Facts Kesi ya Yanga vs Morrison

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,277
9,912
YAMETIMIA

Kuna Jambo naliona, Ngao ya Jamii Yanga Kucheza na Azam FC

Pasipo Shaka Tanzania inaenda kuandika historia yake katika Mchezo wa Mpira wa Miguu, Ni jambo ambalo wengi hawakutarajia kama linaweza kutokea, Kuna asilimia 80% Sasa kwa Klabu ya Simba kwenda kushuka daraja.

Wengi tulijaribu kutumia Elimu na Maarifa ambayo Mungu ametujaaliwa kutoa ushauri wakisheria na ushauri wakihekima kuwaomba wenye mamlaka ya soka Nchini kulitafutia ufumbuzi wa Kihekima juu ya tatizo la Bernad Morrison na Klabu yake halali ya Yanga lakini Bahati mbaya sana tulibezwa na watu kuchukulia mambo kishabiki zaidi. Bahati Mbaya sana mambo yameharibika hayawezi kutengenezeka tena. Bernad Morrison na Klabu ya Simba sasa wapo mdomoni mwa chatu, Chatu ambaye anavuta pumzi kulipa tumbo lake nafasi kwa ajili yakukiweka tumboni kile kilichopo mbele yake.

Logic reasoning

Kesi ya Msingi ambayo Yanga waliipeleka CAS ground yake ilikuwa madai ya YANGA "KUWA NA MKATABA HALALI NA BERNAD MORRISON"

Madai ya Pili ya Yanga

Yalikuwa, Klabu ya Simba kumrubuni Bernad Morrison kwa kumuahidi kumpa Dola Elfu kumi ambapo walimtangulizia Dola Elfu Tano ili aweze kukubali kusajiliwa na Klabu ya Simba ili hali alikuwa na mkataba na Klabu ya Yanga

Lakini pia Shauri B lilikuwa, Klabu ya Simba kumsajili Bernard Morrison akiwa ndani ya Mkataba na Klabu ya Yanga tena Shauri lake likiwa bado lipo katika kamati ya Sheria ya TFF.

Open fact

Kitendo cha CAS , kutoa Taarifa kuwa hukumu itatolewa tarehe 24/8/2021, Tafasiri yake ni kwamba Bernad Morrison alikuwa na mkataba halali dhidi ya Klabu yake ya Yanga, Kama Shauri la kwanza la Yanga la madai kuwa Morrison ana mkataba halali na Yanga lisingekuwa na ukweli, Basi kesi ingeishia hapa hapa kwenye hiki kipengele, CAS wasingekuwa na sababu yeyote ya kwenda kusikiliza tena vipengele B na C . Ambavyo Klabu ya Yanga inailalamikia Klabu ya Simba kumrubuni na kumsajili Bernad Morrison ili hali ana Mkataba na Klabu ya Yanga

Bahati Mbaya sana Shauri hili wakati linajadiliwa kwenye kamati ya Sheria ya TFF , Chini ya Mwenyekiti Mwanjala walishindwa kujikita kwenye Determination of contract extension

Element kuu mbili za kisheria ambazo zimemuangusha Bernad Morrison katika Shauri hili ni

(a) Facts and (b) Defective on the case ground

Jkt Ruvu Kutoshuka Daraja

Kikanuni Klabu ikiwa imemchezesha mchezaji ambaye Ana mkataba na Klabu nyingine, Basi adhabu yake ni kunyang'anywa point katika mechi zote ambazo mchezaji husika ametumika kucheza.

Fact reference ya hukumu

Klabu ya AS VITA inayoshiriki ligi kuu ya Kongo, msimu huu imenyang'anywa Point na Ubingwa baada yakumchezesha Mchezaji anayeitwa Zao Matutala ambaye kipindi wanamtumia alikuwa na kesi CAS kama hivi ilivyo kwa Bernad Morrison, Bahati Mzuri AS VITA mchezaji huyu walimtumia kwenye Mechi Tatu tu za Ligi, Ambapo AS VITA walinyang'anywa point 9 baada ya Zao Matutala kushindwa kesi, Kutokana na AS VITA kunyang'anywa point 9 TP MAZEMBE wakajikuta wanakuwa Mabingwa wa Ligi kuu ya Kongo kwa msimu wa 2021/2022

Kwanini hukumu haijatolewa leo?

Kuna kitu kinaitwa Documents compile
Hii ni stage yapili kutoka mwishoni kabla yakutoa Taarifa ya hukumu
Kwasasa CAS wanacompile documents ili waweze kutoa hukumu

Katika tukio hili lakihistoria JKT RUVU yenye Point 29 itasalimika kushuka Daraja, na Klabu yetu ya Simba itaungana na Gwambina Fc yenye Point 35, Ihefu yenye Point 35 na Mwadui yenye Point 19

Rage naye kaamka usingzini, anasema kesi hii ngumu

Siku zote tunajifunza kutokana na makosa, Ingawa funzo hili ni chungu lakini naamini litakuwa funzo kwenye tasnia ya Mpira wa miguu Nchini

Mwikwabi James
Legendary
0766074160
 
Bongo linapokuja suala la weredi n hovyo Sana

Haojalishi Simba au yanga itakuwa mshindi ila bongo weredi n sifuri

SERIKALI..haturuhusu mikusanyiko

SERIKALI..Kesho tunapokea chanjo hvyo tunaomba tujumuike pamoja

SERIKALI..Rais Kesho atapokea ndege tunaomba tujumuike pamoja

SERIKALI..marufuku kongamano lolote nchi hii Kwan kuna korona

SERIKALI..Mechi ya Simba na yanga ruksa ila vaeni barakoa

Hii nchi n ngumu ngumu ngumu kwani kuna double standard nyingi sana

INABIDI TUTAWALIWE UPYA NA WAKOLONI TENA ULE UKOLONI MKONGWE NA SI MAMBOLEO

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Yaani Yanga pamoja na kucheza Kung fuh Bado hawakufua dafu sasa wamenogewa na mbeleko wanataka na kombe kabisa mezani! Hadi aibu.
Pambaneni uwanjani utopolo. Au mmeacha mpira mmeamua kuwa na law firms!
 
FIFA Transfer Matching System (TMS) Inafanya kazi mara moja tu kila muda wa usajili unapofunguliwa na kufungwa basi, hii ina maana kubwa sana katika kulinda usahihi kwa mchezaji toka sehemu moja kwenda nyingine.

Morrison Msimu wa 2019/2020 alisajiliwa na Yanga kwa Mkataba wa Miezi Sita na ndio uliowekwa kwenye TMS hapa ina maana System ilifungwa mpaka Dirisha kubwa la June 2020.

Mkataba wa Extension wa Morrison na Yanga ambao ndio unaleta ukakasi na kesi CAS haukuwepo kwenye system sababu ulifanyika system ilishafungwa, ulikuwa unasubiria mpaka system iwe wazi tena.

Baada ya Hukumu ya Kamati na Mwezi wa June Morrison aliweza kuwa huru na kusajiliwa na Simba kwa sababu System ilionyesha yupo hivyo kutokana na mkataba uliyokuwepo ni ule wa miezi 6 sio huyo mpya.

Simba waliweza msajili Morrison akiwa huru na TMS ilikubali ombi la Simba kuweka data kutokana na ukweli huo, kama ingekuwa ule mkataba wa Extension upo kwenye TMS basi Simba walipaswa kuomba kwa Yanga Release ya mchezaji ambalo ingekuwa suala gumu sana kukubaliwa na Yanga.

Kwa Mantiki hiyo Suala la Case iliyopo sasa CAS haiwezi kuadhiri Chochote katika msimu huu 2020/2021 katika mkataba wa Morrison na Simba kwa Maana Pana sana tena hata Yanga hawajawahi kuweka Pingamizi kuhusu usajili huo popote pale pindi tu alipotangazwa na Bodi/TFF/TPLB kuwa ni mchezaji wa Simba msimu huu.

Tuendelee kuvuta subra mpaka 14 August tuone nani zitamtoa Fedha za fidia.
 
pole sana kwa kukariri sheria! case ya Morrison na Yanga inamshushaje daraja simba wakati wasimamizi wa mpira tff walisema Morrison alikuwa huru kucheza timu aitakayo! naudia pole sana??!!!!!!
CA's iko juu tff chombo kikubwa ni FIFA ambao Ndiooo wenye kitengo cha CA's
 
pole sana kwa kukariri sheria! case ya Morrison na Yanga inamshushaje daraja simba wakati wasimamizi wa mpira tff walisema Morrison alikuwa huru kucheza timu aitakayo! naudia pole sana??!!!!!!
Kwani huyo Mchezaji wa AS Vita alithibitishwa na nani?
 
Waulize as vita imekuwaje?
Sio kila hukumu ya CAS, ni lazima iwe kama alivyoelezea mtoa mada, kuna kesi nyingi toka huko, timu zilifungiwa kusajiri kwa kipindi fulani, walipigwa faini!!mambo yakaisha., naamini hata hili endapo yanga wakishinda , simba hawezi kupokonywa points, na kushushwa daraja, muda utaongea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom