Msitari wa pambizo
JF-Expert Member
- Sep 25, 2014
- 2,888
- 4,902
Ukistaajabu ha Musa utayaona ya Firauni unaweza kusema hivyo. Na wahenga waliosema tembea ujionee hakika walikuwa sahihi.
Wiki iliyopita nilitembelea mkoani Kigoma wilaya ya Kibondo nilimsindikiza jamaa yangu kusalimia nyumbani kwao. Alikua akinieleza stori ambazo mwanzoni nilidhani ni hadithi za Abunuasi.
Siku moja aliniambia nimsindikize kwa mtaalamu mmoja ambaye alikwenda kumchanja dawa ya kidono. Mtaalamu anasema ukichanja dawa hiyo vitu kama panga, risasi, kisu, nondo na shoka ukipigwa vinadunda yani vitachana au kutoboa shati tu lakini kamwe mwilini haviingii.
Baada ya jamaa kuchanjwa dokta alisema ni sharti kutest dawa hiyo na aliijaribu mbele yangu kwa kumkata panga tena lililonolewa vilivyo sehemu ya chini ya kitovu mara tano na lilidunda. Trust me panga halikumkata jamaa, mpaka na mimi nikachukua nikakata panga halikuingia.
Jamani dawa hizi zipo siyo story yani zipo.