Fahamu namna ya kuibua wazo la mradi (Community project plan)

The Consult

JF-Expert Member
Jan 20, 2017
220
252
img_3243.jpg

Uibuaji wa mradi (Project Plan) ni hatua ya mwanzo kabisa katika mradi. Katika hatua hii wazo la mradi ambalo linaenda kutatua tatizo huainishwa. Kumekuwepo na kasoro nyingi sana katika uibuaji wa mradi, na hii kupelekea miradi mingi kutatua matatizo ambayo kimsingi si matatizo halisi katika jamii husika (Not Real and Root Cause). Miongoni mwa kasoro zitokanazo katika hatua ya uibuaji wa mradi ni pamoja na kutotumia njia sahihi katika kutafuta wazo la mradi.

Mawazo ya mradi (Project Ideas) huweza kupatikana kwa njia/vyanzo mbalimbali; miongoni mwa njia hizo ni hizi zifuatazo;

Malengo katika mipango ya kitaifa (National plans/strategies). Mfano kwa Tanzania sasa tuna mpango wa kimaendeleo ujulikanao Long Term Perspective Plan (LTPP), 2011/12-2025/26 ambao ni njia ya kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo (TDV 2025), mpango huu yaani (LTPP) una lengo (Goal) la kuhakikisha Tanzania inakuja kuwa nchi ya Kipato Cha Kati ifikapo mwaka 2026. Mpango huu unatekelezwa kupitia Mipango ya Maendeleo ya Miaka Mitano (Five Years Development Plans) ambayo ni; FYDP 2010-2015 uliokuwa na lengo la kuchochea fursa za ukuaji (Unleashing potential growth), FYDP 2015-2020 wenye lengo la kuchochea Uchumi wa Viwanda (Nurturing an Industrial Economy) na FYDP 2020-2025 wenye lengo la kukuza mauzo ya nje na kujenga ushindani (Attaining export growth and competitiveness). Kila mpango hapa katika hii mipango ya miaka mitano mitano una malengo yake. Hivyo basi ili kupata wazo lako la mradi unapaswa kuangalia lengo katika mpango husika kisha utalifanyia tathmini (Problem/Idea analysis) katika ngazi ya kitaifa (Kwa maana ki-programu) mpaka ngazi ya kijamii (Kwa maana ki-mradi)

Mawazo kutoka kwa viongozi ngazi ya jamii (Ideas from local leaders). Kimsingi hawa watu wako na ufahamu mkubwa sana juu ya mazingira yao, na wanawafahamu watu wao pia. Hii inawafanya kujua matatizo mbalimbali ambayo yanakabili jamii zao. Hivyo unaweza kuwatumia watu hawa katika kuibua wazo la mradi.

Mawazo kutoka kwa wanajamii husika, wanajamii pia ni kama viongozi, wana uzoefu mkubwa na mazingira yanayowazunguka, hivyo wanafahamu nini kinaisumbua jamii yao. Endapo utatumia njia hii hivyo nao wanaweza kutumika katika kuibua wazo lamradi,ni vyema ukafahamu kwamba kwa kutumia njia hii utaorodheshewa matatizo lukuki, hivyo ni wajibu wako kufanya mapitio ya matatizo yote na kujua lipi haswa ni muhimu na lizingatiwe. Miongoni mwa vigezo utakavyotumia kuchagua wazo/tatizo ni kuangali ukubwa/kiwango cha tatizo husika (Magnitude), mahitaji ya rasilimali katika kukabiliana nalo (Resources needed). Kumbuka kutumia njia shirikishi (Participatory approach) katika uchujaji wa hayo matatizo.

Malengo/maeneo mahsusi (Thematic areas) katika miongozo ya wafadhili. Mara nyingi wafadhili wanapotoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi huweka maeneo (thematic areas) ambapo mradi husika ni lazima ujikite. Kulikuwa na mjadala kuwa kwa kiasi gani/kwa vipi maeneo mahsusi (thematic areas) ambayo yanaainishwa na wafadhili yanaendana na mipango ya Taifa husika ambako mradi unatekelezwa. Katika kuhakikisha maeneo mahsusi (Thematic areas) yanaendana na vipaumbele vya Taifa husika mradi unakotekelezwa mashirika ya Umoja wa Mataifa (UNs) na mashirika mengine makubwa kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakizingatia vipaumbele vya nchi husika kabla ya kuainisha maeneo ya mradi (thematic areas).

KUMBUKA : Matumizi ya njia yoyote kati ya hizo hapo juu yanahitaji utathmini wa tatizo ambalo umeligundua kutokana na wazo (Problem analysis) pia ushirikishwaji wa wadau (stakeholders involvement) lazima uzingatiwe ili kufanikisha utekelezaji wa mradi.


The Consult; +255 719 518 367
Dar es Salaam
Tanzania
 
mkuu. asante sana kwa shule yako iliyotulia hapo juu.

Naomba kama una idea ya namna ya kuanzisha non-profit NGO tafadhali nisaidie. mahitaji na taratibu za kisheria tafadhali.
natanguliza shukrani zangu.
 
mkuu. asante sana kwa shule yako iliyotulia hapo juu.

Naomba kama una idea ya namna ya kuanzisha non-profit NGO tafadhali nisaidie. mahitaji na taratibu za kisheria tafadhali.
natanguliza shukrani zangu.

Shukrani kwa pongezi
Angalia pdf doc hii, iko na taratibu za kuanzisha NGO.
 

Attachments

  • Taratibu_usajili_NGOs.pdf
    219 KB · Views: 202

Similar Discussions

Back
Top Bottom