Facebook: Apps za WhatsApp na Instagram kufanyiwa mabadiliko ya majina

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
apps za whatsapp na instagram

Apps za WhatsApp na Instagram ambazo zinamilikiwa na kampuni ya Facebook, zipo njiani kufanyiwa mabadiliko ya majina.

Inasemekana uamuzi huu umelazimika kufanyika kutokana na mashambulizi/malalamiko ya makampuni mengine kuhusu ukiritimba (monopoly) wa Facebook.

apps za whatsapp na instagram na facebook

Apps hizi tatu zinaongeza kwa wingi wa watumiaji katika eneo la kuchati kwenye masoko yote ya apps: watumiaji wa Android na iOS

Makampuni shindani yameshalalamika kwa muda mrefu kwa taasisi za ushindani wakisema ni vigumu kwa mtumiaji kufahamu kama apps za WhatsApp na Instagram zinamilikiwa na Facebook, na kama watumiaji wakielewa hili linaweza kuwafanya wasikubali kutumia na kuipa data zao nyingi kampuni moja tuu – yaani Facebook.

Kutokana na hilo Facebook wamesema wapo njiani kuboresha majina ya apps hizo; mabadiliko hayo yanamaanisha app ya Instagram itafahamika kwa jina la Instagram from Facebook,- yaani Instagram kutoka kwa Facebook, na WhatsApp ikiwa ni WhatsApp from Facebook – yaani WhatsApp kutoka kwa Facebook.

Lengo kuu hapa ni kuweka wazi kwa watumiaji ya kwamba app wanayotaka kuipakua inatoka kwa kampuni ya Facebook.

Facebook wamesema ila bado ingawa majina hayo yataonekana sehemu zote, hii ikiwa ni pamoja na kwenye masoko ya apps, ila kwenye simu yako baada ya kuipakua majina haya mapya hayataonekana kwenye eneo la apps zilizo kwenye simu yako – bado apps zitaandikwa kwa jina fupi, yaani WhatsApp na Instagram. Hii ni kwa sababu majina mapya ni marefu sana. Majina mapya yatatumika sehemu zingine zote.

Pia uamuzi huu umekuja katika kipindi ambacho tayari Facebook wamesema wamewekeza katika utafiti wa kuunganisha apps hizi maarufu katika eneo la kuchati.Yaani mtumiaji wa Instagram aweze kumtumia ujumbe utakaokwenda WhatsApp, na mtu kupitia WhatsApp aweze kuchati na mtu anayetumia Messenger (Facebook). Muunganisho huu wa huduma ya kuchati upo katika matengenezo kwa sasa.
 
Asante kwa taarifa ssi tunangoja waje lkn wasije kutuharibia uhondo wetu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom