FAHAMU KUHUSU KIDONO: Dawa ya kienyeji inayozuia risasi, panga, shoka, kisu na nondo; havipenyi mwilini kamwe

Ukistaajabu ha Musa utayaona ya Firauni unaweza kusema hivyo. Na wahenga waliosema tembea ujionee hakika walikuwa sahihi.

Wiki iliyopita nilitembelea mkoani Kigoma wilaya ya Kibondo nilimsindikiza jamaa yangu kusalimia nyumbani kwao. Alikua akinieleza stori ambazo mwanzoni nilidhani ni hadithi za Abunuasi.

Siku moja aliniambia nimsindikize kwa mtaalamu mmoja ambaye alikwenda kumchanja dawa ya kidono. Mtaalamu anasema ukichanja dawa hiyo vitu kama panga, risasi, kisu, nondo na shoka ukipigwa vinadunda yani vitachana au kutoboa shati tu lakini kamwe mwilini haviingii.

Baada ya jamaa kuchanjwa dokta alisema ni sharti kutest dawa hiyo na aliijaribu mbele yangu kwa kumkata panga tena lililonolewa vilivyo sehemu ya chini ya kitovu mara tano na lilidunda. Trust me panga halikumkata jamaa, mpaka na mimi nikachukua nikakata panga halikuingia.

Jamani dawa hizi zipo siyo story yani zipo.
ungemuuliza huyo mganga, vp kama huyo jamaa aliyemfanyia hiyo dawa akakutana na virusi vya corona, vitatunda?
 
Nyie dawa yenu rahisi sana mbona! Ngoja nisiiseme mtauawa buree

Cc Smart911
Unachanja na kuna dawa unakunywa

Ahdante kwa ushuhuda mkuu. Watu wanadhani ni masihara
Kidono nimechanjia mwaka 1994 masharti yake sili nyanya chungu(ngogwe),matembele wala bamia.
tashwishwi, Mkuu hyo dawa ipo Nina jamaa yangu Ni muha alipigwa nondo ikapinda mbele yangu katika ugomvi ikabid washikaj wamuombe msamaha tu yaishe Mana aliwakusanya balaaaaa

kilicho akilini kitumie
Ni kweli kabsa na nishawahi ifanya nani sahihi kabsa. Sisi ilikuwa baada ya process unapewa kiwembe ukitafune kizima kizima alafu unalerwa mkuki au panga ukatwe nalo. Trust me, linadunda. tashwishwi,

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
~ kidono kipo watu wanavyo sana ukichanjwa dawa yake kitu chochote chenye ncha Kali hakiingi mwilini iwe panga,shoka,kisu,sururu kwa lengo LA kumdhuru muhusika.

~ kuna VINGUTI hivi ndio baba lao mwenye vinguti akipandisha hasira hakuna Wa kumzuia labda mumtege kwa nyavu kama godzilla,anakuwa na nguvu nyingi sana...MTU Wa hivi anapiga MTU Wa aina yeyote,wajeda sijui wacheza kung fu huwa wanapigika kama watoto,baunsa kama mwarabu fighter anaweza kubinywa vidole na kimbaumbau mpaka mkojo ukamtoka.

Madawa haya yameshamiri sana maeneo ya yenye shughuli za uvuvi mkoani kigoma na mkoa Wa rukwa,asili yake ni nchini Kongo.
Mkuu naomba uje inbox Kuna mjeda ananyemelea my wife nataka nitoe funzo,njoo inbobo
 
Kama ni hivo uyo mganga angekua na pesa sana. Icho ni kiinimacho
Pengine kweli maana wahehe wa zamani majemedari walikuwa hata ukiwaua kwa mikuki hawafi mpaka ujue pa kupiga eg.mmoja code yake ilikuwa kidole na yule aliyenyongewa kitanzini ilikuwa sharia amwagiwe maji kwanza
 
Ukistaajabu ha Musa utayaona ya Firauni unaweza kusema hivyo. Na wahenga waliosema tembea ujionee hakika walikuwa sahihi.

Wiki iliyopita nilitembelea mkoani Kigoma wilaya ya Kibondo nilimsindikiza jamaa yangu kusalimia nyumbani kwao. Alikua akinieleza stori ambazo mwanzoni nilidhani ni hadithi za Abunuasi.

Siku moja aliniambia nimsindikize kwa mtaalamu mmoja ambaye alikwenda kumchanja dawa ya kidono. Mtaalamu anasema ukichanja dawa hiyo vitu kama panga, risasi, kisu, nondo na shoka ukipigwa vinadunda yani vitachana au kutoboa shati tu lakini kamwe mwilini haviingii.

Baada ya jamaa kuchanjwa dokta alisema ni sharti kutest dawa hiyo na aliijaribu mbele yangu kwa kumkata panga tena lililonolewa vilivyo sehemu ya chini ya kitovu mara tano na lilidunda. Trust me panga halikumkata jamaa, mpaka na mimi nikachukua nikakata panga halikuingia.

Jamani dawa hizi zipo siyo story yani zipo.
Mkuu hiyo ipo hata ya kuchelewa kufa watu wanaongeza umri mtu anaoza nusu mwili lakini bado anaongea ,shida unaweza filisi family kwa matibabu na ukaitesa pia,hivo vitu vipo Sana huko home sweet home,December naingia huko kwa upako wa kimwili,
 
Back
Top Bottom