Fahamu kuhusu Shambulio la 9/11 (September ,11 attack)

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Shambulio la 9/11, mwaka 2001, maarufu kama September ,11 attacks.

Hili ndio shambulio la kigaidi liliouwa watu wengi kwa mara moja katika historia ya dunia ,watu 2,977 walikufa na zaidi ya 25,000 walijeruhiwa ikiwemo majereha madogo na ya muda mrefu kama ulemavu.

Shambulizi lilitokea ndani ya nchi ya Marekani, katika majiji ya Newyork katika majengo mawili ya kibiashara maarufu kama Twins towers trade center katika mtaa wa Manhattan, Virginia, Arlington katika jengo la Pentagon, ofisi za Ulinzi za Marekani, na Kwenye viunga vya stony creek, Jimbo la Pennsylvania baada ya shambulio hilo lililopangwa kutekelezwa katika makao makuu ya serikali Washington DC kushindikana.

Mashambulizi hayo yalifanywa na kundi la kigaidi la Al_qaeda chini ya Osama, ambalo lilihusisha ndege 4 za boengi 757 na 767, za mashirika ya american airlines na United airlines baada ya kutekwa na magaidi hao punde baada ya kutoka viwanjani.

Mashambulizi yalitekelezwa asubuhi ya 2:46_4:28 , yalikuwa mashambulizi 4.

Baada ya watekaji kuteka ndege hizo wali waamuru marubani kubadili safari zao na kufuata maelezo yao ,ambao magaidi hao walidaiwa kuwa na mabomu na visu na kufanikisha kuwauwa abiria kadhaa walio onekana kupinga masharti.

Shambulizi lililo husisha ndege american airlines flight 11 na United airlines flight 175 ,ambazo zili gonga majengo mawili ya Twins towers, yenye ghorofa 110 kila moja ndio yaliyoleta maafa makubwa na kusababisha vifo zaidi ya watu 2000 na majeruhi wengi.

Ndege ya american airline flight 11 iligonga jengo la kaskazini muda wa saa 2:46 asubuhi, baadhi ya watu walio kuwa karibu walishuhudia tukio hilo, eneo liliwekwa ulinzi na waokoaji waliwasili na kuokoa watu ndani ya jengo hilo ambapo wale walio ghorofa za chini wengi waliokolewa lakini wale waliokuwa ghorofa za juu wengi wali kufa kutokana na moto na moshi ulio sababishwa na mafuta ya ndege, abilia wote walikufa na magaidi 5 wakiwa ndani ya ndege.

Vyombo vya habari duniani vilikuwa mubashara.

______
Tuchukue Break kidogo....

...
=====
Tunaendelea...

Shambulio la 9/11 , mwaka 2001.

Wakati vyombo vya habari vikiwa mubashara kutoka eneo la tukio, timu ya uokoaji na ulinzi ikiwa eneo la tukio, ilipofika saa 3:03 asubuhi ndege ya United airlines flight 175 awali iliyo kuwa ikielekea jijini Los Angeles California kabla ya kutekwa na magaidi wa 5, nayo iligonga ghorofa la kusini na kusababisha mlipuko mkubwa na hii mamia ya watu walishuhudia na kila mmoja alipo jua sasa kuwa ni shambulio, na kusababisha vifo vya watu wengi.

Haraka ulinzi uliimarishwa nchi nzima taazari ikatolewa hivyo ndege zote zilizo kuwa angani zilitua kwa dharura.

Lakini ndege mbili za merican airlines flight 77 na United airlines flight 93, zilipoteza mawasiliano Kwasababu nazo zilitekwa na baadaye abilia kazaa ambao walikuwa wakiwasiliana na ndugu zao kupitia mail voice, kuomba msaada nao walijulishwa kuhusu ajali za ndege mbili zilizo tokea Newyork.

Ilipo fika saa 3:37 asubuhi ,ndege ya american airlines flight 77, ili gonga katika jengo la makao makuu ya ulinzi wa Marekani pentagon, Virginia na kuharibu upande wa magharibi wa jengo hilo zaidi ya watu 200 walikufa ikiwemo abilia wote, magaidi 5 na wafanyakazi wa pentagon.

Na baada ya abilia wa ndege ya 4 ya United airlines flight 93, ambayo ilipangwa kwenda kuangushwa katika makao makuu ya serikali , Washington DC, katika jengo la Capitol, kujua na kusikia mashambulizi ya awali, basi abilia hao wali pambana na watekaji na baadaye wakiwa katika hatua ya kuwathibiti watekaji, mtekaji mmoja alimua rubani na kuiongoza ndege hiyo kuelekea chini na kugonga viunga vya stony creek, township Pennsylvania Mida ya saa 4:03 asubuhi abilia wote , watekaji wa 4 na wafanyakazi wandege wali kufa.

Baada ya kuungua maghorofa mawili ya world trade center yali poromoka .

Serikali moja kwa moja ili washtumu Al_qaeda lakini Osama alikana kuhusika mpaka mwaka 2004 ndipo alipo kubali kwa madai ya kwamba Marekani inatakiwa iwaondoe majeshi yake mashariki ya kati.
 
Wajomba wapo paradise saiz wanafaidi totoz bikira za huko.
 
Tena wanapewa nguvu za kula mizigo 300 na wana pewa 70 si mchezo
 
  • Thanks
Reactions: ibn
Back
Top Bottom