• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Fahamu kuhusu Virusi vya Corona - China

MalcolM XII

MalcolM XII

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2019
Messages
407
Points
1,000
MalcolM XII

MalcolM XII

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2019
407 1,000
CORONA VIRUS ni virusi vinavyotokea kwenye familia iitwayo Coronaviridae, na vimepewa jina hilo kutokana na muonekano wake wa "Crown-like projection" chini ya light microscope.

Virusi hivi vinaathiri moja kwa moja mfumo wa upumuaji wa binadamu ambapo huweza kupelekea matatizo kwenye mfumo wa upumuaji (Respiratory Tract Infection), especially, "Common Cold"

Pia unatajwa kama ni ugonjwa wa pili unaosababisha atypical pneumonia, baada ya ule unaosababishwa na Rhinovirus

Inasemekana huko China, kwenye mji wa Wuhan, kati ya watu 10, watu 5 wanaweza kukutwa na maambukizi ya hivi virusi.

CHANZO
- Ugonjwa huu unaosababishwa na virusi aina ya coronavirus na unaaminika kuanzia China kwenye mji wa Wuhan.

JINSI UGONJWA UNAVYOSAMBAA (Mode of Transmittion)
Mwanzoni ilikuwa inaaminika kuwa ugonjwa huo umetokea kwa wanyama walioathirika na hivyo virusi (Mfano, Ngamia na Ng'ombe) lakini baadae ikaja kufahamika zaidi kuwa ugonjwa umejikita kwa mtu na mtu (person-to-person transimittion) kupitia:

1. Air transmission (Infective air droplets). Kwa mfano, muathirika anapokohoa ni rahisi kupata vimelea kama ukiwa karibu kwa njia ya hewa.

2. Kugusana moja kwa moja (Direct Contact) na muathirika

DALILI
• Homa (Fever)
• Kikohozi cha mara kwa mara (Cough)
• Kuumwa kichwa (Headache)
• Pia inaweza kupelekea Shortness of breath

KINGA NA MATIBABU
1. KINGA (Vaccination)

Mpaka sasa, hakuna chanjo iliyogundulika kwa ajili ya kutibu hili tatizo. Bado wanasayansi wanaendelea kulifanyia kazi.

Ilikuwa inaaminika kuwa huenda chanjo kwa ajili ya mafua (Flu Vaccine) ingeweza kusaidia kwa kuwa zote zinapelekea Common Cold, lakini kwa bahati mbaya kinga hiyo haijaweza kusababisha tofauti yoyote.

2. MATIBABU

Kama ilivyo kwa magonjwa mengine ya virusi. Hakuna matibabu sahihi ya virusi.
Kwahiyo dawa zitatolewa kutokana na dalili zitakazojitokeza.

NAMNA YA KUZUIA/KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI
- Kama ni muathirika unashauriwa kufunika mdomo na pua wakati wa kukohoa kwa kitambaa safi kuepusha kusambaza vimelea

- Osha mikono yako mara kwa mara kwa sabuni na maji yanayotiririka

- Epuka kugusana na mtu alieathirika

- Epuka kujifanyanga kwenye mkusanyiko mkubwa wa watu (Overcrowded Areas)

- Vaa viziba uso (Mask). Huwenda vikasaidia kupunguza maambukizi

- Wahi kwenye vituo vya afya mapema tu unapoona dalili zinaanza kujitokeza.
 
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Messages
53,065
Points
2,000
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2010
53,065 2,000
Huu ugonjwa utaua sana Wachina na si ajabu ukaenea zaidi kwingineko duniani...

Wachina ni moja ya jamii ya watu wachafu wasiojali afya, hivyo tutarajie takwimu za wagonjwa na wafu kuongezeka kama serikali yao haita act haraka...

Ninawaonea tu huruma Watanzania na waafrika kwa jumla waliopo Wuhan maana jiji la Wuhan lipo kwenye karantini, hakuna kutoka wala kuingia...

Wuhan inaweza ikawa ndio mji wenye Watanzania wengi nchini China baada ya Guangzhou, wengi wakiwa ni wanafunzi...
 
MalcolM XII

MalcolM XII

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2019
Messages
407
Points
1,000
MalcolM XII

MalcolM XII

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2019
407 1,000
Miaka ya nyuma nilikuwa nafikiria, hii population kubwa ya watu nchini China kuna ugonjwa utazuka tu ambao utalenga kuipunguza population yao.

Mambo hayo huwa yanafanywa na mazingira kupitia sheria ya Natural Selection.

Ndio kinachotokea sasa hivi.
 
Alvajumaa

Alvajumaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2018
Messages
2,910
Points
2,000
Alvajumaa

Alvajumaa

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2018
2,910 2,000
Huu ugonjwa utaua sana Wachina na si ajabu ukaenea zaidi kwingineko duniani...

Wachina ni moja ya jamii ya watu wachafu wasiojali afya, hivyo tutarajie takwimu za wagonjwa na wafu kuongezeka kama serikali yao haita act haraka...

Ninawaonea tu huruma Watanzania na waafrika kwa jumla waliopo Wuhan maana jiji la Wuhan lipo kwenye karantini, hakuna kutoka wala kuingia...

Wuhan inaweza ikawa ndio mji wenye Watanzania wengi nchini China baada ya Guangzhou, wengi wakiwa ni wanafunzi...
Aisee ni hatari sana, kuna rafiki yangu yupo kule

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sawima

sawima

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2019
Messages
1,059
Points
2,000
sawima

sawima

JF-Expert Member
Joined Jul 9, 2019
1,059 2,000
Miaka ya nyuma nilikuwa nafikiria, hii population kubwa ya watu nchini China kuna ugonjwa utazuka tu ambao utalenga kuipunguza population yao.

Mambo hayo huwa yanafanywa na mazingira kupitia sheria ya Natural Selection.

Ndio kinachotokea sasa hivi.
Yeah! Ni kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
lazalaza

lazalaza

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2012
Messages
2,794
Points
2,000
lazalaza

lazalaza

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2012
2,794 2,000
Dogo Yuko Wuhan sijui kitabu anakipigaje.
 

Forum statistics

Threads 1,405,606
Members 532,052
Posts 34,490,453
Top