Fahamu kuhusu Principle of Natural Justice

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2015
Posts
1,446
Reaction score
3,319
FAHAMU KUHUSU PRINCIPLES OF NATURAL JUSTICE

Hapo zamani Mfalme alikuwa juu ya kila kitu katika nchi na alichokifanya kilihesabika kuwa ni sahihi, neno la mfalme lilikuwa sheria hakuna wa kupinga, baadaye mambo yalibadilika kukawepo sheria sasa mfalme anakuwa chini ya sheria, anatakiwa kufuata sheria kwa waingereza common laws. Angalau sasa kuna misingi mfalme anapaswa kuifuata na kuitii katiks kufanya maamuzi yake. Kutokea kwa Principles of natural justice ni kama namna ya watu kukata rufaa, watu wasiporidhika na maamuzi ya wenye mamlaka wanakata rufaa kwa mamlaka ya juu zaidi, mamlaka ya juu zaidi ya mfalme yaweza kuwa nani? Mungu na sheria zake ama sheria za asili (natural laws) ambazo matendo ya mfalme yanapaswa kutokuzikiuka. Chombo chochote kile kinachotoa huduma kwa umma katika maamuzi yake yanayoathiri haki za watu kinapaswa kuzingatia principles of natural justice. Principles of natural justice huhusisha mambo mawili nayo ni haki ya kusikilizwa (right to be heard) na (rule against bias) ambayo ni msingi dhidi ya upendeleo.

Principles of natural justice ni haki ya msingi sana na ni haki ya kikatiba ambapo kwa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inapatikana katika ibara ya 13(6)(a), ni katika sehemu ya haki za binadamu ambazo huanzia ibara ya 12 mpaka 24 kwa URT constitution ya 1977.

HAKI YA KUSIKILIZWA

(The rule of fair hearing/ the right to be heard)

Kawaida inajulikana kwa kilatini kama Audi alteram partem pia omnipotency inherent kwa kiingereza no one should be condemned unheard. Misingi ya haki ya kusikilizwa inapatikana kutoka kwenye msingi kwa kilatini "qui alquid statuerit, parte inaudita altera aiuquum liset dixarit haud aiuquum facerit" ikiwa na maana kwamba yeyote anayefanya maamuzi yoyote au kutoa hukumu bila kuusikiliza upande wa pili hata kama amesema au amehukumu ukweli lakini kwa kutosikiliza upande wa pili hajafanya jambo lililo sahihi.
Lord Hewart aliwahi kusema kuwa jambo la msingi siyo tu haki itendeke bali ionekane ikitendeka.

Principle of natural justice ilianzishwa na Mungu mwenyewe ukisoma Biblia utagundua kuwa Mungu alizingatia haki ya kusikilizwa alipotoa hukumu kwa Adam na Eva baada ya kufanya kosa la kura tunda walilokatazwa, rejea kitabu cha Mwanzo 3;1-19. Bwana Mungu alipoona Adam na Hawa wamefanya kosa la kula tunda la mti waliokatazwa hakuwahukumu mpaka amewasikiliza alimwita Adam akamuuliza kama amekula matunda ya mti waliokatazwa Adam akajitetea kuwa ni yule mwanamke aliyepewa amemdanganya. Bwana Mungu akamwita Hawa naye akajitetea kuwa amedanganywa na nyoka. Mungu baada ya kuwasikiliza wote wawili ndipo akatoa hukumu kila mtu na hukumu yake kama ilivyoandikwa kwenye kitabu tajwa hapo juu!

Hii ni ishara kuwa principles of natural justice ni kitu ambacho hakijaanza leo bali kilianza na Mungu mwenyewe kwa kuwa Mungu ni muweza anaona sirini hakuwa na haja hata ya Kuwaita Adam na Hawa na kuwauliza kitu ambacho anakijua lakini alifanya hivyo na kuwapatia haki ya kusikilizwa ili si tu atende haki bali haki ionekane imetendeka. Hii leo hata ukikamatwa redhanded kama wengine wanavyoita lazima upewe haki ya kusikilizwa maana ndiyo utaratibu ulioanzishwa na kuwa developed na mahakama na pasipo kufuatwa kwa haki ya kusikilizwa maamuzi na hukumu huwa batili. Haki ya kusikilizwa huhusisha vitu vifuatavyo

1) Haki ya kupata notisi(Right to notice)

2)Haki ya kutoa ushahidi na kuleta mashahidi kama wapo.

3)Haki ya kuwa na mwanasheria wa kukuwakilisha.

4)Haki ya kupinga ushahidi unaotolewa na upande wa pili.

5)Haki ya kupewa sababu ya hukumu. Mtoa hukumu au uamuzi lazima aeleze sababu za kwanini amefikia uamuzi huo.

6) Anayesikiliza kesi ndiye anayetakiwa kutoa hukumu. Siyo kesi isikilizwe na mwingine halafu hukumu itolewe na mwingine hairuhusiwi.
 
Hivi Natura Justice ni nini kwa kiswahili ?
 
Back
Top Bottom