and the salts ion and hinder plant water uptake via capillarity and osmosis). Pia magadi huharibu mfumo wa udongo(soil structure) na kuufanya udongo kuwa mgumu na kuzuia mizizi ya mmea kupenya vizuri kwenye ardhi na hivyo kupunguza udhabiti wa mimea iwapo shambani na kusababisha kuanguka angauka kwa mazao yanapofikia wakati wa kubeba matunda au maua kwani hukosa nguvu za kujishikilia kwenye ardhi na hali hii husababishwa sana uwepo na sodium nyingi shambani na mkulima hupata hasara kubwa sana.

VYANZO VYA MAGADI KWENYE UDONGO
  • Asili ya udongo wenyewe
Baadhi ya maeneo yana udongo wenye asili ya chumvi kwa Tanzania maeneo hayo yanapatikana kwa wingi dodoma na singida na hasa wakati wa kiangazi baada ya mvua kukatika unaweza ukaona kabsa mabonge ya chumvi ardhini

  • Maji yanatumika kwa umwagiliaji
Kuna baadhi ya maeneo maji yake huwa na chumvi kiasi kwenye mito na hapa chemichemi na wakulima hutumia maji kutoka kwenye vyanzo hivyo vyenye maji ya chumvi katika kumwagilia mashammba yao, hii huongeza chumvi kidogo kidogo kwenye ardhi na kama mwendelezo wa kutumia maji hayo utafanyika kwa miaka mitano basi shamba hilo litakuwa limejaa chumvi na halitafaa tena kwa kilimo endapo njia na mbinu stahiki hazitachukuliwa

  • Utumiaji wa mbolea za viwandani bila maelekezo ya kitaalamu
Tujue ya kuwa sio kila mbolea ya kiwandani inafaa kwenye kila aina ya udongo, pili tunapokuwa tunaweka mbolea shambani lazima tuwatumie wataalamu ili watupe vipimo sahihi vya uwekaji wa mbolea hizi ili ziwe kwa kiwango kinachotakiwa pasipo kuzidisha wala kupunguza , kila shamba lina rutuba tofauti na lingine kwa hiyo ata uwekaji wa mbolea utatofautiana, pia kila zao lila vipimo vyake vya kiasi cha mbolea kinachotakiwa, kumbuka ni muhimu kufuata ushauri wa wataalamu kabla ya kuweka mbolea shambani ili kuondokana na matatizo na uweze kuzalisha mazao yenye tija

  • Mfumo mbaya wa utoaji maji shambani(poor drainage system)
Tatizo hili ni kubwa sana hasa pale wakulima wengi wanapoamini kuwa katika kumwagilia shamba lazima aone maji yametuama ndio aridhike kuwa amemwagilia, hili ni kosa kubwa kwani tunatakiwa tujue kuwa mimea hufyonza maji yaliyo ardhini tuu(plants absorb water, and they don't drink water ......... Myth), maji yaliyotuama shambani hupandisha chumvi iliyopo chini kuja juu na baada ya ardhi kukauka chumvi ile hubakia juu ya ardhi na kuadhiri mimea

NJIA ZA KUONDOA MAGADI SHAMBANI
Hili ndilo lengo kuu la makala hii ili kumsaidia mkulima kuondokana na tatizo hili, nitaeleza njia za kitaalumu na za gharama nafuu za kuondoa na kupunguza magadi shambani.

  1. Kuzamisha chumvi(Leaching of salts)
Wakati wa kumwagilia shamba unashauriwa umwagilie maji mengi kiasi kuliko yale yanayotosheleza mmea wako ili maji hayo ya ziada yasaidia katika kuzamisha chumvi iliyoko juu wa udongo iende chini zaidi ambako mizizi ya mimea haifiki, njia hii lazima utumie wataalamu wa umwagiliaji (irrigation engineers) kama mimi ambao tutakusaidia kitaalamu kuendena na udongo wako na tutakuambia ni kiasi gani cha maji inatakiwa umwagilie katika shamba lako ili kuondoa chumvi na kusaidia mimea yako kukua (irrigation and leaching requirements)

