FACEBOOK, KATI YA MAREKANI NA BONGO

FACEBOOK, KATI YA MAREKANI NA BONGO

Icon Special

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2019
Posts
257
Reaction score
230
Hello, Naitwa Sandra, Nipo New York, nampenda mume wangu Sana, naweza kufanya chochote ili nimridhishe na kumfurahisha.. Lakini hivi karibuni, nimetokea kumpenda binamu wa mume wangu.. Tena mapenzi mazito.. Naombeni ushauri nifanyeje?

WACHANGIAJI WA KIMAREKANI:

JAMES SILVER: Nadhani unapaswa kuongea na mumeo, kwa sababu ndoa ni kushea kila jambo.

SARAH WATER: OH my dear, sorry.. Imewahi kunitokea hiyo hali na mie. Ilinilazimu nijifunge kibwebwe kuiepuka ili kulinda ndoa.

MICHAEL MOORE: Ondosha fikra zako kwa huyo binamu wa mumeo.. Mfanye mumeo yale unayoyaona kwa huyo binamu yake..

MADA HIYO HIYO KWENYE JAMII FORUM, BONGO INAKUWA HIVI:
Hello, ( Jina siri yangu), Naishi Unga Limited, Arusha. Nimeolewa na Nina mtoto mmoja. Nimetokea kumpenda binamu wa mume wangu.. Nifanyeje, naombeni ushauri..

WACHANGIAJI WA KIBONGO, MAJIBU YAO:

EVARIST MASSAWE: Huna akili mpumbavu wee. Tumbili mkubwa, nyau wa kike.. YAANI unataka uanze balaa kwa binamu wa mumeo?

JOYCE MPIGAUZI: Unatutia aibu na kutudhalilisha wanawake wenzako loooh
Na vile Unga Limited ilivyo ndogo, tutakujua tu.

SELE MPEMBA:
Hivi Simba wanakipiga lini na TP Mazembe?

ANDENDEKISYE MWAKIFUGE: Kama ukiona binamu wa mumeo anazingua, mie nipo available 0710808312. Nipo Mwanjelwa.

JONES RUTTA:
Sio kosa lako. Ni kosa la wazazi wako.. Hawakutumia akili wakati wa kukuzaa.

TZ SWAG:
Wazee Nani Ana chaja ya smartphone? Simu yangu imeisha chaji.

RAMESH MATUKUTUKU: Je, una tatizo la kuwahi kileleni, upungufu wa nguvu za kiume? Inbox me na tatzo lako litaisha ndani ya wiki moja ujenge heshima

ANDREW THE DON:
Wow.. Mtoto uko Bomba.. Ni add please..

MTUMISHI: Wewe ni kahaba uliyeshindikana, unatakiwa Uokoke.. Njoo ufanyiwe maombi.

MAC MUGA: Tengeneza mpaka milioni mbili ndani ya wiki moja tu bila kuathiri kazi zako. Kwa maelezo zaidi nitafute 07356

MWAJEY MIKIDADI: Pumbaaaaaf.

DEVOTA JILANGILA:
Napita tuuu.

DULLA BOY:
Mie huwa sichangiaji post za kijinga kama hii...

wabongo bana [emoji38][emoji38]
 
Kwani ulifikiri ule utafiti wa wananchi wa Tanzania kuwa kwenye list ya mwisho ya wenye furaha ilikuwa ni uongo?

Hizo ndio dalili za msongo wa mawazo sasa
Exactly bro, coz unakuta mtu yupo serious na jambo lake anataka ushaur wenye maana,
Kituko sasa watu wanamwandikia madudu, cjui makorokocho gani
Mtu utaacha kukosa stress!!? Wabongo sie n Shida Sana
 
Hello, Naitwa Sandra, Nipo New York, nampenda mume wangu Sana, naweza kufanya chochote ili nimridhishe na kumfurahisha.. Lakini hivi karibuni, nimetokea kumpenda binamu wa mume wangu.. Tena mapenzi mazito.. Naombeni ushauri nifanyeje?

WACHANGIAJI WA KIMAREKANI:

JAMES SILVER: Nadhani unapaswa kuongea na mumeo, kwa sababu ndoa ni kushea kila jambo.

SARAH WATER: OH my dear, sorry.. Imewahi kunitokea hiyo hali na mie. Ilinilazimu nijifunge kibwebwe kuiepuka ili kulinda ndoa.

MICHAEL MOORE: Ondosha fikra zako kwa huyo binamu wa mumeo.. Mfanye mumeo yale unayoyaona kwa huyo binamu yake..

MADA HIYO HIYO KWENYE JAMII FORUM, BONGO INAKUWA HIVI:
Hello, ( Jina siri yangu), Naishi Unga Limited, Arusha. Nimeolewa na Nina mtoto mmoja. Nimetokea kumpenda binamu wa mume wangu.. Nifanyeje, naombeni ushauri..

WACHANGIAJI WA KIBONGO, MAJIBU YAO:

EVARIST MASSAWE: Huna akili mpumbavu wee. Tumbili mkubwa, nyau wa kike.. YAANI unataka uanze balaa kwa binamu wa mumeo?

JOYCE MPIGAUZI: Unatutia aibu na kutudhalilisha wanawake wenzako loooh
Na vile Unga Limited ilivyo ndogo, tutakujua tu.

SELE MPEMBA:
Hivi Simba wanakipiga lini na TP Mazembe?

ANDENDEKISYE MWAKIFUGE: Kama ukiona binamu wa mumeo anazingua, mie nipo available 0710808312. Nipo Mwanjelwa.

JONES RUTTA:
Sio kosa lako. Ni kosa la wazazi wako.. Hawakutumia akili wakati wa kukuzaa.

TZ SWAG:
Wazee Nani Ana chaja ya smartphone? Simu yangu imeisha chaji.

RAMESH MATUKUTUKU: Je, una tatizo la kuwahi kileleni, upungufu wa nguvu za kiume? Inbox me na tatzo lako litaisha ndani ya wiki moja ujenge heshima

ANDREW THE DON:
Wow.. Mtoto uko Bomba.. Ni add please..

MTUMISHI: Wewe ni kahaba uliyeshindikana, unatakiwa Uokoke.. Njoo ufanyiwe maombi.

MAC MUGA: Tengeneza mpaka milioni mbili ndani ya wiki moja tu bila kuathiri kazi zako. Kwa maelezo zaidi nitafute 07356

MWAJEY MIKIDADI: Pumbaaaaaf.

DEVOTA JILANGILA:
Napita tuuu.

DULLA BOY:
Mie huwa sichangiaji post za kijinga kama hii...

wabongo bana [emoji38][emoji38]
Hahahahahah. Hii ni kweli kabisa
 
Ukiwa serious na mambo ya mitandaoni utaumwa kichwa tu wakati maisha yenyewe hayaeleweki huku uswahilini...
 
Ulimbukeni kwenye matumizi ya mtandao pia ni tatizo, watu ni ilimradi tu wame komenti.

NB: Kutoa ushauri sio ma ta ko kwamba kila mtu anayo, inahitaji skills pia sometime
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom