FB imeleta maumivu mengi kwa baadhi ya watu.
Ushauri wa bure, kwa wale ambao wana wenza wasiokuwa na uelewa na haya mambo ya mitandao ya kijamii, Usimweke mkeo/mumeo/mchumba kwenye FB maana inaweza kuwa mwanzo wa migogoro.Tandaa na marafiki wa kawaida na ndugu zako kama baba, mama, kaka, dada, watoto, shangazi, wajomba. Pia tandaa na marafiki zako wa kikazi, kibiashara nk.Epuka kukubali kuingiza watu usiowajua wawe kwenye list YA MARAFIKI Zako.Tumia nyenzo za usalama wako kama vile kuzuia watu usiowafahamu ku access your pictures na taarifa zako muhimu kwenye FB.Ukitaka usalama zaidi tumia jina tofauti ambalo watu wanalifahamu au kulizoea maana ni rahisi watu ku search jina lako na kukupata.