Fahamu Kuhusu Fedha za Mfuko wa Jimbo

Wolle Melkas Fernando

JF-Expert Member
May 4, 2016
218
297
Kama ulikuwa unasikia tu kuna Fedha za "๐Œ๐Ÿ๐ฎ๐ค๐จ ๐ฐ๐š ๐‰๐ข๐ฆ๐›๐จ," basi tuelimishane hapa na kuchangia hoja hii.
Kwanza fedha za mfuko wa Jimbo zimetokana na sheria namba 16 ya mwaka 2009 ambayo ilitungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutambua mfuko huo kama "Constituency Development Catalyst Fund" (CDCF) yaani kwa maana ya "Mfuko wa kuchochea Maendeleo ya Jimbo".

Lengo la fedha hizi katika mfuko huu ni kutekeleza miradi mbalimbali kwenye kata na vijiji, miradi ambayo huibuliwa na wananchi wenyewe kulingana na hitaji lao ndani ya eneo lao.

Fedha hizi hutolewa kila mwaka kwa kila Jimbo, na mthibitishaji wa kwanza kwamba fedha zimepokelewa huwa ni Mbunge wa Jimbo ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya mfuko wa Jimbo.
Kiujumla kamati ya Fedha za mfuko wa Jimbo huundwa na watu 6 hadi 7.

i) Mbunge -Mwenyekiti wa Mfuko
ii)Afisa mipango (W)-Katibu wa Mfuko
Wajumbe wa kamati ya mfuko wa Jimbo ni;
iii) madiwani wawili wanaotoka ndani ya Jimbo (mmoja ni lazima awe mwanamke)
iv) Watendaji wa Kata wawili wanaotoka ndani ya Jimbo.
v) Mtu mmoja kutoka Taasisi hai isiyo ya kiserikali kama yupo. Huyu huchaguliwa na kamati ya mfuko wa Jimbo yaani watu hao niliotangulia kuwaorodhesha ndio huwa wanapendekeza, na Mbunge anaamua kukubali au kukataa.

Kwa ujumla Mbunge ndio huwa anawateua Hawa watu wote kwamba ni nani atamfaa kufanya nae Kazi katika kupanga matumizi ya Fedha hizi. Mbunge ndiye mwenye sauti ya mwisho (last say) kuhusu fedha hizi zifanye kitu gani na kitu gani zisifanye.

Lakini sheria imetamka waziwazi kuhusu matumizi. Sheria imekataza kutumia fedha hizi kwa mbunge yeyote kutaka kujijenga kisiasa au kutumia kwenye sherehe za chama ama dini ama hafla zisizohusiana na miradi ya wananchi wa Jimbo husika. Hivyo mwananchi ana haki zote za kuhoji Fedha hizi zimetumika katika miradi ipi? Je miradi inaonekana? Je imekamilika? N.K.

Kwahiyo tukubaliane kwamba mwananchi yeyote mkazi wa Jimbo husika akihoji asisumbuliwe kwasababu sheria iko wazi kabisa na inaturuhusu.

Kabla ya kuhitimisha nieleze kwa ufupi kwamba fedha hizi hutofautiana viwango kulingana na vigezo vilivyowekwa kisheria. Lakini kuna asilimia 25 ya mgao wa sawa kwa sawa, hii kila Jimbo hupewa asilimia yote. Kisha kuna idadi ya watu ambayo inabeba 45% Jimbo likiwa na idadi kubwa ya watu wanaotakiwa kisheria basi hupewa asilimia yote. Kigezo kingine ni ukubwa wa Jimbo Kijiografia hapa kuna 10% na kuna 20% ambayo hutolewa kwa kuzingatia kiwango cha umaskini wa wananchi katika Jimbo husika, kama ni maskini wa kutupwa kabisa basi hupewa asilimia yote
๐Ÿ˜Š
.

Je, umewahi kujua Jimbo lako hupewa kiasi gani cha Fedha za mfuko wa Jimbo? Na je umewahi kuambiwa Zimetekeleza mradi gani? Mchango wa comment yako ndio utafanya tuendelee kufuatilia na kujua ukweli zaidi.

Wolle Fernando
 
Huku jimboni kwetu Kibakwe sijawahi kuambiwa hizi hela zinafanya kazi gani na mbunge wetu hatembelei jimbo letu wala kufanya mikutano ya hadhara kutuelezea hizo hela za jimbo zinaenda wapi.
 
Huyo mbunge wenu wa Kibakwe hana time na nyie, kuna maneno yake anasema hatampa mtu jimbo ila anamuandaa mtoto wake amrithishe, kwahiyo muongee vizuri na wajumbe mapema sana waje kufanya yao ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜„
 
Kama ulikuwa unasikia tu kuna Fedha za "๐Œ๐Ÿ๐ฎ๐ค๐จ ๐ฐ๐š ๐‰๐ข๐ฆ๐›๐จ," basi tuelimishane hapa na kuchangia hoja hii.
Kwanza fedha za mfuko wa Jimbo zimetokana na sheria namba 16 ya mwaka 2009 ambayo ilitungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutambua mfuko huo kama "Constituency Development Catalyst Fund" (CDCF) yaani kwa maana ya "Mfuko wa kuchochea Maendeleo ya Jimbo".

Lengo la fedha hizi katika mfuko huu ni kutekeleza miradi mbalimbali kwenye kata na vijiji, miradi ambayo huibuliwa na wananchi wenyewe kulingana na hitaji lao ndani ya eneo lao.

Fedha hizi hutolewa kila mwaka kwa kila Jimbo, na mthibitishaji wa kwanza kwamba fedha zimepokelewa huwa ni Mbunge wa Jimbo ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya mfuko wa Jimbo.
Kiujumla kamati ya Fedha za mfuko wa Jimbo huundwa na watu 6 hadi 7.

i) Mbunge -Mwenyekiti wa Mfuko
ii)Afisa mipango (W)-Katibu wa Mfuko
Wajumbe wa kamati ya mfuko wa Jimbo ni;
iii) madiwani wawili wanaotoka ndani ya Jimbo (mmoja ni lazima awe mwanamke)
iv) Watendaji wa Kata wawili wanaotoka ndani ya Jimbo.
v) Mtu mmoja kutoka Taasisi hai isiyo ya kiserikali kama yupo. Huyu huchaguliwa na kamati ya mfuko wa Jimbo yaani watu hao niliotangulia kuwaorodhesha ndio huwa wanapendekeza, na Mbunge anaamua kukubali au kukataa.

Kwa ujumla Mbunge ndio huwa anawateua Hawa watu wote kwamba ni nani atamfaa kufanya nae Kazi katika kupanga matumizi ya Fedha hizi. Mbunge ndiye mwenye sauti ya mwisho (last say) kuhusu fedha hizi zifanye kitu gani na kitu gani zisifanye.

Lakini sheria imetamka waziwazi kuhusu matumizi. Sheria imekataza kutumia fedha hizi kwa mbunge yeyote kutaka kujijenga kisiasa au kutumia kwenye sherehe za chama ama dini ama hafla zisizohusiana na miradi ya wananchi wa Jimbo husika. Hivyo mwananchi ana haki zote za kuhoji Fedha hizi zimetumika katika miradi ipi? Je miradi inaonekana? Je imekamilika? N.K.

Kwahiyo tukubaliane kwamba mwananchi yeyote mkazi wa Jimbo husika akihoji asisumbuliwe kwasababu sheria iko wazi kabisa na inaturuhusu.

Kabla ya kuhitimisha nieleze kwa ufupi kwamba fedha hizi hutofautiana viwango kulingana na vigezo vilivyowekwa kisheria. Lakini kuna asilimia 25 ya mgao wa sawa kwa sawa, hii kila Jimbo hupewa asilimia yote. Kisha kuna idadi ya watu ambayo inabeba 45% Jimbo likiwa na idadi kubwa ya watu wanaotakiwa kisheria basi hupewa asilimia yote. Kigezo kingine ni ukubwa wa Jimbo Kijiografia hapa kuna 10% na kuna 20% ambayo hutolewa kwa kuzingatia kiwango cha umaskini wa wananchi katika Jimbo husika, kama ni maskini wa kutupwa kabisa basi hupewa asilimia yote
๐Ÿ˜Š
.

Je, umewahi kujua Jimbo lako hupewa kiasi gani cha Fedha za mfuko wa Jimbo? Na je umewahi kuambiwa Zimetekeleza mradi gani? Mchango wa comment yako ndio utafanya tuendelee kufuatilia na kujua ukweli zaidi.

Wolle Fernando
Posho za vikao kwenye mfuko wa Jimbo Ni TSH ngapi? Wanakutana mara ngapi kwa mwezi?
 
Wabunge wengi wanazitamka tu na kuzitumia kujujenga kisiasa.
 
Back
Top Bottom