Fahamu kuhusu CCTV; Mitambo maalumu ya kuzuia wezi

the great wizard

JF-Expert Member
Dec 21, 2015
1,482
887
Kumekuwako na ongezeko la mahitaji ya mitambo maalumu ya kuzuia wezi ya CCTV siku za hivi karibuni kutokana na ukweli kwamba kumekuwa na ongezeko la watu wasio waaminifu katika jamii
CCTV ni mfumo ambao unajumuisha kamera ambazo zinauwezo wa kurekodi video pamoja na kifaa kinachoweza kuhifadhi video ambazo zimerekodiwa na kamera hizo ambacho kinaitwa DVR ama NVR.
diagram_analog_system.jpg

Zipo kamera za aina mbalimbali na maranyingi huchambuliwa kutokana na maumbo yake ama matumizi yake, katika uchambuzi wa maumbo zipo kamera za bullet ambazo zinaumbo kama la risasi na ambazo mara nyingi hufungwa madhingira ya nje. Aina nyingne kutokana na umbo ni kamera za dome ambazo hizi huwa na umbo la dome ambalo ni la mviringo kamera hizi mara nyingi hutumika katika maeneo ya ndani ya nyumba
images.jpg

Wakati mwingine kamera huchambuliwa kufuata matumizi yake katika kipengele hiki maanayake utapata kamera za aina mbili zile za kawaida na za kuzunguka ambazo huitwa PAN TILT ZOOM ama kwa kifupi PTZ. Kamera za kawaida ni zile ambazo ukiifunga basi huangalia eneo moja tu ambalo umeielekezea kwa wakati huo tuu wakati zile za PTZ zenyewe zinaweza kuzunguka pande tofauti na zinakuwa controlled kwa kutumia umeme.
images-1.jpg

Uchambuzi huu wa aina ya kamera bado haukutoshi wewe kuweza kwenda kununua kamera dukani maana bado itabidi ujue ni teknolojia gani ya kamera unataka kutumia, zipo teknolojia mbili kuu katika teknolojia ya kamera.

Kamera zinazotumia mfumo wa Analojia.
Kamera hizi hutumia waya mmoja wa ambao unabeba signal za data kutoka katika kamera hadi katika chombo cha kurekodia. Ingawa kamera hizi hazina garama kubwa ukiringanisha na teknolojia nyingine lakini zinakuja na gharama kwa sababu ni lazima ufanye mpango wa kuzipa umeme na hii inaweza kuongeza gharama.

Hii ni teknolojia ya zamani kidogo lakini bado inaweza kutumiaka hadi sasa kwa maana ni ya gharama za chini hasa kwa matumizi ya nyumbani.

Kamera zinazotumia mfumo wa IP.
Teknolojia ya IP ni teknolojia mpya ukilinganisha na teknolojia ya analojia, teknolojia hii inatumia waya za network kwa ajiri ya kusafirisha data ila katika nyakati nyingine zinaweza kutumika kusafirisha hata umeme wa kamera pia. Teknolojia hii ni ghari ukilinganisha na teknolojia ya analojia lakini inafaida nyingi zaidi.
 
Unaposena kuwa CCTV ni mtambo wa kuzuia wezi unakuwa hauko sahihi,kuzuia manaake ni kufanya tukio la wizi lisitokee, CCTV kiuhalisia ni mfumo tu wa kufuatilia mienendo mbalimbali, inaweza ikawa kwenye majumba, maofisini, mitaani, mabarabarani, kwenye migodi na sehemu nyinginezo.mfumo huu hauzuii wezi bali unakufanya wewe kufuatilia mienendo na kama ukiona mienendo hiyo unaitilia shaka basi unachukua hatua, na kama limefanyika tukio basi CCTV inaweza kukusaidia kuwabaini waliofanya hilo tukio, mfano wenzetu walioenselea wanefunga mifumo hii kwenye mitaa yao na mabarabarani, hivyo basi mifumo hii huwawezesha kufuatilia mambo na ama kuyazuia kama ni mabaya au kufuatilia wahusika kama tiyati tukio limefanyika.
 
Shukran sana mkuu kwa hii thread.

Unaweza kutuwekea bei ya aina hizo za camera na installation yake inagharimu kiasi gani?
 
Sasa zinazuia au ni kwamba wanaonekana wakifanya uhalifu?

Sehemu nyingi tu zina hizo cctv na waibaji wanaiba tu na cctv inawarekodi....kwenye you tube zipo video kibao za cctv zikionyesha vibaka wakiiba....ila sijui kama baadae wanaenda kudakwa ama la.
 
Kumekuwako na ongezeko la mahitaji ya mitambo maalumu ya kuzuia wezi ya CCTV siku za hivi karibuni kutokana na ukweli kwamba kumekuwa na ongezeko la watu wasio waaminifu katika jamii
CCTV ni mfumo ambao unajumuisha kamera ambazo zinauwezo wa kurekodi video pamoja na kifaa kinachoweza kuhifadhi video ambazo zimerekodiwa na kamera hizo ambacho kinaitwa DVR ama NVR.
diagram_analog_system.jpg

Zipo kamera za aina mbalimbali na maranyingi huchambuliwa kutokana na maumbo yake ama matumizi yake, katika uchambuzi wa maumbo zipo kamera za bullet ambazo zinaumbo kama la risasi na ambazo mara nyingi hufungwa madhingira ya nje. Aina nyingne kutokana na umbo ni kamera za dome ambazo hizi huwa na umbo la dome ambalo ni la mviringo kamera hizi mara nyingi hutumika katika maeneo ya ndani ya nyumba
images.jpg

Wakati mwingine kamera huchambuliwa kufuata matumizi yake katika kipengele hiki maanayake utapata kamera za aina mbili zile za kawaida na za kuzunguka ambazo huitwa PAN TILT ZOOM ama kwa kifupi PTZ. Kamera za kawaida ni zile ambazo ukiifunga basi huangalia eneo moja tu ambalo umeielekezea kwa wakati huo tuu wakati zile za PTZ zenyewe zinaweza kuzunguka pande tofauti na zinakuwa controlled kwa kutumia umeme.
images-1.jpg

Uchambuzi huu wa aina ya kamera bado haukutoshi wewe kuweza kwenda kununua kamera dukani maana bado itabidi ujue ni teknolojia gani ya kamera unataka kutumia, zipo teknolojia mbili kuu katika teknolojia ya kamera.

Kamera zinazotumia mfumo wa Analojia.
Kamera hizi hutumia waya mmoja wa ambao unabeba signal za data kutoka katika kamera hadi katika chombo cha kurekodia. Ingawa kamera hizi hazina garama kubwa ukiringanisha na teknolojia nyingine lakini zinakuja na gharama kwa sababu ni lazima ufanye mpango wa kuzipa umeme na hii inaweza kuongeza gharama.

Hii ni teknolojia ya zamani kidogo lakini bado inaweza kutumiaka hadi sasa kwa maana ni ya gharama za chini hasa kwa matumizi ya nyumbani.

Kamera zinazotumia mfumo wa IP.
Teknolojia ya IP ni teknolojia mpya ukilinganisha na teknolojia ya analojia, teknolojia hii inatumia waya za network kwa ajiri ya kusafirisha data ila katika nyakati nyingine zinaweza kutumika kusafirisha hata umeme wa kamera pia. Teknolojia hii ni ghari ukilinganisha na teknolojia ya analojia lakini inafaida nyingi zaidi.
Mkuu kwamfano izo camera za Analojia zinapatikana kuanzia shillingi ngapi naweza pata mkuu... maana nina mpango ofsini kwangu niweke.. Maana mwaka juzi nilivamiwa na majambazi wenye silaha za moto mapema kabisa hata sura hawakuziba na yale mavazi yakininja Camera ingekuwepo ingenisaidia sana...!!
 
Hivi nawezaje kuzipata data baada ya wezi kuchukua DVR baada ya kufanya tukio la wizi!!mfano nilikua natumia DVR ya Hkvision!""
 
Unaposena kuwa CCTV ni mtambo wa kuzuia wezi unakuwa hauko sahihi,kuzuia manaake ni kufanya tukio la wizi lisitokee, CCTV kiuhalisia ni mfumo tu wa kufuatilia mienendo mbalimbali, inaweza ikawa kwenye majumba, maofisini, mitaani, mabarabarani, kwenye migodi na sehemu nyinginezo.mfumo huu hauzuii wezi bali unakufanya wewe kufuatilia mienendo na kama ukiona mienendo hiyo unaitilia shaka basi unachukua hatua, na kama limefanyika tukio basi CCTV inaweza kukusaidia kuwabaini waliofanya hilo tukio, mfano wenzetu walioenselea wanefunga mifumo hii kwenye mitaa yao na mabarabarani, hivyo basi mifumo hii huwawezesha kufuatilia mambo na ama kuyazuia kama ni mabaya au kufuatilia wahusika kama tiyati tukio limefanyika.
Exactly Mkuu.

Nami pia nilitaka kumueleza hivyo.
 
c6c9d2b015977274713dab5661f3bde8.jpg
kwangu mimi hii motion detector ndio komesha ya wezi. Ukifunga darini na ndani ya jengo wakikatiza tu hizo kelele zake watajuta kusogelea hapo.
 
Kama mfuko unaruhusu ni vizuri kuwa na system mbili:
1. Intruder alarm
2. CCTV

Intruder itasaidia kuzuia wezi wasikuibie na CCTV itakusaidia kujua kilichotokea - yaani yenyewe haizui tukio lisitokee bali kukusaidia katika uchunguzi wa namna tukio lilivyotokea.

Lakini kiukweli ni kuwa unapoweka CCTV pekee inaleta changamoto kubwa kwa anayetaka kukuibia. Pia inadaidia kuleta nidhamu hata kwa wafanyakazi wako.

Kwenye Intruder unaweza weka sensors za aina mbali mbali kutegemea mazingira ya eneo husika na unachotaka kukilinda. Kwa mfano kama ni chumba unaweza weka motion sensor au unaweza weka ceiling sensor n.k. Unaweza weka sensor za mlangoni (door contact) na pia unaweza weka sensor za ukuta (wall sensor), n.k. Ukweli ni kuwa sensors ziko za aina nyingi ni wewe tu kuamua.

Changamoto kubwa ya CCTV iko kwenye namna ya kuwa na "real time backup". Nina maana kuwa wezi au majambazi wakifanikiwa kuingia ndani huku wakijua kuna CCTV system basi wataitafuta DVR na kuondoka nayo. Na hapo maana yake ndo "ujanja" hakuna tena kwa kuwa ndo roho ya mfumo wote. Kwa hiyo kama unaweza kuwa na DVR nyingine au computer sehemu nyingine na ukafanya "synchronisation" basi hapo utakuwa umepata tiba inayojitosheleza.

Kwa hiyo namalizia kwa kusema ni heri kuzuia tukio (Intruder alarm system) kuliko kuanza kuhangaika na uchunguzi baada ya kuibiwa (CCTV). Weka system zote mbili kwa pamoja.
 
Back
Top Bottom