Fahamu machache kuhusu granite tile

Jan 20, 2022
32
31
FAHAMU MACHACHE KUHUSU GRANITE.
Na tiles Installation
INSTAGRAM @tiles_installation_team
0714 12 20 11
Karibu,

GRANITE(Itale)

Itale ni aina ya jiwe la asili ambalo limetengenezwa kutoka kwa magma baridi,
Granite imeundwa na madini kama vile quartz na feldspar, ambayo inachangia kuangaza kwake kwa tabia,
Yaani kama ukiweka granite kwenye sakafu ya nyumba yako itaakisi vitu vilivyo kuwa juu yake au pembeni yake,

GHARAMA YAKE

Shida inaanziaga hapa,
Wengi wanashindwa kumudu gharama yake kwasababu ni kubwa kiasi ukilinganisha na tile aina nyengine...

MUONEKANO WAKE

granite ni nzuri sana kwa muonekano na itafanya nyongeza ya kupendeza na ya kuvutia kwa sehemu yoyote ya nyumba yako. Granite inaonekana ya kifahari na ya kisasa,
Granite pia inaweza kuwa baridi chini ya miguu, kwa hivyo hii inaweza kutoa msaada mzuri majira ya joto katika hali ya hewa ya joto,

KUDUMU KWA GRANITE

Moja ya faida kubwa zaidi ya granite ni uimara wake wa kipekee. Hata kati ya chaguzi zote za sakafu za tile, ambazo tayari zinajulikana kwa muda mrefu wa maisha na muundo mgumu, granite ni ngumu zaidi na ya kudumu. Ikiwekwa vizuri, hautalazimika kuwa na wasiwasi juu ya granite kuchafuliwa na kubanduka au kuharibiwa na unyevu, na uso mgumu sana unamaanisha kuwa granite inakaribia kukosekana kwa mikwaruzo,
Sio rahisi kuchakaa sana hata sehemu yenye mzunguko mkubwa sana wa watu..
Pia granite ni rahisi mno kusafishika

UTUNZAJI WA GRANITE

Epuka kusafisha tile yako ya granite kwa madawa yenye kemikali sumu kwasababu hupelekea kupoteza ulemng'ao wake haraka sana hivyo hii itafanya kuzichoka tile zako,

ANGALIZO

Epuka kuacha tile zako na maji kwa muda mrefu kwani hizi granite huteleza mno hivyo ni hatari kwa afya yako,
Pia sio vyema kukanyaga tile za granite zikiwa na unyevu kwa nyayo za miguu yako moja kwa moja(haswa sehemu zenyebaridi kali sana wakati wa asubuhi au baada ya kuzisafisha kwa maji)
Ndio maana tunaona kunabaafhi ya watu wameweka utaratibu wa kuvaa viatu ndani ya nyumba iliowekwa sakafu ya granite
Japokuwa kwa hali yajewa yetu ya Tanzania sio ya baridi sana lakini hakikisha unavaa viatu/soksi angalau masaa mawili baada ya kusafisha tile kwa maji(kudeki)

Ahsante

NENO LA LEO

"Kumchukia mwerevu hakuwezi kukutoa katika ujinga"
Pia
"Kuelewa kipaji huwa kunahitaji kipaji"

Kwa ujenzi bora wa tiles na marble usisite kututafuta team ya tiles Installation

0714 12 20 11
Karibu sana tukuhudumie mteja wetu
Weledi na ubunifu katika kazi tunazingatia.

#NYUMBAyakoFAHARIyako
#IFANYEiweYAtofauti
#TUPEtuipandisheTHAMANI
#JENGAnasi

Tunahusika na
Ujenzi wa nyumba
Plaster decorations
Gypsum design
Rangi & Skimming
Tiles
Site Survey tunafanya kwa TZS 20,000/= tu
Tunakupimia
Tunakushauri kitaalam
Tunakusaidia kupata materials bora kwa gharama nafuu.
Tunakujengea kisasa.
Karibu tukufanyie kazi safi na bora kabisa
Tunapatikana Goba Dar es salaam
Popote tunakufikia

20220117_134201.jpg
View attachment 2089127
 
FAHAMU MACHACHE KUHUSU CERAMIC TILE

Na Tiles Installation

IG Tiles_Installation_

NI ZIPI CERAMIC TILE?
Ceramic tile ni zile tiles zote zinazonyonya maji kuanzia asilimia 6.9 na kuendelea (6.9%...)
Hizi zimetengenezwa kwa material mepesi zaidi...

AINA ZA CERAMIC TILE.
Kunaaina mbili za Ceramic tile....
1/Ceramic floor tile (Tile ya sakafu ya Ceramic)
2/Ceramic wall tile (Tile ya ukuta ya Ceramic)

CERAMIC FLOOR TILE
Hii inanyonya maji asilimia 6.9 mpaka asilimia 7.9(6.9%-7.9%)
Tiles hii ni nyepesi sana/sio ngumu hivyo ni vyema ukaijenga katika sakafu ambayo haina mzunguko mkubwa sana wa watu...
Mfano katika nyumba ya kuishi...
Epuka kujenga katika kumbi za mikutano,Bar,mashuleni n.k,
Kwani baada ya muda mfupi tuu zitakuwa zimechakaa zaidi na kupasuka (baadhi) kwa kuangushiwa vitu vizito na vigumu juu yake..
Pia hizi ni rahisi sana kuchubuka na kuweka mikwaruzo...

CERAMIC WALL TILE
Hizi ni tiles zote zinazonyonya maji kuanzia asilimia 7.9 mpaka asilimia 10(7.9%-10%)
Ndio chaguo bora zaidi kwa kuta za nyumba yako..
Kwasababu endapo utaiweka ukutani itakusaidia kupunguza unyevunyevu katika kuta zako kwani hii tile huwa inatabia ya kunyonya maji...
Na endapo itapunguza unyevu basi athari ya fangasi pia itapungua(haitakuwa kwa kiasi kikubwa sana)
Pia ni salama zaidi kwa kuzijenga ukutani kwasababu hizi tiles za Ceramic huwa zinashikana zaidi na udongo...
Hivyo hupunguza uwezekano wa tile kuanguka/kubanguka na kuleta madhara kwa wahusika wa eneo hilo....

FAIDA ZAKE KIUFUPI
1/Hizi tile ni gharama nafuu
2/Rahisi kubebeka/kuhamishika kutoka eneo moja kwenda jengine kwasababu ni nyepesi
3/Ni salama zaidi kwa ukutani

HASARA ZAKE KIUFUPI
1/Zinawahi kuchoka/kuharibika(haswa za sakafuni)
2/Sio rahisi kuiondoa baada ya kujenga kama itakuwa na hitilafu.
3/Ni rahisi kuvunjika/kupasuka

SPECIAL QUOTE

!!!! Ceramic tile ni chaguo bora zaidi kwa kuta za nyumba yako..
!!!! Ceramic tile ni gharama nafuu zaidi..
!!!! Ceramic tile ni rahisi zaidi kuchubuka,kupauka,kupasuka..
!!!! Ni vyema zaidi zikawekwa katika jengo lisilo na mzunguko mkubwa sana wa watu tofauti tofauti kama bar,ofisi,kumbi n.k

Mtag mwenzio ajifunze

KWA UJENZI BORA WA TILES USISITE KUITAFUTA TEAM YAKO YA KUAMINIKA YA TILES INSTALLATION

#NyumbaYakoFahariYako
#TupeTuipandisheThamani
#JengaNasi
Kwaniiii....
#UboraNdioFahariYetu

Tupigie sasa
0714 12 20 11

20220115_130019.jpg
tiles_installation_1621259339045830.jpg
FB_IMG_1630831785894.jpg
IMG20211117160936(0).jpg
IMG20210605173643(0).jpg
 
Granite tile size zote kwa maitaji..
Kwa maitaji nichek 0623152344
IMG_20220107_193026.jpg
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom