Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,103
- 128,718
Wanabodi
Utangulizi
Kuna kitu kinaitwa facts na kuna fallacies. Kuna msemo wa kizungu usemao, "facts are stubborn things", yaani fact ni kitu ambacho kipo, kina exist in reality, you can't deny facts. huwezi kusema hukitambui, unaweza usikikubali lakini kipo, unaweza usikipende lakini kipo, unaweza kusema hukitambui, kutokukitambua huko, hakubadilishi kitu, kwasababu kipo!.
Baada ya kuapishwa rasmi, sasa it's a fact: Rais Samia ndiye rais wa JMT!, uwe ulimchagua, hukumchagua, uwe ulipiga kura, hukupiga kura, uwe uko Tanzania au uko ughaibuni, uwe unayatambua matokeo ya uchaguzi mkuu au hauyatambui, uwe unamtambua kama rais wa JMT au humtambui, Rais Samia Suluhu Hassan ndie Rais wa JMT, ndie Rais wa nchi, ndie wa Watanzania wote popote walipo duniani, umtambue usimtambue, umpende usimpende, umkubali usimkubali, it's not gonna change anything!, kwasababu Samia kuwa Rais, its a fact, na facts are very stubborn things, facts lazima uikubali, kinyume cha hapo ni fallacies!.
Declaration of Interest
Mimi Pascal Mayalla, pia nimeguswa sana na kuumizwa na picha za miili ya Watanzania wenzetu zinazopostiwa mitandaoni, mimi nimeumia zaidi kwasababu nina mabandiko zaidi ya 100 humu nikishinikiza we do the right thing, tuache kumanya maigizo ya uchaguzi, tufanye chaguzi huru na za Kweli, hivyo kilichotokea kwenye uchaguzi mkuu huu ni matokeo tuu na sio chanzo, chanzo sote tunakijua na kinafahamika, ni mapuuza ya not doing the right thing, hata kama chanzo chenyewe ni mtu, kisha ukafanyika uchaguzi mkuu wa a mere sham, akatangazwa kushinda kwa asilimia 98%, baada ya kuapishwa, ndiye rais wa JMT, this is a fact, hivyo sasa ni lazima aheshimiwe!.
Leo Jumatatu, Rais Samia Suluhu Hassan, ameapishwa kuwa Rais wa JMT kwa kipindi cha pili cha miaka mitano baada ya ushindi wa kishindo cha asilimia 98% katika uchaguzi ambao ulikumbwa na vurugu za hapa na pale zilizosababisha na maandamano yaliyopelekea umwagaji wa machozi, jasho na damu za Watanzania.
Rais akiisha apishwa sasa ni Rais wa JMT, uwe ulimchagua, hukumchagua, uwe unampenda au humpendi, uwe ulipiga kura au hukupiga kura, uwe upo nchini Tanzania au upo nje ya Tanzania, as long as wewe ni Mtanzania, Rais Samia ndie Rais wako, ndie Rais wetu, ndie Rais wa Tanzania, ni Rais wa wote, this is a fact.
Watanzania pekee wenye locus stand ya kutomtambua Rais Samia kama rais wao, ni Watanzania wa diaspora ambao waliisha ukana uraia wao wa Tanzania na kuchukua uraia wa nchi nyingine, hivyo kupoteza uraia wao wa Tanzania, hawa wakisema hawamtambui na Rais Samia sio rais wao, hawa they are right, lakini kwa raia wa Tanzania, popote pale walipo, rais Samia ndie Rais wao.
Hivyo anapaswa kuheshimiwa ile heshima ya wajibu wa kuheshimu mamlaka.
Kufuatia kilichotokea kwenye uchaguzi mkuu huu, kuna watu hawakubaliani na matokeo haya, na kujiapiza kuwa hawamtambui, Rais akiisha apishwa ni rais wa JMT, umtambue, usimtambue, hakubadili kitu chochote, rais Samia ndie Rais wa JMT.
Makala hii ni kuwaelimisha Watanzania haswa vijana na wale wa mitandao ya kijamii, kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote, kufuatia kilichotokea kwenye uchaguzi huu, lakini ni lazima aheshimiwe na wote kwasababu mtu akiishakuwa rais wa nchi, hapo hapo ana assume status ya dual personality, yaani japo ni mtu mmoja, lakini anakuwa na wajihi mbili, hivyo ni watu wawili ndani ya mmoja, two in one!.
Kwa upande mmoja rais ni binadamu wa kawaida, na wakati huo huo rais ni taasisi ya urais, hivyo rais wa nchi ni lazima aheshimiwe kwa heshima ya lazima ya kimamlaka, akosolewe kwa lugha ya staha, asitukanwe wala asitusiwe!.
Hoja hii ni kufuatia mjadala mingi kwenye mitandao ya kijamii kufuatia yaliyojitokeza kwenye uchaguzi huu. kuna watu wamevuka mipaka na kumkosea heshima Rais Samia kwa kumkosoa kwa lugha kali, kumtweza, kumkashifu na wengine kuvuka mipaka hadi kumtukana matusi ya nguoni!, kitu ambacho sio sawa.
Hii ya rais kuwa japo ni mtu mmoja lakini ana wajihi mbili, inaitwa duality.
Persnality ya kwanza ya Rais wa nchi ni human personality, yaani rais ni binadamu, a human being kama binadamu mwingine yoyote wa kawaida anayestahili mahitaji yote ya kibinadamu, hivyo rais wetu Samia ni mtu anayeitwa Samia Suluhu Hassan, huyu ni binadamu.
Soma Pia: INEC yamtangaza Samia Suluhu Hassan kuwa Mshindi wa Urais kwa 98%
Hivyo huyu Samia ambaye ni binadamu, unaweza kumpenda au usimpende, unaweza kumkubali au usimkubali, unaweza kumchukia, kumbeza, unaweza kumtukana na kumdhalilisha au kusema chochote kumhusu mtu anayeitwa Samia Suluhu Hassan na hakuna tatizo!.
Kumpenda mtu yoyote ni utashi binafsi wa mtu, anaweza kumpenda mtu mwingine yeyote, kwa sababu zozote au bila sababu, au unaweza usimpende mtu kwa sababu zozote, au bila sababu, na hakuna kosa lolote kutompenda yeyote lakini hata ikitokea mtu fulani humpendi, bado una wajibu wa kumheshimu na kuulinda utu wake.
Personality ya pili ya Rais Samia, ni rais wa nchi, hivyo huyu binadamu anaitwa Samia Suluhu Hassan, baada ya kuapishwa na kuwa ni rais wa nchi sasa ana, assume kitu kinachoitwa presidential personality, huyu sasa sio mtu binadamu, ni mtu taasisi yenye mamlaka ya juu kabisa ndani ya JMT, hivyo rais wa nchi kwa personality yake ya urais, ni lazima aheshimiwe, utii kwa mamlaka, utake usitake, huwezi kumtukana, huwezi kumdhalilisha, itakuwa ni kuitukana taasisi ya urais. Dini zote zinafundisha utii kwa mamlaka, iwe ni mamlaka halali au haramu, una wajibu wa kutii mamlaka.
Hakuna binadamu anayeunga mkono yatokanayo na maandamano ya kupinga uchaguzi, vifo, fujo, uharibifu wa mali, lakini maadam ametangazwa kushinda na ameapishwa sasa Rais Samia ndie Rais wa JMT, tunaweza tusimpende wote, na tusimkubali kufuatia kilichotokea, lakini ni lazima tumuheshimu kama binadamu, kila binadamu anastahili heshima na kwa vile ni rais lazima aheshimiwe heshima ya lazima ya wajibu wa kuheshimu mamlaka halali, na ukitokea ukosoaji, tumkosoe kwa lugha ya staha na sio kumtukana na kumdhalilisha.
Hitimisho
Nijiunge na Watanzania wote kutoa pole kwa hotte yaliyotokea na wahanga wa kilichotokea, lakini kila mtu anajua kula Rais Samia hakushika bunduki yoyote kufanya chochote, yeye ni rais wetu aliyetangazwa kushinda uchaguzi, baada ya kuapishwa, tumpende, tumheshimu, tumsuport, na hata ikitokea, kuna sehemu anakosea tumkosoe kwa heshima na staha.
Nitoe pongezi zangu kwa rais Samia kwa ushindi wa kishindo, ila kwa vile ushindi huu, umeandamana na umwagaji damu, namuomba Rais Samia na serikali yake, kwanza wasijitape sana kwa us hindi sente mazongezonge, pili wakubali kuwajibika kwa kilichotokea, kwa kuwapa pole Watanzania, kuonyesçha kujutia kilichotokea ukiwemo umwagaji wa damu, na kutubu kwa kuomba radio, kuomba msamaha na kukubali kuwajibika.
Serikali mkubali kulipa fidia uharibifu wowote wa mali uliotokana na vurugu zilizosababishwa na maandamano hayo, na kutoa kifuta machozi kwa wafiwa, na pole kwa majeruhi kwasababu maandamano hayo sio chanzo, ni matokeo, chanzo kinafahamika, kwa vile serikali yetu ilishindwa kutibu chanzo, inabidi kukubali kubeba mzigo wa kulipa fidia.
Namuomba Rais Samia, kazi yake ya kwanza iwe ni kuliponya taifa, kidonda hiki bado ni kibichi kabisa, Rais bombe msamaha wa jumla kwa kote, watangaze idadi ya tifo na majeruhi, watu waruhusiwe kuwazika wapendwa wao, Rais Samia atangaze msamaha wa jumla kwa wote na kwa yote yaliyotokea wakati wa uchaguzi, ila fujo na vurugu zitakazoendelea baada ya kuapishwa, hizi sasa ndizo zishughuliwe bila nywinywi wala nywinywini!
Mungu Ibariki Tanzania .
Paskali