2. Uwekaji wa Gypsum (Calcium Sulfate)

Gypsum hufanya kitu kinachoitwa neutralization ambapo hubadilisha chumvi iliyopo ardhini isilete madhara kwa mimea na katika maduka mengi ya pembejeo zinauzwa hizi gypsum kwa ajili ya mashamba ili kudhibiti chumvi na magadi lakini njia hii ni ya gharama kidogo

3. Utumiaji wa Samadi

Mbolea za wanyama na mimea husaidia sana kwenye kuongeza rutuba kwenye ardhi pia katika kuhakikisha na kupungiuza magadi kwenye udongo na njia hii matokeo yake ni polepole lakini ina uhakika na pia samadi ina faida nyingine nyingi katika kuimarisha udongo na kuongeza upatikanaji wa madini kwa mimea

4.Njia ya mafuriko (flooding)

Njia hii hufanywa katika maeneo yenye maji mengi na hasa kipindicha mvua , shamba lenye magadi hutifuliwa na kufurishwa au kumwagiliwa mpka maji yanatuama (wakati hamna mazao shambani) na baada ya hapo maji hutolewa kwa mifereji maalumu na maji hayo huchukua magadi katika shamba husika

NB. njia hii usiifanye kwenye mashamba yaliosongamana ili maji yaliyo na magadi yasiende kwenye shamba la jirani yako na kumpa hasara

5. Utumiaji wa njia za kisasa za kufanya umwagiliaji kama drip irrigation,sprinkler system hupunguza uwepo wa magadi kwenye udongo na kama unahitaji system hizi nitafute kwa mawasiliano mwishoni mwa makala hii

Lakini kwa maeneo ambayo yana magadi sana unashauriwa kupanda mazao yanayoshahimili ardhi yenye chumvi

mazao yanayoshahimili chumvi zabibu,mbaazi,Nanasi,Miembe hasa mazao ya miti ndio hushauriwa sana katika ardhi yenye magadi

mazao yasiostahimili udongo wenye magadi
Mahindi,Tikiti maji,Nyanya, Mbogamboga, na mengne mengi

fuata ushairi wa kitaalamu kabla ya kuanza kulima na kupanda
SOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI ZA KILIMO HAPA

Eng(T) Octavian Justine Lasway
Bsc irrigation and water Resources Engineering
Sokoine University of Agriculture(SUA)
Phone. 0763347985
Email . octavianlaswai@gmail.com

asante sana mkuu kwa elimu,dakawa irr.scheme ndipo kwenye shamba langu na kuna sehemu ina magadi,ngoja nitumie shule yako niongeze mavuno na kukuza kipato changu,ubarikiwe sana
 
QUOTE="ABDUL sungita, post: 16473306, member: 321329"]GARLICIDAL-Hii aina ya sumu itokanayo na vitunguu saumu+mafuta ya taa. Chukua v/saumu vikubwa 3, visage/vitwange kisha weka ndan ya mafuta ya taa lita 1 na uviache siku 2 kisha uchuje hayo makapi v/saumu. Kisha weka sabuni ya unga kijiko 1 cha chai, hapo sumu tayari kwa matumizi yako au biashara. Matumizi, lita 1 ya sumu kwa lita 10 za maji( Nimeanza ufugaji wa kuku wa kienyeji, bado sija survey soko la kuku wa kienyeji likoje.

Kama kuna mtu mwenye uzoefu na hili anishauri, pros and cons etc.

By the way, nimeanza na Jogoo mmoja, ila natarajia kuongeza kuku within a week, projections ni kuwa na kuku 1,000, hapo ndio nianze kuuza, matarajio yangu ni kuuza via interent - hapa nalenga watu wa DAR, ambao wako bize, I can do delivery maofisini within city center, na baadae kuweka vituo vya kufanya pickup wakati watu wanarudi home jioni, e.g Mwenge Junction, Morocco Petrol Station, etc. Malipo via M-Pesa, SMS banking pia na mahoteli.

Sitarajii faida ya haraka, naomba ushauri kwa wale walifanya biashara hii, au wanajua mtu wa karibu aliyeifanya.

). Na unyunyizie ktk mbogamboga na usichume baada ya siku 5 au 6.

kwa utengnezaji wa sumu zingne 067311461 au sungitaabdul@gmail.com, mafunzo ni kwa njia ya email.[/QUOTE]

Mkuu hiyo Hapo hakuna suala la cancer na imethibitishwa na UTAFITI(Scientific Researcher Council of Tanzania, P.O.BOX 221, DODOMA, TANZANIA)
 
Mkuu hapa kuna uzi jinsi ya kufuga kuku, uzi n wa ukweli, utafute ktk nyuzi zenye stick utafaidi zaidi.
 
286527-saline-soil.jpg

FAHAMU NJIA NZURI YA KUONDOA MAGADI(SALTS) SHAMBANI
Katika mashamba mengi tatizo la udongo na ardhi kwa ujumla kujaa chumvi au magadi limekuwa tatizo kubwa kwa wakulima wengi kwani magadi au chumvi huleta madhara makubwa sana kwa mazao na hata mazao mengine hufa kabisa pale yanapooteshwa kwenye udongo wenye magadi mfano wa mashamba yalioadhirika ni Ndungu irrigation scheme,kitivo irrigation scheme, Dakawa,Kiroka na Mkindo irrigation scheme (Morogoro), Kinyasugwe scheme (Dodoma) pia baadhi ya maeneo ya Lower moshi,Mawala,Kikavu chini, na hivyo kufanya mashamba yalio na tatizo hilo yasitumike katika uzalishaji,makala hii itakusaidia kujua namna ya kurudisha ardhi ya shamba lako katika hali nzuri na kuzuia uwezekano wa magadi kuongezeka katika shamba lako na hii itaongeza uzalishaji kwani utaweza kuotesha mazao mengi na ya aina mbalimbali kama udongo wako utakuwa na hali nzuri ya kuupatia mmea wako maji na madini or (nutrients) za kuuwezesha kukua vizuri na kuzaa sana

AINA ZA MAGADI ZILIZOPO KWENYE UDONGO
Kuna aina nyingi za chumvichumvi zilizopo ardhini na huwa katika viwango tofauti kulingana eneo moja na lingine na tofauti hii husababishwa na asili ya udongo wa mahali husika chumvi hizi ni kama Sodium ambayo hupatikana kwenye chumvi ya kawaida(NaCl), Potasium, Boron,Magnesium, Calcium, Phosphorous madini mengine ni muhimu katika ukuaji wa mmea lakini kwa kiwango kinachotakiwa na huwa ni sumu endapo yatazidi kiwango chake

NAMNA AMBAVYO MAGADI HUDHOOFISHA MIMEA
Madhara yatokanayo ma magadi ni makubwa sana na huleta hasara kwa wakulima wengi sana, kitaalamu magadi huzuia mizizi ya mimea kufyonza maji kwenye udongo na kuufanya mmea kushindwa kukua kwani maji ni muhimu katika mfumo wa mimea kujitengenezea chakula chake hata kama utamwagilia maji ya kutosha katika shamba lenye magadi bado mimea haitaweza kupata maji hayo (salts induce water stress to crops through matrix forces build up between the soil particles and the salts ion and hinder plant water uptake via capillarity and osmosis). Pia magadi huharibu mfumo wa udongo(soil structure) na kuufanya udongo kuwa mgumu na kuzuia mizizi ya mmea kupenya vizuri kwenye ardhi na hivyo kupunguza udhabiti wa mimea iwapo shambani na kusababisha kuanguka angauka kwa mazao yanapofikia wakati wa kubeba matunda au maua kwani hukosa nguvu za kujishikilia kwenye ardhi na hali hii husababishwa sana uwepo na sodium nyingi shambani na mkulima hupata hasara kubwa sana.

VYANZO VYA MAGADI KWENYE UDONGO
  • Asili ya udongo wenyewe
Baadhi ya maeneo yana udongo wenye asili ya chumvi kwa Tanzania maeneo hayo yanapatikana kwa wingi dodoma na singida na hasa wakati wa kiangazi baada ya mvua kukatika unaweza ukaona kabsa mabonge ya chumvi ardhini

  • Maji yanatumika kwa umwagiliaji
Kuna baadhi ya maeneo maji yake huwa na chumvi kiasi kwenye mito na hapa chemichemi na wakulima hutumia maji kutoka kwenye vyanzo hivyo vyenye maji ya chumvi katika kumwagilia mashammba yao, hii huongeza chumvi kidogo kidogo kwenye ardhi na kama mwendelezo wa kutumia maji hayo utafanyika kwa miaka mitano basi shamba hilo litakuwa limejaa chumvi na halitafaa tena kwa kilimo endapo njia na mbinu stahiki hazitachukuliwa

