Ezekiel Wenje na Alphonce Mawazo kuwasha moto uzinduzi wa kampeni za udiwani Lwenzera-Geita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ezekiel Wenje na Alphonce Mawazo kuwasha moto uzinduzi wa kampeni za udiwani Lwenzera-Geita

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Idimulwa, Oct 4, 2012.

 1. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mbunge wa Nyamagana-MWANZA Ezekiel Wenje na aliyekuwa diwani wa kata ya Sombetini-ARUSHA kupitia CCM kabla ya kujiuzulu na kujiunga CHADEMA bwana Alphonce Mawazo,watazindua kampeni za CHADEMA kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa diwani katika kata ya Lwenzera iliyoko tarafa ya Bugando,wilayani Geita ndani ya mkoa mpya wa GEITA kesho kutwa tarehe 06/10/2012.

  Uchaguzi huo unafanyika kufuatia kifo cha diwani ANATORY MKUFU wa CCM.Katika uchaguzi huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kati ya vyama vya CCM na CHADEMA,CHADEMA itashirisha vikosi kutoka ndani ya mkoa wa Geita, Mwanza pamoja na Makao makuu katika kusaka ushindi.Makada na Madiwani wote wa mikoa ya Mwanza na Geita waliohama kutoka CCM na kujiunga CHADEMA watashiriki kikamilifu pamoja na timu yote iliyokiwezesha CHADEMA kuitetea kata ya KIRUMBA jijini MWANZA hapo 01,April 2012, licha ya upinzani mkali na mbinu chafu kutoka CCM,ikiwemo kuraruliwa kwa mapanga baadhi ya wafuasi na madiwani wa CHADEMA usiku wa kuamkia siku ya kupiga kura Kirumba.

  Matokeo ya chaguzi ndogo zinazotarajiwa kufanyika katika kata 29 nchini,mnamo tarehe 28-10-2012 yatatumika kama kipimo cha kuweza kufahamu kama harakati za kisiasa zinazoendelea kufanyika nchi nzima chini ya kauli mbiu 'Vuguvugu la Mabadiliko'(Movement For Change) zinafanikiwa au la.Na ili kuhakikisha kuwa kanda ya ziwa ukiwemo mkoa huu mpya wa GEITA, inaendelea kuwa ngome imara ya CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu 2015,viongozi wa Taifa CHADEMA akiwemo katibu mkuu Dr W.Slaa watashiriki pia katika kampeni za Lwenzera.

  Chama Cha Wananchi-CUF kinashiriki pia na tayari kimeshazindua kampeni zake juzi,CCM bado na haijajulikana bayana watazindua kampeni zao lini.

  Ni kiwaahidi kuwa taarifuni kila kitakachokuwa kinajiri juu ya uchaguzi huu, ni mimi IDIMULWA wa JF.
   
 2. N

  Nyota Njema Senior Member

  #2
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naam, Geita ni ngome nyingine ya CDM ambayo ujenzi wake sasa umefika kwenye paa! Ni matumaini yetu kuwa uchaguzi huu utaiandaa vema CHADEMA Geita katika mkakati wake wa kuzibeba halmashauri zote zitakazoundwa humo pamoja na majimbo yote ya Mkoa huu mpya wenye rasilimali nyingi yakiwemo madini ya dhahabu.

  Kila laheri CDM katika uchaguzi huu ambao uhakika wa kushinda ni mkubwa kutokana na harakati zilipo kwa sasa na uelewa walionao wananchi wa Geita wa sera na misingi ya ukombozi ya CHADEMA.
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Makamanda wetu wote chini ya M4C juhudi zenu kwa kila kitongoji katika kila kaya hivi sasa HADI RAHA!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Wakati mabeki wengi walioko ndani ya chama hicho na hata wale wengine wengi zaidi waliojificha ndani ya hivi vyama vya 'upinzani ghiliba' wanavyoendelea kumkaba bila mafanikio mfungaji bora wa CHADEMA kwa misimu yote mfululizo,Mhe Dkt Slaa tu machoni mwao, hapo ndipo makamanda wetu lukuki wasioku na majina sana masikioni mwao Wana-CCM hufanya MASHAMBULIZI YA KUFA MTU kila pembe ya nchi.

  Mabadiliko mbeeeeeeeeeeeeeeeleee kama tai bila kugeuka nyuma hata kwa theluthe moja tu.
   
 4. M

  MORIAH Senior Member

  #4
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 103
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Good one
   
 5. L

  Lwesye JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2012
  Joined: Sep 29, 2012
  Messages: 5,297
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hakuna kulala mpaka kieleweke
   
Loading...