Fahamu kuhusu watoto njiti (Premature babies)

Fahamu kuhusu watoto njiti (Premature babies)

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,881
Reaction score
6,377
NINI MAANA YA MTOTO KUZALIWA NJITI?

Watoto njiti ni wale ambao huzaliwa kabla ya wiki 37 za ujauzito. Inakadiriwa watoto Milioni 15 huzaliwa kabla ya muda kila mwaka duniani, ikimaanisha kati ya watoto 10 mtoto 1 ni njiti

Mwaka 2018, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ilitoa takwimu zilizoonyesha kuwa, 13% hadi 17% ya watoto wote wanaozaliwa hapa nchini wanazaliwa wakiwa njiti

Inapotokea Mtoto amezaliwa kabla ya muda mwili wake unakuwa mdogo zaidi na baadhi ya viungo vyake vikiwemo ubongo, moyo, mapafu na figo vinakuwa havijakomaa ipasavyo

Kwa mujibu wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC), kadri mtoto anavyozaliwa mapema ndivyo hatari ya kupoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu inavyoongezeka

Shirika la Afya (WHO) linasema watoto kuzaliwa wakiwa njiti ni tatizo la ulimwengu mzima na takriban watoto Milioni 1 hufariki kila mwaka kutokana na changamoto za kiafya zinazosababishwa na kuzaliwa kabla ya wakati

FAHAMU BAADHI YA SABABU ZA MAMA KUJIFUNGUA MTOTO NJITI

Kuna sababu mbalimbali zinazopelekea Mama kujifungua kabla mtoto ambaye hajatimiza wiki 37 tumboni. Baadhi ni kama ifuatavyo:

1. Umri mdogo wa Mama unaweza kupelekea ajifungue kabla ya miezi tisa kutimia. Hii ni kwasababu maumbile yao yanakuwa hayapo tayari kubeba mtoto

2. Magonjwa au maambukizi aliyonayo Mama yanaweza kuathiri ujauzito na kusababisha ajifungue mtoto wake mapema

3. Lishe duni. Ni muhimu kuzingatia lishe bora kabla na baada ya kupata ujauzito, Mama anaweza kujifungua mtoto njiti akikosa virutubisho muhimu ikiwemo Madini ya Chuma (Iron)

4. Msongo wa mawazo. Matukio kama kifo cha mtu wa karibu au unyanyasaji nyumbani yanaweza kupelekea mtoto kuzaliwa njiti

5. Uvutaji sigara, madawa ya kulevya na unywaji pombe ni sababu nyingine ambazo husababisha wakinamama kujifungua watoto njiti

JINSI YA KUWATAMBUA WATOTO NJITI (PRE-TERM BABIES)

Kwa kuangalia tarehe ya kwanza mama alipoziona siku zake za mwisho,kama muda huo ni chini ya wiki 37 basi mtoto huyo atakuwa njiti(pre –term baby)

Hata hivyo njia hii haitumiki saana kutokana na sababu kuwa akinamama wengi hawakumbuki kwa usahihi tarehe ya siku ya kwanza kuona hedhi yake ya mwisho(wrong date),

Ngozi ya Mtoto Njiti inakuwa kama inanata mfano wa ngozi iliyopakwa mafuta mazito kama vile grisi ama kimiminika kama asali

Chuchu Breast nodule za mtoto njiti hazionekani vizuri wakati za mtoto aliyetimiza muda chuchu zinaonekana vizuri

Mtoto njiti hana mistari inayopatikana viganjani na miguuni(Sole creases)

FAHAMU BAADHI YA CHANGAMOTO ZINAZOMKABILI MTOTO NJITI

Mtoto Njiti hawezi kuhimili maisha kama ilivyo kwa mtoto aliyezaliwa kwa wakati. Hii ni kwasababu anakuwa mdogo na viungo vyake bado havijakomaa

Watoto wanaozaliwa kabla ya kutimiza wiki 37 tumboni kwa Mama wanakumbwa na changamoto mbalimbali zikiwemo:-