  • Utumiaji wa mbolea za viwandani bila maelekezo ya kitaalamu
Tujue ya kuwa sio kila mbolea ya kiwandani inafaa kwenye kila aina ya udongo, pili tunapokuwa tunaweka mbolea shambani lazima tuwatumie wataalamu ili watupe vipimo sahihi vya uwekaji wa mbolea hizi ili ziwe kwa kiwango kinachotakiwa pasipo kuzidisha wala kupunguza , kila shamba lina rutuba tofauti na lingine kwa hiyo ata uwekaji wa mbolea utatofautiana, pia kila zao lila vipimo vyake vya kiasi cha mbolea kinachotakiwa, kumbuka ni muhimu kufuata ushauri wa wataalamu kabla ya kuweka mbolea shambani ili kuondokana na matatizo na uweze kuzalisha mazao yenye tija

  • Mfumo mbaya wa utoaji maji shambani(poor drainage system)
Tatizo hili ni kubwa sana hasa pale wakulima wengi wanapoamini kuwa katika kumwagilia shamba lazima aone maji yametuama ndio aridhike kuwa amemwagilia, hili ni kosa kubwa kwani tunatakiwa tujue kuwa mimea hufyonza maji yaliyo ardhini tuu(plants absorb water, and they don't drink water ......... Myth), maji yaliyotuama shambani hupandisha chumvi iliyopo chini kuja juu na baada ya ardhi kukauka chumvi ile hubakia juu ya ardhi na kuadhiri mimea

NJIA ZA KUONDOA MAGADI SHAMBANI
Hili ndilo lengo kuu la makala hii ili kumsaidia mkulima kuondokana na tatizo hili, nitaeleza njia za kitaalumu na za gharama nafuu za kuondoa na kupunguza magadi shambani.

  1. Kuzamisha chumvi(Leaching of salts)
Wakati wa kumwagilia shamba unashauriwa umwagilie maji mengi kiasi kuliko yale yanayotosheleza mmea wako ili maji hayo ya ziada yasaidia katika kuzamisha chumvi iliyoko juu wa udongo iende chini zaidi ambako mizizi ya mimea haifiki, njia hii lazima utumie wataalamu wa umwagiliaji (irrigation engineers) kama mimi ambao tutakusaidia kitaalamu kuendena na udongo wako na tutakuambia ni kiasi gani cha maji inatakiwa umwagilie katika shamba lako ili kuondoa chumvi na kusaidia mimea yako kukua (irrigation and leaching requirements)

2. Uwekaji wa Gypsum (Calcium Sulfate)

Gypsum hufanya kitu kinachoitwa neutralization ambapo hubadilisha chumvi iliyopo ardhini isilete madhara kwa mimea na katika maduka mengi ya pembejeo zinauzwa hizi gypsum kwa ajili ya mashamba ili kudhibiti chumvi na magadi lakini njia hii ni ya gharama kidogo

3. Utumiaji wa Samadi

Mbolea za wanyama na mimea husaidia sana kwenye kuongeza rutuba kwenye ardhi pia katika kuhakikisha na kupungiuza magadi kwenye udongo na njia hii matokeo yake ni polepole lakini ina uhakika na pia samadi ina faida nyingine nyingi katika kuimarisha udongo na kuongeza upatikanaji wa madini kwa mimea

4.Njia ya mafuriko (flooding)

Njia hii hufanywa katika maeneo yenye maji mengi na hasa kipindicha mvua , shamba lenye magadi hutifuliwa na kufurishwa au kumwagiliwa mpka maji yanatuama (wakati hamna mazao shambani) na baada ya hapo maji hutolewa kwa mifereji maalumu na maji hayo huchukua magadi katika shamba husika

NB. njia hii usiifanye kwenye mashamba yaliosongamana ili maji yaliyo na magadi yasiende kwenye shamba la jirani yako na kumpa hasara

5. Utumiaji wa njia za kisasa za kufanya umwagiliaji kama drip irrigation,sprinkler system hupunguza uwepo wa magadi kwenye udongo na kama unahitaji system hizi nitafute kwa mawasiliano mwishoni mwa makala hii

Lakini kwa maeneo ambayo yana magadi sana unashauriwa kupanda mazao yanayoshahimili ardhi yenye chumvi

mazao yanayoshahimili chumvi zabibu,mbaazi,Nanasi,Miembe hasa mazao ya miti ndio hushauriwa sana katika ardhi yenye magadi

mazao yasiostahimili udongo wenye magadi
Mahindi,Tikiti maji,Nyanya, Mbogamboga, na mengne mengi

fuata ushairi wa kitaalamu kabla ya kuanza kulima na kupanda
SOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI ZA KILIMO HAPA

bofya hapa chini
www.greenagricultureskills.blogspot.com

Eng(T) Octavian Justine Lasway
Bsc irrigation and water Resources Engineering
Sokoine University of Agriculture(SUA)
Phone. 0763347985
Email . octavianlaswai@gmail.com

Mazao ya mboga mboga pia yako yanayofaa kwenye ardhi yenye magadi mfano beet root ,sema njia zako nzuri saaana tatizo ni pale kama magadi / chumvi iko kwenye maji unayonyeshea hapo unajinsi zaidi ya kubadilisha zao au kubalisha maji
 
asante sana mkuu kwa elimu,dakawa irr.scheme ndipo kwenye shamba langu na kuna sehemu ina magadi,ngoja nitumie shule yako niongeze mavuno na kukuza kipato changu,ubarikiwe sana
asante sana , kwa upande wa dakawa unaweza kunitafuta nipo morogoro
 
Mimi nna shamba langu, na sehemu nilipo kuna maji ambayo yana chumvi chumvi, je ni vipi naweza tumia haya maji nisipate madhara??

Je utumiaji wa njia kama drip kwenye umwagiliaji wa maji yenye chumvi chumvi hautaweza pelekea kuziba kwa sehemu za kutolea maji??

Je ni vipi utumiaji wa drip au sprinkler utapelekea utoaji wa chumvi kwenye shamba langu??
 
Mimi nimekuwa na tatizo la magadi shambani kwangu. Nilifanya research na kugundua kuwa source ya maji nayomwagilizia ndiyo ilikuwa na chumvi/ magadi.

Kwakuwa nilikuwa nafuga samaki niliacha kutumia maji yale na nikawa natumia maji yaliyomo kwenye bwawa la samaki pekee. Matokeo yalikuwa mazuri na ya hali ya juu.

Baadaye niligundua kuwa kinyesi cha samaki ambacho kina high content ya amonia ambayo hubadlika kuwa nitrate na baadye nitrogen hufanya kazi kubwa ku neutrize chumvi/ magadi. Na hya maji huwa na bacteria pamoja na trace elements ambazo husaidia ukuaji wa mimea.

Kwa sasa nafanya kilimo kwa kutumia mbolea ya kutoka kwenye bwawa la samaki na mazao yanapendeza sana.

d7653a87d0e35a234451b671c1d19468.jpg
 
Majibu

maji yenye chumvi huwa yana madhara sana kwenye ardhi hasa kwenye udongo pale unapoyatumia kumwagilia na madhara yake ni kidogokidogo yataonekana even ten years lakini hapa nitakueleza njia za kumwagilia kwa kutumia maji yalio na chumvi kiasi na sio ile chumvi iliyozid sana (maji yalio na chumvi iliyozid hayafai kabsa katika umwagiliaji )
cha kufanya cha kwanza ni kupanda mazao yanayoweza kuvumilia uwepo wa chumvi kwenye udongo , cha pili kulingana na udongo wako katika kumwagilia kwako lazima umwagilie extra water to meet leaching requrement ili uweze kuzamisha chumvi iliyo juu iende deep chini kabsa ardhini depend on your crop root zone(root depth), cha tatu lazma utumie mbolea za samadi na composte manure sana kwenye shamba lako , mwsho kabsa nakushaur kila mwaka uwe unaapply gypsum mara moja kwa ajili ya kufanya nutralization ukifanya ivo madhara yatakuw kidogo sana

Je utumiaji wa njia kama drip kwenye umwagiliaji wa maji yenye chumvi chumvi hautaweza pelekea kuziba kwa sehemu za kutolea maji??

Ningependa ujue kuwa maji yenye chumvi hayafai kabsaa nasititiza hayafai kabisa kutumika kwenye drip irrigation system na kama kuna mtu alikufanyia design ya drip na hakuanagalia maji yako kama yana chumvi alafu mwshoni ukakuta yana chumvi nenda kamshitaki kwa sababu katika Irrigation engineering hicho kitu hakitakiwi
pili njia ya micro irrigation pekee amabayo unaweza kuitumia kwa maji ya chumvi ni sprinkler , na ukitumia sprinkler then fuata maelekezo kama hapo juu

Je ni vipi utumiaji wa drip au sprinkler utapelekea utoaji wa chumvi kwenye shamba langu??

hapana utumiaji wa drip na sprinkler hauwezi kuondoa chumvi shambani bali utumia wa njia hizi unasaidia chumvi kutokujijenda shambani (yaan zinazuia inbuilt in salts) kama nilivyoeleza hapo awali kuwa unaweza kuanza na shamba vzr kabsa halina chumvi lakn baada ya miaka kadhaa chumvi ikaanza kutokea na hii inatokana na poor design of irrigation system , kwa hyo ukitumia drip na sprinkler itasaidia kwan designer lazma afanye design in such a way that chumvi haitajijenga ardhini

Lasway Octavian J
Bsc Irrigation and Water resources Engineering
0763347985
Octavianlaswai@gmail.com
www.greenagricultureskills.blogspot.com

Green Agriculture Team
One Drop,More Production
we are to save you
 
Keep up the good work ,watanzania tujifunze profession za watu kuziheshimu ,yaan kama unataka kujenga green house nenda kampuni husika fuata ushauri hizi short cuts zitatumaliza ,haswa watu wa pwani na dar es salaam kuna shida sana ya maji ya chumvi utalaumu green house haifai kumbe shida maji yalo na hukifiata itaratibu ,any investment ya hela nyingi basi usikurupuke ,ahsanteni
 
Mimi nimekuwa na tatizo la magadi shambani kwangu. Nilifanya research na kugundua kuwa source ya maji nayomwagilizia ndiyo ilikuwa na chumvi/ magadi.

Kwakuwa nilikuwa nafuga samaki niliacha kutumia maji yale na nikawa natumia maji yaliyomo kwenye bwawa la samaki pekee. Matokeo yalikuwa mazuri na ya hali ya juu.

Baadaye niligundua kuwa kinyesi cha samaki ambacho kina high content ya amonia ambayo hubadlika kuwa nitrate na baadye nitrogen hufanya kazi kubwa ku neutrize chumvi/ magadi. Na hya maji huwa na bacteria pamoja na trace elements ambazo husaidia ukuaji wa mimea.

Kwa sasa nafanya kilimo kwa kutumia mbolea ya kutoka kwenye bwawa la samaki na mazao yanapendeza sana.

d7653a87d0e35a234451b671c1d19468.jpg
Safi sana
 
Mk

Mkuu unapatikana wapi?
 
Je ni vipi utumiaji wa drip au sprinkler utapelekea utoaji wa chumvi kwenye shamba langu??

hapana utumiaji wa drip na sprinkler hauwezi kuondoa chumvi shambani bali utumia wa njia hizi unasaidia chumvi kutokujijenda shambani (yaan zinazuia inbuilt in salts) kama nilivyoeleza hapo awali kuwa unaweza kuanza na shamba vzr kabsa halina chumvi lakn baada ya miaka kadhaa chumvi ikaanza kutokea na hii inatokana na poor design of irrigation system , kwa hyo ukitumia drip na sprinkler itasaidia kwan designer lazma afanye design in such a way that chumvi haitajijenga ardhini

Lasway Octavian J
Bsc Irrigation and Water resources Engineering
0763347985
Octavianlaswai@gmail.com
www.greenagricultureskills.blogspot.com

Green Agriculture Team
One Drop,More Production
we are to save you
Shamba lenye ukubwa wa hekari moja unaweza install sprinkler za shilingi ngapi mkuu?
 
Inategemea na vitu vifuatavyo
1.mazao unayotaka kulima
2.Je una maji kiasi gani
3. Unapenda sprinkler zako ziwe na mfumo gani (solid set, semi solid set, permanent system etc
Wasiliana na mm 0763347985
Mm ni mtaalam wa masuala ya umwagiliaji na maji
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom