Facebook yatoa sera mpya ya kuchagua mtu wa kushughulikia akaunti baada ya kufa

Dark Angel

JF-Expert Member
Sep 12, 2013
212
220
Je unajua kipi kinafanyika kwa akaunti ya Facebook ya mtu aliyefariki?

Hiyo ndio mada yetu ya wiki hii katika kipindi cha Sema Uvume. Facebook imetangaza sera mpya inayokuruhusu kuchagua mtu atakayeishughulikia akaunti yako baada ya kufariki.

Awali kulikuwa na njia mbili tu, zilizokuwa zikitumika. Baada ya kifo chako kuripotiwa Facebook, akaunti yako inaweza kufutwa kabisa, ama inaweza kufungwa na kubaki kama ukubusho ila hamna mtu anayeweza kuingia na kubadilisha chochote ulichokituma ukiwa hai.

Je, kama mtumiaji wa mtandao wa Facebook ungependelea njia gani?
 
Nilikuwa sijui kama mtu akifa wanafuta akaunti yake, nilikuja gundua mara baada ya mtangazaji wa bbc focus on Africa Komlar Dumor kufariki.
 
what if dunia nzima tumekufa kwa pamoja paaaa we are dead.. nani atakuwa mrithi wetu kwenye facebook?!! mh natumia nguvu sana kujiuliza!!?
 
Back
Top Bottom