1. Matatizo ya kupumua: Watoto Njiti wanaweza kuwa na changamoto ya kupumua hivyo punde tu baada ya kuzaliwa, wanatakiwa kupatiwa huduma ya kwanza ya kupumulia

2. Hawezi kuhimili baridi: Mtoto Njiti anatakiwa awe kwenye chumba chenye joto la kutosha. Pia, punde anapozaliwa, anatakiwa kukaushwa na kufungwa nguo zitakazosaidia kumpa joto

3. Maambukizi: Watoto hawa wana hatari kubwa ya kupata maambukizi kwasababu kinga yao ya mwili haijakomaa. Ni muhimu kuzingatia usafi kuanzia katika mazingira anayozaliwa

4. Vilevile, Mtoto Njiti anaweza kushindwa kunyonya vizuri hivyo atahitaji msaada ikiwa ni pamoja na kumkamulia maziwa kwenye chombo kisafi. Wengine hulazimika kupewa chakula kupitia mirija

5. Mara nyingi mishipa ya damu ya Mtoto njiti ni laini na kuna uwezekano mkubwa wa kuvilia damu na hata mishipa kupasuka wakati anazaliwa au baada ya kuzaliwa. Endapo hali hiyo itatokea, inaweza kusababisha ubongo wa Mtoto kushindwa kufanya kazi inavyotakiwa

Taarifa Zaidi:

1600936685564.png


1600936733885.png
 
Watoto njiti ni wale ambao huzaliwa kabla ya wiki 37 za ujauzito. Inakadiriwa watoto Milioni 15 huzaliwa kabla ya muda kila mwaka duniani, ikimaanisha kati ya watoto 10 mtoto 1 ni njiti

Mwaka 2018, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ilitoa takwimu zilizoonyesha kuwa, 13% hadi 17% ya watoto wote wanaozaliwa hapa nchini wanazaliwa wakiwa njiti...
Nini huwa sababu za mtoto kupelekea kuzaliwa njiti??
 
nini huwa sababbu za mtoto kupelekea kuzaliwa njiti??
Preterm birth occurs for a variety of reasons. Most preterm births happen spontaneously, but some are due to early induction of labour or caesarean birth, whether for medical or non-medical reasons.

Common causes of preterm birth include multiple pregnancies, infections and chronic conditions such as diabetes and high blood pressure; however, often no cause is identified. There could also be a genetic influence. Better understanding of the causes and mechanisms will advance the development of solutions to prevent preterm birth.
 
I gave birth to a premature baby na Hizo sababu zilizokuwa mentioned hapo sikuwa na yoyote nadhani sometimes inatokea tu.

Kwa nchi niliyozalia madaktari wa watoto wanajaribu Sana kuokoa maisha yao, they will try their best. Ila Ni ngumu as mother ukiingia huko NICU looking at your tiny baby unawaza Kama kweli atakuja Kuwa mkubwa Yani unaskia tu kulia. Our paed alikuwa akiwaita "Little fighters".

Lakini Kama mama akijifungua huko vijijini au hata baadhi ya hospital za wilaya hakuna nyenzo Kama incubator, Oxygen, feeding tubes Ni ngumu kuokoa maisha yao wengi wa watoto wanapoteza maisha. Very Sad
 
Waja wazito kuleni vizuri
especially matunda na mboga
Juice kama zote na supu zaa kila aina (sio za box)
Kumuomba Mungu kila wakati
 
I gave birth to a premature baby na Hizo sababu zilizokuwa mentioned hapo sikuwa na yoyote nadhani sometimes inatokea tu...
Nilimppteza mtoto wangu kwaajili ya ukosefu wa vifaa tiba. Hospital za serikali zinachangamoto sana. Hakukua na incubator zaid ya mashine moja ya oxygen watoto mapacha unawaweka kwa zamu yaan bas tu
 
Back
Top Bottom