Fahamu historia ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ndogo ya Bunge, William Ngeleja

Ajol

Senior Member
Dec 22, 2015
140
75
HISTORIA YAKE:

William Mganga Ngeleja alizaliwa Oktoba 5, 1967 mkoa Mwanza kwa sasa ana umri wa miaka 48.

Mh. William Ngeleja alisoma katika Shule ya Msingi Bitoto mwaka 1976 – 1982 kabla ya kuelekea mkoani Dodoma kwa masomo ya kidato cha kwanza mpaka cha nne katika Shule ya Sekondari Mpwapwa kati ya mwaka 1983 –1986.

Baada ya kufaulu vizuri aliendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Ihungo mkoani Kagera kati ya mwaka 1987 – 1989. alifaulu vizuri masomo yake na akajiunga moja kwa moja Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) sehemu ya Mlimani akichukua kozi ya sheria mwaka 1991.

Alihitimu na kutunukiwa shahada ya kwanza ya sheria (LLB) mwaka 1994 na kuajiriwa serikalini kama Mwanasheria wa Serikali mwaka 1994–1996. Ngeleja aliamua kujiendeleza zaidi, akarejea UDSM mwaka 1996 kusomea shahada ya uzamili ya sheria (LLM) na kuhitimu mwaka 1999.

Kati ya mwaka 1995 hadi 2000 Mh. William Ngeleja pia alifanya kazi na kampuni maarufu ya uwakili duniani ya Price WaterHouse Coopers, ambayo ina matawi mengi ulimwenguni ikiwamo Tanzania.

Mwaka 2000 aliacha kazi Price WaterHouse Coopers na kujiunga na kampuni ya Vodacom Tanzania ambako alifanya kazi kama mwanasheria wa kampuni, kwa miaka mitano, hadi 2005. Katika kipindi chote hiki Ngeleja aliendelea na kazi huku akikisaidia chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika masuala mbalimbali na wakati huohuo akifikiria kuingia katika siasa kwa kuwa alikuwa anaguswa na changamoto zinazo wakabili watanzania wa halo ya chini.

Toka 2005 hadi sasa ni Mbunge wa jimbo la Sengerema iliyopo mkoa wa Mwanza, Mwenyekiti wa Kamati hii ya Sheria ndogo za Bunge ni Mh. Andrew Chenge. Watanzania tuwe na imani na kamati hii kwani ina wanasheria Makini sana akiwemo Mh. Tundu Lissu, Mh. Halima Mdee nk.

Kamati hii INA jumla ya wajumbe 23, 17 kutoka Chama Cha Mapinduzi(CCM), na 6 kutoka Ukawa( 2 Civic United Front (CUF) na 4 kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Naomba kuwasilisha.......
 
Kwenye sheria hakuna ujanja ujanja its all about fact so wajumbe wakamati hii wote ni wataalam wa sheria.
 
Back
Top Bottom