kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,685
Man U na Chelsea zimekutana mara 166 katika mashindano mbalimbali, ambapo Manchester United imeshinda mechi 72, Chelsea (45), na wametoka sare mechi 49.
Chelsea itamkosa kiungo wake Juan Mata katika mchezo wa leo wa Kombe la FA dhidi ya Manchester United kwa sababu anaumwa. Kocha wa wa Chelsea Rafael Benitez anahitaji wachezaji wake kutulia zaidi kwani wanatakiwa kucheza mechi mbili muhimu katika saa 48 baada ya kuchapwa mwishoni mwa wiki.
Wakati Mata akiwa benchi, beki Gary Cahill anatarajiwa kurejea leo akiwa amepona goti lake lililomkosesha mechi waliyofungwa 2-1 na Southampton siku ya Jumamosi.
Vinara wa Ligi Kuu, Manchester United watamkosa beki wake Rafael anayesumbuliwa na nyonga aliyoumia wakati wa mechi dhidi ya Sunderland mwishoni mwa wiki. Wakati beki Rio Ferdinand, mkongwe Ryan Giggs na mshambuliaji Wayne Rooney waliopumzishwa Jumamosi wanatarajiwa kushuka dimbani leo.
Manchester United mchezo wa kwanza walitangulia kushinda 2-0 kabla ya kulazimishwa sare 2-2 na Chelsea. Mechi ya leo mchana tutegemee kuwa kali zaidi ukilinganisha na iliyopita.