Fahamu kwa ufupi kuhusu International Space Station (ISS); kituo cha anga cha kimataifa

Mkuu, Shukrani kwa kutupatia elimu juu ya ISS, naomba niulize; kwakuwa jamaa huko huwa wanakula mara 3 je haja zao huwa wanazihifadhi vipi au wana zi dispose vipi??.

Juu ya sex, umesema kwamba hakuna ushahidi wa jambo hilo kufanyika, je kama ushahidi utapatikana kutatokea nini??
Kuhusu kuhifadhiwa kwa haja kuna kipande kimoja ambacho ni maalum kama tank katika muunganiko wa kituo hicho.
kuhusu swali lako la pili. Inawezekana endapo Ushahidi ukiwepo wataweka wazi jambo hilo mkuu.
 
Kifaa gani kitasababisha uone vizuri
Nafikiri unaongelea muonekano wa hicho kituo huko angani kati ya siku hizo itakapoonekana??
Jibu ni; Itaonekana kama nyota fulani kubwa kiasi kwa kuitazama kwa macho ila kwa kifaa maalumu itaonekana kama kilivyo.
 
Kuhusu kuhifadhiwa kwa haja kuna kipande kimoja ambacho ni maalum kama tank katika muunganiko wa kituo hicho.
kuhusu swali lako la pili. Inawezekana endapo Ushahidi ukiwepo wataweka wazi jambo hilo mkuu.


Hicho kipande "tank" la kuhifadhi hizo haja, baada ya kuzihifadhi zinapelekwa wapi??--- mfano septic tank za nyumbani zikijaa tunakodi gari la kunyonya na kwenda kumwaga huko mbali baadaye huo uchafu hubadilika na kuwa harmless normal matter, sasa vipi kwa hizo haja au huwa wakirudi duniani wanarudi nazo kama mzigo kwa ajili ya tafiti zingine za kisayansi, si tunajua mambo ya wazungu !!!🤣
 
Hicho kipande "tank" la kuhifadhi hizo haja, baada ya kuzihifadhi zinapelekwa wapi??--- mfano septic tank za nyumbani zikijaa tunakodi gari la kunyonya na kwenda kumwaga huko mbali baadaye huo uchafu hubadilika na kuwa harmless normal matter, sasa vipi kwa hizo haja au huwa wakirudi duniani wanarudi nazo kama mzigo kwa ajili ya tafiti zingine za kisayansi, si tunajua mambo ya wazungu !!!🤣
Sijajua watapeleka wapi. Kwa nini nimesema 'wata'? Kwa sababu hakijawahi kujaa na wanasayansi waoishi huko angani sio wengi na wanapokezana kwa kila baada ya miezi 6. Waliokuwepo angani hurudi duniani na kuwaachia wengine waendeleze mission.
 
UPDATE
=======

Ikiwa siku ya jumamosi 30 may 2020 space X kampuni ya roket iliyoanzishwa na Elon Musk ilirusha angani roket inayokwenda kwa jina la FALCON 9 ikiwa na crew members / wanaanga wawili kutoka NASA.

Kabla ya siku ya jumamosi kuisha, toka chombohewa (spacecraft) kuondoka katika uso wa dunia iliweza kufika katika katika orbit na kuungana kikamilifu na International Space Station (ISS) kwa mara ya kwanza katika safari yake.

Dragon crew waliosafiri:

-ROBERT L. BEHNKEN
-DOUGLAS G. HULEY
*wataekuwepo space mpaka ifikapo mwezi November mwaka hii.

->Picha ya wanaanga waliowasili siku ya jumamosi (waliovalia t-shirt nyeusi) na wenyeji wao.
31astronauts4-mobileMasterAt3x.jpg
 
Mbona hao wanaoneka ni wazembe tu,kuna mmarekani alika siku 275 na mwenzake Wa urusi alika Siku
205
INTERNATIONAL SPACE STATION (ISS)

Ni kituo anga za juu cha kimataifa kinachojihusisha na maswala mbalimbali ya kisayansi juu ya tabia anga na mswala ya anga za juu kwa ujumla. Kituo hichi kipo katika mzunguko wa chini wa anga Dunia. Mara nyingine huweza kuonekana kwa macho kikiwa angani kutoka duniani lakini kiking'aa kama nyota itembeayo kwa mwendo wa wastani. Mwendo wake kikiwa angani hufikia mpaka zaidi ya 27,590km/h. Programu ya ISS ni mradi wa ushirikiano wa kitaifa kati ya wakala watano wa shirika zinazoshirikiana kama: NASA, Roscosmos, JAXA, ESA, na CSA.

MAISHA KATIKA ISS
. Wakati wa kukaa kwao kwenye Kituo cha Angani cha Kimataifa cha Space (ISS) lazima waendelee kuishi na kufanya kazi katika mazingira ambayo ni tofauti sana na ile hapa Duniani. ... Hii inamaanisha kuwa wanaanga wanapaswa kuhifadhi rasilimali kama vile maji na chakula na taka zinahitaji kutunzwa kwa kiwango kidogo.Aina hizo za vyakula ni pamoja na mboga zilizohifadhiwa na vyakula kavu kama biscuti, chakula cha jokofu, matunda na bidhaa za maziwa. Leo, orodha ya vyakula kwenye Kituo cha Nafasi cha Kimataifa inajumuisha vitu zaidi ya 100.

CHAKULA.
Wanaanga huchagua menyu yao ya kila siku kwa muda mrefu kabla ya kuruka kwenye nafasi. Kuna milo mitatu kwa siku, pamoja na vitafunio ambavyo vinaweza kuliwa wakati wowote.

SEX/KUJAMIIANA
"Hakuna ushahidi rasmi au usio rasmi kwamba kulikuwa na matukio ya kujamiiana au kufanya majaribio ya kijinsia katika nafasi anga."

MICHEZO
"Alikadhalika wanaanga wa kituo cha sayansi ya anga ya kimataifa (iss) hawawezi kuwa na chaguzo za michezo huko angani kutokana na tafiti zilizowapeleka, lakini ili wasiwe wakiwa, wanaweza kucheza michezo michache katika chumba maalum kati ya vyumba vilivyomo katika chombo hicho cha anga. Michezo hiyo ni kama basket ball isiyohusisha mivutano ya asili (gravitational force), kuendesha baiskeli na kurusha boomerangs pamoja na aina ya mchezo wa golf.

WANAANGA WALIOPO ANGANI MUDA HUU KATIKA CHOMBO CHA ISS mpaka leo 29/05/2020

- Christopher J. Cassindy
Siku alizokaa angahewa: 53
-Anatoli Ivanishin
Siku alizokaa angahewa: 53
-Ivan Vagener
Siku alizokaa angahewa: 53

LINI UTAWEZA KUSHUGHUDIA ISS ANGA YA TANZANIA?

~ALHAMISI 11/0/20
Kuanzia 08:04:22
Mpaka 08:07:40
Na
19:44:47 mpaka 19:46:30

~IJUMAA 12/06/20
kuanzia 06:30:06 mpaka 06:31:56
na
Kuanzia 19:44:05 mpaka 19:47:23

~JUMAMOSI 13/06/20
Kuanzia 06:30:06 mpaka 06:31:56
na
Kuanzia 19:44:05 mpaka 19:47:23

~JUMAPILI 14/06/20
Kuanzia 18:56:39 mpaka 18:59:42

~JUMATATU 15/06/20
Kuanzia 06:29:39 mpaka 06:36:42
na
Kuanzia 19:45:46 mpaka 19:50:22

~JUMANNE 16/06/20
Kuanzia 05:42:41 mpaka 05:48:10
na
Kuanzia 19:03:14 mpaka 19:03:49

~JUMATANO 17/06/20
Kuanzia 04:57:26 mpaka 04:59:04
na
Kuanzia 06:31:18 mpaka 06:36:25View attachment 1462028View attachment 1462029
 
Ni kweli kuwa chombo hiki ni mali ya Urusi ?
Hapana! Ni mali iliyo chini ya ushirika wa mataifa mbalimbali. Ukiangalia mpaka chombo hicho chote kukamilika kuna nguvu imetumika kutoka mataifa kama USA, RUSIA,CHINA,INDIA, KOREA n.k na kila taifa kuna kifaa walichotengeneza (separately) katika nchi husika ,kikatumwa space kwa kutumia shuttle na kikaenda kuungwa kutengeneza chombo kamili.
 
Back
Top Bottom