FAHAMU KUHUSU KIDONO: Dawa ya kienyeji inayozuia risasi, panga, shoka, kisu na nondo; havipenyi mwilini kamwe

Msitari wa pambizo

JF-Expert Member
Sep 25, 2014
2,884
4,897
Ukistaajabu ha Musa utayaona ya Firauni unaweza kusema hivyo. Na wahenga waliosema tembea ujionee hakika walikuwa sahihi.

Wiki iliyopita nilitembelea mkoani Kigoma wilaya ya Kibondo nilimsindikiza jamaa yangu kusalimia nyumbani kwao. Alikua akinieleza stori ambazo mwanzoni nilidhani ni hadithi za Abunuasi.

Siku moja aliniambia nimsindikize kwa mtaalamu mmoja ambaye alikwenda kumchanja dawa ya kidono. Mtaalamu anasema ukichanja dawa hiyo vitu kama panga, risasi, kisu, nondo na shoka ukipigwa vinadunda yani vitachana au kutoboa shati tu lakini kamwe mwilini haviingii.

Baada ya jamaa kuchanjwa dokta alisema ni sharti kutest dawa hiyo na aliijaribu mbele yangu kwa kumkata panga tena lililonolewa vilivyo sehemu ya chini ya kitovu mara tano na lilidunda. Trust me panga halikumkata jamaa, mpaka na mimi nikachukua nikakata panga halikuingia.

Jamani dawa hizi zipo siyo story yani zipo.
 
tashwishwi, Safi sana kwa ubunifu wa kutangaza!

Bila shaka wateja wa huduma hii utapata wengi sana, hivyo jitahidi uandae dawa ya kutosha iwe tayari tayari

Masaihost.com
Web designing and Web hosting solutions
 
Kuna jamaa mmoja mtu wa kigoma mtaani huku hivyo hivyo watu wanasema jamaa anayo dawa panga kwake halipenyi kabisa kwani kwnye matukio kapatwa matukio kibao ya kukatwa mapanga lakini hakuumia sehemu yeyote .
 
~ kidono kipo watu wanavyo sana ukichanjwa dawa yake kitu chochote chenye ncha Kali hakiingi mwilini iwe panga,shoka,kisu,sururu kwa lengo LA kumdhuru muhusika.

~ kuna VINGUTI hivi ndio baba lao mwenye vinguti akipandisha hasira hakuna Wa kumzuia labda mumtege kwa nyavu kama godzilla,anakuwa na nguvu nyingi sana...MTU Wa hivi anapiga MTU Wa aina yeyote,wajeda sijui wacheza kung fu huwa wanapigika kama watoto,baunsa kama mwarabu fighter anaweza kubinywa vidole na kimbaumbau mpaka mkojo ukamtoka.

Madawa haya yameshamiri sana maeneo ya yenye shughuli za uvuvi mkoani kigoma na mkoa Wa rukwa,asili yake ni nchini Kongo.
 
Back
Top Bottom