Facebook yarejesha picha ya 'msichana wa Napalm'

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,092
Facebook imebatilisha uamuzi wake wa awali wa kufuta moja ya picha mashuhuri ya wakati wa vita vya Vietnam.

Picha hiyo inamuonyesha mtoto msichana aliyekuwa bila nguo akikimbia moto katika kijiji kimoja, katika shambulizi lililotekelezwa kwa kutumia kemikali ya napalm.

Facebook ilifuta picha hiyo kwa misingi kwamba ilikuwa ya uchi.

Facebook inasema imerejesha picha hiyo kutokana na umuhimu wake wa kihistoria.

Gazeti moja nchini Norway, Aftenposten, liliongoza shutuma dhidi ya Facebook, baada ya kampuni hiyo kufunga akaunti ya mmoja wa wanahabari wake, aliyetumia picha hiyo.

Mhariri wa gazeti la Afte-posten la Norway, amesema uamuzi wa Facebook kufuta picha hiyo inaonyesha wazi haiwezi kutofautisha kati ya picha za ponografia na zile zinazohusiana na historia ya matukio muhumu duniani.

Waziri mkuu wa Norway ambaye awali alichapisha picha hiyo kwenye akaunti yake kama ishara ya maandamano, amekaribisha uamuzi wa Facebook wa kurejesha picha hiyo.

_91100923_d95ca202-fe9f-4ef6-bd54-59892c21636d.jpg

Waziri mkuu wa Norway anasema uamuzi wa Facebook ulionyesha ushawishi mkubwa wa mitandao ya kijamii.

"Wamefanya vizuri sana, mimi ni waziri mkuu aliye na furaha, inaonyesha kwamba matumizi ya mitandao ya kijamii yanaweza kuleta mabadiliko ya kisiasa, hata kwa mitandao ya kijamii yenyewe" Waziri mkuu Erna Solberg ameiambia BBC.

Msichana huyo ni nani?

Kim Phuc, alikuwa mwenye umri wa miaka 9 wakati picha hiyo ilipochukuliwa, akikimbia kuokoa maisha yake, baada ya shambulizi la Napalm, kaskazini mwa Saigon mwezi Juni 1972.

Alikumbwa na majeraha mabaya ya moto.

Mpiga picha Nick Ut na mwanahabari wa ITN Christopher Wain walimpeleka hospitalini.

Waliambiwa kwamba hakukuwa na matumaini kwamba msichana huyo angeendelea kuishi.

_91100922__91083634_mediaitem91079975.jpg

Facebook inasema imerejesha picha hii kutokana na umuhimu wake wa kihistoria.

Baada ya kulazwa hospitalini kwa kipindi cha miezi 14, na kufanyiwa upasuaji mara 17 , aliruhusiwa kuenda nyumbani.

Chanzo: BBC Swahili
 
Attachments

  • e8a8e1aaee6e46ecb5ee4dc0c55dafe0_18.jpg
    e8a8e1aaee6e46ecb5ee4dc0c55dafe0_18.jpg
    28 KB · Views: 123

  • kimphuc-nickut-duyanh-9.jpg
    kimphuc-nickut-duyanh-9.jpg
    35.4 KB · Views: 108
  • kim-phuc.jpg
    kim-phuc.jpg
    15.6 KB · Views: 40
Back
Top Bottom