clion dismas
Senior Member
- Aug 6, 2017
- 185
- 170
SOMO LA 23
AFYA YA MENO
clion odhiambo , contacts : odhiamboclion@gmail.com : BE BLESSED
Utangulizi
MENO YALIYOOZA YANATIBIKA.
Meno kuoza ni ugonjwa ambao umeathiri rika zote kwa sasa, si watoto wala watu wazima. Ni ugonjwa ambao kwa hakika mtu anajitengenezea mazingira ya kuupata, ni ugonjwa wa tabia.
KWA UFUPI
Tafiti nyingi ulimwenguni kama FDA na ADA za marekani, zimeonyesha uhusiano wa vyakula vya kusindikwa pamoja na maradhi ya meno. Chanzo kikuu cha meno kuoza, usababishwa na sukari inayozalishwa baada ya mmeng`enyo wa vyakula vya wanga inayopelekea bakteria aina ya Streptococcus mutans kushambulia afya ya kinywa na bakteria wengine wengi kufuatia kudhuru meno na kinywa. Sababu nyingine ni kama: Upungufu wa madini ( CHOKAA, FOSFORASI, MAGNEZIAMU) , upungufu wa vitamini kwenye vyakula( A,D,K), usafi wa meno usio sawa, vyakula vyenye winggi wa tindikali lakini pia tabia mbaya za mlo.
Sukari hii, hubadilishwa na bakteria walio kinywani na kusababisha tindikali. Ambapo hii tindikali utafuna madini ya chokaa yaliyo katika uso wa juu wa jino (enameli) na kusababisha kuoza kwa jino au meno.
FLORAIDI INA MCHANGO GANI?
Floraidi ni aina ya kampaundi asilia ( au ya kutengeneza) inayo patikana katika aina kadhaa za vyakula inayosaidia meno kuwa imara. Floraidi inapatikana kwa wingi katika miamba na udongo, pale maji yanapopita katika miamba uzalisha floraidi ayoni ambazo zinaingia katika miili yetu na kujenga maeneo ya meno na mifupa kwa ujumla. Tafiti zinaonyesha kwamba, watoto kwa asilimia 60 na watu wazima kwa asilimia 35 wanaotumia madini ya floraidi afya ya meno yao inakua bora Zaidi.
Baikaboneti (baking soda)
Ni aina ya chumvichumvi yenye asili ya alkali iliyo na uwezo wa kuzuia makuzi ya bakteria aina ya S.mutan na kufanya meno kuwa meupe. Katika Journal of Dental Hygiene, Vol. 79, No. 4, October 2005, imebaini jambo hili.Ukiamua kutumia kuswaki nayo, hakikisha huimezi, sukutua na uiteme. kwa sababu ya uwingi wa madini ya sodiamu na pia, mwili unazalisha baikaboneti unayoihitaji. uzuri ni kwamba, hii, sio sumu.
Haidrojeni perokisaidi ( hydrogen peroxide)
Ni aina ya kampaundi ambayo inauwezo wa kuzia lakini pia kuondoa utando wa njano kwenye meno kwa kuua bakteria jamii ya S. mutans. huu ni utofauti ambao upo kati ya bicarbonate na hii kampaundi. Journal of Dental Hygiene, Vol. 79, No. 4, October 2005 imeeleza kwamba pale ivi vitu viwili vinapotumika kwa pamoja matokeo bado ni yaleyale. Sodium Bicarbonate and Bicarbonate of Soda
Onyo Ni vyema ifahamike, baking soda inapotumika inaongeza madini mengi ya sodiamu mwilini ambayo uhusishwa na maradhi ya shinikizo la damu.kijiko kimoja cha chai kina gramu 1.259 za sodiamu ambazo ni nyingi. Kwa mtu asiye na maradhi ya shinikizo la damu la juu, kwa siku anashauriwa kutumia kiasi chini ya 2.3 gramu, aliye na maradhi , anatumia chini ya gramu 1.5.
Usitumie hii baikaboneti kama dawa labda kama tuu, tabibu wako amekuambia kufanya hivyo.
VYAKULA VYA KUTIBU MENO YALIYOOZA.
Zingatia, vyakula ndio suluhu ya kutibu meno yaliyooza. Tafiti zimeonyesha kwamba, baadhi ya vyakula vya asili vinaweza kuziba na kukuza tena sehemu ya jino iliyoliwa na bakteria. Navyo ni:-
1. Vyakula vyenye uwingi wa vitamin D na chokaa (Ca)
Tafiti ilifanywa uko jijini uingereza katika makundi matatu ya watoto wenye meno yaliyooza, 1.waliopewa vyakula vya nafaka na tindikali phytic 2. Walipewa chakula cha kawaida na vitamin D, 3. Walikula nafaka nzima, mbogamboga na matunda pamoja na vitamin D.
MATOKEO,
kundi la 3 walionyesha kupona kabisa ndani ya miezi 6, wakati kundi la 2 walikua na afadhali lakini kundi la 1 kuoza kuliongezeka.
2. Vyakula vyisivyo na sukari za kuongezwa
Sukari ina tindikali nyingi ambayo ndio chanzo kikubwa cha meno kuoza, ni chakula cha bakteria kinywani, jitahidi kutumia asali na matunda na sio sukari na vitu vyote vyenye sukari ya kuongeza kama pipi, soda, lambalamba na chokoleti.
3. Tumia lishe bora ya kila kitu asilia
vyakula vyote vyafaa vilivyoelezewa humu. Zingatia njia sahihi za mapishi ya vyakula asilia, rejea juu na usome MAHARAGWE YA SOYA.Lazima fahamike, hata chakula kizuri kinaitaji utaratibu wa kukiandaa ili kiweze kua bora.Lakini pia zingatia usafi wa kinywa, haya yote kuyafanya bila usafi wa kinywa ni sawa na bure. Sukutua kwa mafuta ya nazi na karafuu Tafiti zimeonesha kuwepo ahueni na kupona kabisa kwa kutumia njia hii. Vuta mafuta ya nazi kinywani, asubuhi na mapema, sukutua kwa dakika 10 hadi 20, tema mafuta, safisha kinywa kwa maji ya vuguvugu yenye chumvichumvi. Alafu sukutua kama kawaida, kwa kutumia dawa za asili.
WAZAZI/WALEZI
NI MUDA WA KUJIHOJI, TAFITI ZA AFYA ZINAONYESHA KWAMBA VITU VYENYE SUKARI NYINGI VINACHANGIA SANA KATIKA KUATHIRI UBONGO WA MTOTO. UPEO WAKE WA KUFIKIRIA, AKILI YAKE KWA UJUMLA PAMOJA NA UBONGO.
KWA SEHEMU KUBWA, WAZAZI TUNAWANUNULIA WATOTO WETU VITU VITAMU KAMA ZAWADI ZA WATOTO, KWA AJILI YA KUWAFURAHISHA KWA MUDA BILA YA KUFAHAMU YA KWAMBA TUNAWAATHIRI PIA. NIWASIHI NINYI MNAOWAPA WATOTO MALEZI, WAZOEZENI WATOTO VITU VIZURI VYA ASILIA KAMA MATUNDA PALE WANAPOKUA WADOGO ILI KIZAZI CHA KESHO KIWEZE KUWA KIZAZI CHENYE MANUFAA KATIKA TAIFA NA DUNIA KWA UJUMLA KIAFYA, KIAKILI LAKINI PIA KIROHO.
MAANDIKO YANASEMA:- “Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.” (Mithali 22:6)
JIHOJI: "Unamlea mtoto wako?"
Rejea
Center for disease control and prevention (CDC) American dental association (ADA) Fluoride in Water. THE INFLUENCE OF A CEREAL-FREE DIE RICH IN VITAMIN D AND CALCIUM ON DENTAL CARIES IN CHILDREN IT I BY MAY MELLANBY AND C. LEE PATTISON, M.B., B.S. (Pharmacology Department, University of Sheffield, and King Edward VII Hospital, Sheffield)