Fahamu haya kuhusu bodaboda

Fahamu haya kuhusu bodaboda

King _Of_Everything

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
704
Reaction score
1,394
UTANGULIZI.
Ni matumaini yangu wazima nyote. Baada ya Maisha kunichapa mwaka 2016 nikajikuta nimeingia katika kazi ya bodaboda. Kazi ambayo nimedumu nayo mpaka sasa, Licha ya kuwa nimepata kazi ya ofisi inayoniingizia kipato kidogo sijawaza kabisa kuiacha. Pamoja na mafanikio niliyoyapata pia nimepitia changamoto kama vile kukoswa na Ajali mara kadhaa, kuibiwa, kulala Polisi, kusingizia kesi za wizi na hata shutuma za kuchukua mke wa mtu. Pamoja na changamoto zote hizo nilijitahidi kukomaa na katu sikuruhusu changamoto zinizuie kukamilisha malengo yangu.

KUHUSU BODABODA.
Ni kweli Bodaboda walio wengi (japo si wote) wametokea katika kazi za kihuni.(Wizi, ukabaji, Nk) Wengi wanakili kabisa tangu waingie katika kazi hii wameachana kabisa na Maisha yao ya awali kutokana na kukidhi mahitaji yao kwa kazi hii. Kwa sababu Serikali haijatangaza Ajira kwa miaka ya hivi karibuni kundi kubwa la vijana wasomi wameingia katika kazi ya Bodaboda hali inayoleta Heshima, Nidhamu na kuaminika tofauti na ilivyokua miaka ya nyuma. Wengi tunaipenda kazi yetu na tunaitii sheria bila shuruti, japo kuna wenzetu wengi bado hawana ufahamu wa kutosha katika kutumia alama za barabarani na baadhi yao wanaendesha kwa mazoea na ubishi tu.

CHANGAMOTO.
Bodaboda ni miongoni mwa kundi linaloathiriwa na wizi kwa kiwango kikubwa sana. Wengi tunaibiwa pikipiki na pengine hata kupoteza Maisha au kuachwa na ulemavu wa kudumu. Kuna sababu nyingi zinazopelekea kuibiwa, Uzembe (kwenda maeneo hatari na usiyoyajua hasa nyakati za usiku au kukubali kula kitu unachopewa na abiria usiyemjua).

Kukosa ufahamu (Baadhi hatuvijui vitambulisho vya polisi, wengi wanaibiwa na watu wanaojitambulisha kama maofisa wa Polisi tena wanakuonesha na ID kwa kuwa hatuvifahamu unakubali unashuka na Helmet yako jamaa wanachukua chuma kiulaini, hii ilitokea mataa ya Uhasibu mchana kweupee na Askari wapo pale pembeni kwenye banda lao).

Ukabaji hapa huwa unatumika ubavu unapigwa kabali hadi unahisi unachungulia kuzimu mwishowe unaachwa ukiwa hoi kama wakiona inafaa na ikibidi wanakumaliza kabisa kisha kutokomea na Boda (Hapa mara nyingi wanatumika wadada kama chambo, huwa wanajifanya kudondosha simu au kiatu akifika eneo husika na ukisimama tu wazee wa kazi wanaingia kazini).

NIDHAMU.
Kazi ya Bodaboda ni kazi kam ilivyo kazi nyingine, wapo wazee na vijana ambao kwa pamoja tunashirikiana ili kuweza kumudu kuendesha familia zetu. Si sawa kutuchukulia kama Wahuni, Wezi, au watu tusioenda shule, wengi tunajiheshimu na wengine tuna Elimu zetu kukuzidi hata wewe unayeleta dharau wakati kula kwa Mama, tunapitia tu kama sehemu ya Maisha kupunguza jam kwa wazee.

HITIMISHO.
Mwisho natoa wito kwa madereva wa magari aina zote, Barabara ni ya kwetu sote (Kodi tunalipa wote) Acheni dharau muwapo Barabarani. Polisi tunawaomba watoe ushirikiano mzuri kwetu, Kuna makosa mengine ya kumwelesha tu dereva hasa yale ya alama za usalama, wakati mwingine wanatumia ubabe kupitiliza hali inayopelekea kujengeka kwa chuki kati yetu na Polisi
NB: Ni uchambuzi unaotokana na uzoefu Binafsi, unaweza kuongeza unayoyafahamu. Karibuni kwa michango. Asante.
 
Muda mwingine bodaboda wanakuwa na haraka ya wapi sijui mpaka wanaweka lehani uhai wao.Jirekebisheni katika hili hasa kwenye mataa.
Punguzeni machejo na mwendo kasi mkiwa barabarani.
Ni sawa ila kutokana na watu huchukua boda kwa lengo la kuwahi, inapotokea Boda unazingatia sana taratibu za usalama unaonekana mzembe, wakati mwingine abiria hushuka na kuita Boda nyingine ndipo pale inabidi ujiongeze mkuu, hili nalo tatizo abiria huwa chanzo cha Ajali nyingi.
 
Siri
Boda boda hutunza siri za wateje wao, sekta ya bodaboda inahusika sana kufanikisha michepuko ya wanandoa kwa hiyo inabidi kuwa wasiri sana pale wanapowafikisha wateja wao kwenye nyumba za wageni kwa shughuri hizo.
 
Ni kweli na wengine wanakutongoza wenyewe.
 
Hivi mtu ukishakalia kiti cha bodaboda tu akili inaruka? Maanake haiwezekani kila bodaboda awe na akili mbovu!!!
 
HITIMISHO.
Mwisho natoa wito kwa madereva wa magari aina zote, Barabara ni ya kwetu sote (Kodi tunalipa wote) Acheni dharau muwapo Barabarani.
Ukijitoa ufahamu magari yanakupitia, kama huwezi kujali maisha yako hamna atakaeyajali.
 
Ukijitoa ufahamu magari yanakupitia, kama huwezi kujali maisha yako hamna atakaeyajali.
Hakuna Boda anayejitoa ufahamu isipokua watu wa magari wanadharau tu, upo upande wako jamaa anapiga horn kaliii ili umpishe na ukifika kwenye mataa ukasubiri kwenye foleni kama chombo chochote cha moto hapo kabisaa jamaa wa gari nyuma anakuona wa kuja, fujo nyingi Horn hiviiiii mradi tu ukae kando yeye apite.
 
Kama wewe sio bodaboda basi hutumii barabara za Dar. Kama ningeamua kugonga kila mwenye bodaboda anaekosea na kuingia anga zangu kwa siku ningegonga si chini wa watano.
 
Kama wewe sio bodaboda basi hutumii barabara za Dar. Kama ningeamua kugonga kila mwenye bodaboda anaekosea na kuingia anga zangu kwa siku ningegonga si chini wa watano.
Mjomba nipo hapa Town hizo mistake unazozizungumzia zipo sana (Wapo wasiozingatia) ila hata hayo niliyoyasema kuhusu ninyi watu wamagari yanafanyika na pengine ndio chanzo cha hili tatizo unalosema. Mnatupiga push sana Road naingia Boda Daily hapa ofisini haya nayaona.
 
Kama tabia ya bodaboda wangekuwa nayo madereva hata 30% tu barabara za mjini zingekuwa machinjioni.
 
Back
Top Bottom