Fahamu kuhusu artificial intelligence?

Fahamu kuhusu artificial intelligence?

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,293
Reaction score
2,620
FAHAMU KUHUSU ARTIFICIAL INTELLIGENCE ?

Neno artificial intelligence tunaweza sema ni "Akili bandia" ule uwezo wa teknolojia kufanya mambo mbalimbali ambayo kwa kawaida uhitaji kutumia uwezo wa akili kama wa binadamu kuweza kutambua vitu, watu, lugha , sauti , kufanya maamuzi, kujifunza, kutabiri, kutafsiri na nk.

Watu wengi wakisikia Artificial intelligence huwa wanafikiri inahusisha labda maroboti na teknolojia zenye nguvu zaidi kupindukia Ambazo mtu anafikiri kuwa hajawahi kutumia Kwenye Maisha yake.

AI Hipo Kwenye teknolojia kubwa pia ziko Kwenye teknolojia za kawaida kila siku Kwenye Maisha yetu.

Watu wengi duniani tunatumia mifumo hii ya artificial intelligence Kwenye Maisha yetu kila siku nazani [emoji3]umeshtuka kidogo sio relax , najua unatumia google , Instagram , Twitter , facebooks , bolt , kamera za simu , online payment, YouTube, Gmail nk

Mifano [emoji116][emoji880]

• 𝗬𝗼𝘂𝗧𝘂𝗯𝗲[emoji271]
Unapotizama au unapotafuta kitu huwa YouTube wanapendekeza kuangalia video nyingine zinatokea hivyo utaona wanakuletea video inayoendana na kitu ulichokitafuta apa AI inafanya kazi ya kukusaidia kutambua na kukusogezea video zinahusiana na unachokitafuta.

• 𝗸𝗮𝗺𝗲𝗿𝗮 𝘇𝗲𝘁𝘂 𝘇𝗮 𝘀𝗶𝗺𝘂 [emoji991]
Ukifungua kamera Kwenye simu Yako ukitaka kujipiga picha utaona kuna wakati Kuna msaada unakuja wa kuchagua effect ambayo inaenda na mazingira unayotaka kupiga picha au unapotaka kujipiga selfie utaona kitu kinatokea kuzunguka USO wako apa AI inatambua uwepo wa USO wako Kwenye kamera.

•𝗚𝗼𝗼𝗴𝗹𝗲 𝘀𝗲𝗮𝗿𝗰𝗵 [emoji361]
Unapotafuta kitu Kwenye Google mifumo ya Artificial Intelligence inakusaidia kuweza kukuletea majibu ya kile unachokitafuta ivyo google Utumia teknolojia ya Artificial Intelligence.

AI inatumika pia Kwenye masuala ya mawasiliano ,viwandani , Huduma za afya ,usalama , biashara , kilimo na nk.

Ebu tuachie maoni Yako ukisikia Artificial Intelligence ulikua unawaza kitu gani [emoji3] tuambie tujue ?

Teknolojia ni yetu sote [emoji110]
 
Kuna battle moja YouTube kuhusu hii artificial intelligence kati ya Elon musk na Jack maa aisee wale jamaa ni magenius sana japo Jack ma alipotezwa na Elon ila hii technology sio rafiki kwa binadamu.
 
Siyo rafiki kwa nini?
Mbona inarahisisha sana matumizi ya mitandao
Kuna battle moja YouTube kuhusu hii artificial intelligence kati ya Elon musk na Jack maa aisee wale jamaa ni magenius sana japo Jack ma alipotezwa na Elon ila hii technology sio rafiki kwa binadamu.
 
Mimi nimetumia simple AI katika game langu la bao BaoTz ambalo linacheza mchezo wa asili wa bao vs binadamu. Shida ni kwamba hizi terms watu wanaziogopa na wanadhani lazima kiwe kitu kikuubwa nawewe ukijaribu wanaona kama haiwezekani na wanakudharau. Hii JF yenyewe ina AI. AI ni logics tu ambazo zinaweza kuwa advanced kwa kutumia machine learning, evaluation function nk.
 
FAHAMU KUHUSU ARTIFICIAL INTELLIGENCE ?

Neno artificial intelligence tunaweza sema ni "Akili bandia" ule uwezo wa teknolojia kufanya mambo mbalimbali ambayo kwa kawaida uhitaji kutumia uwezo wa akili kama wa binadamu kuweza kutambua vitu, watu, lugha , sauti , kufanya maamuzi, kujifunza, kutabiri, kutafsiri na nk.

Watu wengi wakisikia Artificial intelligence huwa wanafikiri inahusisha labda maroboti na teknolojia zenye nguvu zaidi kupindukia Ambazo mtu anafikiri kuwa hajawahi kutumia Kwenye Maisha yake.

AI Hipo Kwenye teknolojia kubwa pia ziko Kwenye teknolojia za kawaida kila siku Kwenye Maisha yetu.

Watu wengi duniani tunatumia mifumo hii ya artificial intelligence Kwenye Maisha yetu kila siku nazani [emoji3]umeshtuka kidogo sio relax , najua unatumia google , Instagram , Twitter , facebooks , bolt , kamera za simu , online payment, YouTube, Gmail nk

Mifano [emoji116][emoji880]

• 𝗬𝗼𝘂𝗧𝘂𝗯𝗲[emoji271]
Unapotizama au unapotafuta kitu huwa YouTube wanapendekeza kuangalia video nyingine zinatokea hivyo utaona wanakuletea video inayoendana na kitu ulichokitafuta apa AI inafanya kazi ya kukusaidia kutambua na kukusogezea video zinahusiana na unachokitafuta.

• 𝗸𝗮𝗺𝗲𝗿𝗮 𝘇𝗲𝘁𝘂 𝘇𝗮 𝘀𝗶𝗺𝘂 [emoji991]
Ukifungua kamera Kwenye simu Yako ukitaka kujipiga picha utaona kuna wakati Kuna msaada unakuja wa kuchagua effect ambayo inaenda na mazingira unayotaka kupiga picha au unapotaka kujipiga selfie utaona kitu kinatokea kuzunguka USO wako apa AI inatambua uwepo wa USO wako Kwenye kamera.

•𝗚𝗼𝗼𝗴𝗹𝗲 𝘀𝗲𝗮𝗿𝗰𝗵 [emoji361]
Unapotafuta kitu Kwenye Google mifumo ya Artificial Intelligence inakusaidia kuweza kukuletea majibu ya kile unachokitafuta ivyo google Utumia teknolojia ya Artificial Intelligence.

AI inatumika pia Kwenye masuala ya mawasiliano ,viwandani , Huduma za afya ,usalama , biashara , kilimo na nk.

Ebu tuachie maoni Yako ukisikia Artificial Intelligence ulikua unawaza kitu gani [emoji3] tuambie tujue ?

Teknolojia ni yetu sote [emoji110]
Kila kitu kina faida na madhara, it it/they fall in to the wrong hands. Mfano tech ya AI inaweza tumika kwenye drones za kivita(military Drones) deadly kama MQ9 reapers, predators etc. How? Wanaweza fix facial recognition softwares ili iuwe certain people tu itakayo wa recognize. So imagine that handful of software/tech or hardware falling to the wrong hands. Bora ztumike na intelligence agencies tu kwenye tracking nakdhalika.
 
Back
Top Bottom